Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
mahali ambapo wamwabuduo halisi wanaabudu. Yohana 4:23 imeandikwa, "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu". tafuta watu wanaomwabudu Mungu katika Roho na kweli jiunge nao, hao ndio wanaabudu na hawapotezi muda. kuabudu katiak Roho na Kweli sio tu kunyenyekea toka moyoni, ni pale Roho Mtakatifu anapohusika kwenye ibada zenu. kwanza uokoke, pili jiunge na waliookoka kama wewe, na kama kuimba imba katika uwepo wa Roho, kama kuabudu hivyo hivyo na kama ni kuhubiri ni kwa Roho Mtakatifu, yaani Roho Mtakatifu awe kiongozi sio tu kwenye maisha yako bali kweney abudu yako.Hapo mahali sahihi ambapo watu wote tunakubaliana kwamba hapa ndio sahihi ni wapi?
Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. duniani kuna umwengu wa mwili na ulimwengu wa Roho, Mungu yupo rohoni hayupo mwilini, hii inamaana kwamba, ili umpate lazima uende rohoni. na mashetani pia hivyo hivyo, ili uyapate yanapatikana rohoni, huo ndio ulimwengu wa roho, watu wapo tayari wamfuate shetani rohoni ila Mungu wasimfuate rohoni wakati Mungu anapatikana rohoni pia. shida ya watu wengi, madhehebu mengi ya kikristo, yanamwabudu Mungu kimwili, na hawatamwona Mungu kimwili bali kiroho, katika Roho Mtakatifu na katika kweli ya Mungu.