Mahakama yaruhusu Mkuu wa Wilaya kumpinga Rais Samia kumstaafisha kabla ya muda kisheria

Nimeisoma habari hiyo, jamaa anayo madai ya msingi. Mtumishi wa umma akitenguliwa kwenye hizo nafasi za u DC anapaswa kurejeshwa kwenye nafasi yake ya awali kwenye utumishi.

Sijui kama Rais alifahamu kuhusu hiyo barua ya katibu mkuu kiongozi au jamaa alijiongeza tu. Tena bahati mbaya nayeye KMK wa kipindi hicho alishaliwa kichwa, hayupo tena ikulu.
Dk Ndumbaro alikua mtu wa hovyo kabisa kukalia ile nafasi ya Katibu Mkuu Utumishi, afadhali AMENYAMAZISHWA
 
Hukumu ilitoka mwaka jana mwishoni kabisa, 30 Dec.

Sina taarifa, kwa sasa sipo huko. Ila huyo hana hiyo hela.

Mbeleko za JPM, kutokana na ukaribu na baba yake ndiyo ulimpa ujira. Akapata bichwa na kujiona Rais.

Huyu wamtulize kimya kimya tu.
Hivi Magufuli kweli alikuwa anakwenda kanisani kumuomba mungu?? au shetani dhambi zote hizo za kuweka ndugu zake kwenye kazi za serikali utafikiri nchi ilikuwa mali yake na ndugu zake na marafiki zake ni dhuluma kwa Watanzania na mungu amlaani yeye na ndugu zake wote alafu hao ndugu wakawa hawana aibu wakatumia madaraka kama mafisi msituni kweli ushenzi wao utaitesa Tanzania mda mrefu sana
 
Dungu ni nn
Dungu ni gari yenye bodi kubwa (SUV) kama Range Rover, Land Cruiser nk. Dungu ni neno la kihehe. Chris Lukosi anawashauri watanzania waache kununua magari madogo (hatchback na saloon) akiyaita ni vibakuli, wanunue madungu kwani yanauzwa bei chee tu, anayasafirisha kutoka Uingereza anakoishi.

Kazi ni kipimo cha utu.
 
Hawa ndio wale wakuu wa wilaya wapumbavu sana waliowekwa na Magufuli haswa kulikuwa na mmoja mshenzi pia alikuwa Kigamboni anaitwa Sara Msafiri sijui nae ameishia wapi alikuwa anapelekea watu wapekuzi wa madawa ya kulevya akitaka ardhi yako Kigamboni anakusingizia lika ushenzi raisi asiruhushe upumbavu wao afukuze makizi yote ya wakati wa Magufuli kwani walikuwa wanatumia madaraka vibaya sana
Sara si alileta ule ufisadi wa kigambani wa mafuta, kumbe nae anayake.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini wakati wa Magufuli Komanya Kitwala ameruhusiwa kufungua kesi na Mahakama, Ili kupinga kustaafishwa kwa lazima na Mkuu wa nchi, kwa manufaa ya Umma.
Kwa taarifa kamili soma kiambatisho Cha gazeti hapo chini.View attachment 2640476
View attachment 2640484
Kwa mujibu wa sheria za utumishi wa uma rais ndiye mamlaka kuu ya nidhamu na mdhibiti mkuu wa utumishi wa umma.

Rufaa ya utumishi iliyoamriwa na rais haiwezi pingwa popote.

Pole zake maana siasa ilimfanya asahau kesho leo hii anaomba hadi bia ya 2500!!
 
Mkuu! Rufaa iliyoamriwa na Rais bado inaweza kwenda Mahakamani kwa ajili ya kufanyiwa mapitio (Judicial review) endapo kama hatua (procedure) zilifuatwa katika kufikia maamuzi hayo.
 
Dk Ndumbaro alikua mtu wa hovyo kabisa kukalia ile nafasi ya Katibu Mkuu Utumishi, afadhali AMENYAMAZISHWA
Pale Utumishi tatizo si Katibu Mkuu, bali ni wale watendaji wa chini ambao hufanya kazi kwa niaba yake, yaani hata akibadilishwa Katibu Mkuu ni kazi bure, kuna Vijana pale wameaminiwa lakini ni wa hovyo sana, yaani wanajifanya wanajua tabia za Watumishi wote Tanzania, ndiyo hao humshauri vibaya Katibu Mkuu, Kuna siku nilitaka kumtukana kijana mmoja wa kisukuma pale, nikaishia kumtusi kimoyomoyo.
 
Hukumu ilitoka mwaka jana mwishoni kabisa, 30 Dec.

Sina taarifa, kwa sasa sipo huko. Ila huyo hana hiyo hela.

Mbeleko za JPM, kutokana na ukaribu na baba yake ndiyo ulimpa ujira. Akapata bichwa na kujiona Rais.

Huyu wamtulize kimya kimya tu.
JPM sijui angekuwa hai Hadi sasa ivi ingekuwaje, Bashite angekuwa waziri wa elimu, sabaya angekuwa RC Dar
 
Mkuu! Rufaa iliyoamriwa na Rais bado inaweza kwenda Mahakamani kwa ajili ya kufanyiwa mapitio (Judicial review) endapo kama haatua (procedure) zilifuatwa katika kufikia maamuzi hayo.
Kasome tena sheria ya utumishi wa umma. Uamuzi wa Rais ni wa mwisho.
 
