Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda

Mahakama yaridhia kunyongwa aliyemuua Dereva Bodaboda

Mahakama ya Rufani Morogoro, imetupilia mbali rufani ya Justine Chamashine aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua dereva wa bodaboda, Joseph Frorence 'Msimbe'.

Uamuzi huo ulitolewa wiki iliyopita na Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma. Majaji wengine ni Augustine Mwarija na Othman Makungu.

Chamashine alikata rufani kupinga hatia na adhabu aliyopewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Majaji hao walisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili wamebaini hoja za rufani hazina mashiko
na Mahakama Kuu ilimhukumu mrufani kwa usahihi. Walibainisha miongoni mwa hoja za mrufani kupinga adhabu hiyo ilikuwa ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea kumhukumu kwa kutumia ushahidi wa kukutwa na vitu vya marehemu huku kukiwa hakuna ushahidi iwapo wakati Msimbe anauawa alikuwa akitumia pikipiki aliyokutwa nayo yeye.

Pia, alidai hakuna ushahidi wa malalamiko unaomuunganisha mrufani na pikipiki iliyoibwa kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kumuita Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuthibitisha umiliki wake.
Wakizichambua hoja hizo, Majaji walisema Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa sahihi kusema mrufani ndiye aliyemuua Msimbe. Aidha, walisema ushahidi unaonyesha mrufani alikamatwa na polisi akiwa anamiliki pikipiki hiyo ilithibitishwa na mmiliki wake halali ambaye alimkabidhi Msimbe kufanya biashara ya kubeba abiria Januari 6, mwaka 2017.

Ilielezwa Januari 9, mwaka 2017, Msimbe aliuawa na siku iliyofuata saa 7:30 mchana askari walimkamata mrufani akiwa anaendesha pikipiki hiyo, ndipo walipomfungulia shtaka la mauaji kwasababu alikutwa na pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Msimbe.​

Majaji hao walisema kwa ushahidi huo, hawaoni hitimisho lingine isipokuwa kama Jaji wa mahakama ya chini alivyoeleza kwamba mrufani alihusika na mauaji ya Msimbe na kuiba pikipiki.
Majaji hao walisema kutokana na hali hiyo wameona hoja za mrufani hazina mashiko, hivyo wanaitupa rufani kama ilivyokatwa. Chamashine alitenda kosa hilo, Januari 9, mwaka 2017, eneo la Kikwaraza, Kata ya Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro.
Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu.....

Circimstatial evidence became nevitable
 
Yan Leo pikipiki ipotee kesho ukutwe nayo wewe, mnataka kusema nin nyie huko juu mnaotetea, huyu ni muuaji,kama sio basi kahusika na anawajua wauaji awataje wakapumzike wote huko.

Nyumban kwetu sisi ni njian kuna siku usiku tunakula tukawatunasikia watu wanabishana hiv ila tunasikia kwa mbali yan tunakuja kushtuka yule boda anapiga kelele za msaada tunafika pale kashakatwa katwaapanga, kichwan, mabegan na mikononi, wezi wabayaa saaana
Unadhani aliyeua ni mpumbavu kiasi cha kuendesha pikipiki ya marehemu kesho yake?
 
Yan Leo pikipiki ipotee kesho ukutwe nayo wewe, mnataka kusema nin nyie huko juu mnaotetea, huyu ni muuaji,kama sio basi kahusika na anawajua wauaji awataje wakapumzike wote huko.

Nyumban kwetu sisi ni njian kuna siku usiku tunakula tukawatunasikia watu wanabishana hiv ila tunasikia kwa mbali yan tunakuja kushtuka yule boda anapiga kelele za msaada tunafika pale kashakatwa katwaapanga, kichwan, mabegan na mikononi, wezi wabayaa saaana
Pikipiki aibe leo kwa kumuua mtu halafu kesho atembee nayo mitaani ! Hii nayo imekaa sawa?, ni mwizi gani anaweza kufanya kosa la namna hiyo?
Si kwamba natetea , mimi ni mhanga wa ujambazi wa kikatili ambao umenisababishia ulemavu hadi leo hii, lakini pia namna watuhumiwa wanavyokamatwa inatakiwa iwe safi ili tufurahie hukumu,
 
Aliiipataje pikipiki ya marehemu ,masaa 24 baada ya kuwawa?
Kuna series of misfortunes zikikuandama unaweza jikuta umeingia kwenye matatizo makubwa kwa bahati mbaya , kuna uwezekano kuwa jamaa ni mnunuzi maarufu wa vitu vya mazabe, akaletewa pikipiki hiyo akanunua kwa bei chee bila kujua msala wake.
Piki piki mbali sana , simu ya kununua mitaani tu inaweza kukuletea msala kama huo na kwa mahakama zetu zinavyofanya kazi unaweza kunyongwa kweli
 
Halafu watu ni maajabu sana, unamwua mtu kwa ajiri ya kumpora pikipiki tu.
Toka hapo unaanza kuishi maisha ya wasiwasi tele.
Ndio maana wanahukumiwa adhabu kali
Sina shida na hukumu kama ni kweli aliyekamatwa ni muuaji halisi.
Hofu yangu ni kuwa mtuhumiwa anaweza akawa ametenda kosa la kununua mali ya wizi na sio mwizi mwenyewe, na kwa maelezo yanayotolewa kuna uwezekano sio aliyeuwa na kuiba pikipiki
 
Muuaji hawezi UA, akachukua pikipiki afu kesho aiendeshe maeneo hayo hayo
Hiyo ni common sense !! Bahati mbaya sana watanzania hatuna uwezo wa kutumia common sense , akili ya mwanzo kabisa ambayo mwanadamu kapewa bure kabisa bila ya kwenda darasani.
Unaona hata kwenye huu mjadala baadhi ya watu hawajaitumia common sense , wanahukumu tu .bila kuhoji
 
Hiyo ni common sense !! Bahati mbaya sana watanzania hatuna uwezo wa kutumia common sense , akili ya mwanzo kabisa ambayo mwanadamu kapewa bure kabisa bila ya kwenda darasani.
Unaona hata kwenye huu mjadala baadhi ya watu hawajaitumia common sense , wanahukumu tu .bila kuhoji
Matukio yote ya uporaji kitu kikiibiwa,hakiuzwi mtaa huo wala hakitatumika mtaa huo.

Huyu akaombe mapitio atachomoka
 
Back
Top Bottom