Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Habari iliyoko hapa ni kwamba amehukumiwa kunyongwa kwa kukutwa na pikipiki ambayo wanasema ni ya marehemu. Lakini pia kabla ya kusema pikipiki hiyo ameipata wapi, ni lazima kwanza wathibitishe kuwa pikipiki iliyokamatwa ndiyo hiyo aliyokuwa akiiendesha marehemu. Na hili linawezekana kwa kupata taarifa za umiliki kutoka TRA.
Na inaonekana hakuulizwa hilo swali la kuwa kaipata wapi hiyo pikipiki. Na sababu ni kwamba mahakama yenyewe Haika om na ushahidi kutoka TRA kuthibitisha umiliki.
Soma hapo chini…
“Walibainisha miongoni mwa hoja za mrufani kupinga adhabu hiyo ilikuwa ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea kumhukumu kwa kutumia ushahidi wa kukutwa na vitu vya marehemu huku kukiwa hakuna ushahidi iwapo wakati Msimbe anauawa alikuwa akitumia pikipiki aliyokutwa nayo yeye”
Mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya sheria lakini Katika shauri hilo kuna kesi mbili, ya kwanza ni mauaji ambayo ni kubwa na ya pili ni uporaji, kesi kubwa huwa inameza kesi ndogo.
Kesi ya huyo mhusika ilikuwa ni kesi ya mauaji, hivyo ninachokiona mimi ni kwamba alishindwa kujitetea jinsi alivyopata hiyo pikipiki ndio maana katiwa hatiani hata kama hakuhusika na hayo mauaji.