Wakiondolewa kwenye V8 wanapagawa kabisa
Pambaf kabisa haya majitu yaliyozowea mserereko kitaa kwa moto kinoma hayana pa kukamata zinabaki yowe tu Mheshimiwa Raisi kama unasoma nikumbuke na Mimi mama Angu nna ka bachela[emoji112][emoji112][emoji112]
 
1685522054587.png

Mahakama Kuu Masjala Kuu imemruhusu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini (DC), Komanya Kitwala kufungua shauri kupinga uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumlazimisha kustaafu bila kumpa sababu.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lilian Mongela Mei 23, mwaka huu katika shauri la maombi lililofunguliwa na Kitwala dhidi ya Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Katika uamuzi huo, Jaji Mongela alimtaka Kitwala kufungua shauri hilo la mapitio ya mahakama la kupinga uamuzi huo wa Rais ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi huo. Siku 14 zinaisha Juni 5.

Kitwala aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya kuhakiki mali za Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoundwa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, aliteuliwa Julai 27, 2018 kuwa DC wa Tabora Mjini.

Kwa mujibu wa kiapo chake kilichounga mkono maombi hayo kabla ya uteuzi huo, alikuwa akifanya kazi PSSSF, akiwa Ofisa Sheria.

Hata hivyo, uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Juni 19, 2021 na nafasi yake kujazwa na Dk Yahya Nawanda.
Baada ya uteuzi wake wa U-DC kutenguliwa alimwandikia barua Katibu Mkuu Utumishi, akiomba amrejeshe katika ajira yake ya awali PSSF.

Hata hivyo, barua yake hiyo haikujibiwa mapema, lakini baadaye alipokea barua ya Katibu Mkuu Kiongozi ya Agosti 15, 2022 iliyomfahamisha Rais amemstaafisha kwa maslahi ya umma.

Hakukubaliana na uamuzi huo ndipo akafungua maombi ya ruhusa ya kufungua shauri la maombi ya mapitio ya Mahakama ili kupinga uamuzi huo wa Rais.

Jaji Mongela katika uamuzi wake baada ya kusikiliza hoja za pande zote na kurejea sheria na uamuzi wa kesi mbalimbali za mahakama hiyo na Mahakama ya Rufani, amekubaliana na hoja za wakili wa Kitwala, Jeremiah Mtobesya kwamba mwombaji amekidhi vigezo kustahiki kupewa ruhusa hiyo.

Alisema ni dhahiri mwombaji anaomba ruhusa kupinga uamuzi wa Rais unaomlazimisha kustaafu mapema, kwanza kwa kutumia kifungu cha sheria kisicho sahihi ambacho kinasababiaha usumbufu kwa mwombaji. Pia alisema jambo la pili linaloonekana katika kumbukumbu za shauri hilo ni kwamba hakupewa fursa ya kusikilizwa kabla ya kufikiwa kwa uamuzi na la tatu kwa kutokupewa sababu zote za uamuzi wa kumstaafisha kwa lazima.

"Kwa kuzingatia hoja zilizotolewa na mwombaji, zinazothibitisha kuwepo kesi ya kusikilizwa hususan kunyimwa haki ya kusikilizwa, ninaona kwamba maombi haya ni sahihi, yamekidhi matakwa ya kisheria kupewa ruhusa kufungua maombi hayo.

Katika shauri hilo, Kitwala alikuwa anaiomba mahakama imruhusu kufungua shauri la maombi ya Mapitio ya Mahakama, kupinga uamuzi wa Rais Samia wa Agosti 15, 2022 kumlazimisha kustaafu kabla ya muda wake kisheria.

Katika shauri hilo la mapitio atakalolifungua, Kitwala anataka kuiomba Mahakama hiyo iitishe na kisha kutengua na kutupilia mbali uamuzi huo wa Rais kwa kuwa amekwenda nje ya mamlaka yake kisheria dhidi ya kanuni ya haki asili na wa usumbufu kwake.

Pia anakusudia kuiomba mahakama hiyo imuamuru Katibu Mkuu, Utumishi amrejeshe katika ajira yake ya awali kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya, kulipwa madeni ya mishahara yake na mafao mengine kuanzia Juni 28, 2021 mpaka tarehe ya kurejeshwa katika ajira yake.

Vilevile anakusudia kuiomba mahakama hiyo kuiamuru bodi hiyo ya wadhamini wa PSSSF kumrejesha katika nafasi yake ya awali.

Awali, Serikali ilijaribu kumzuia Kitwala kupata ruhusa hiyo baada ya kuwasilisha pingamizi la awal, ikiiomba mahakama ilitupilie mbali shauri hilo la maombi ya ruhusa, lakini jitihada hizo ziligonga mwamba.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa njia ya maandishi na Kitwala aliwakilishwa na Wakili Mtobesya na wajibu maombi waliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Selina Kapange.

CREDIT: MWANANCHI
 
View attachment 2641172

KAZA BUTI UNAWEZA SHINDA INGAWA KWA SASA HATUNA BOLD JUDGES, TUNA SHYSTER JUDGES

Unahitaji lawyer mahiri na sijui kama kwa sasa tuna lawyer anayeweza ku handle case kama hiyo.
 
Attachments

Raha ya uhuru ndio hii, nani angethubutu hivyo mbele ya Jiwe?
 
Back
Top Bottom