Mahakama yastukia utapeli wa Mchungaji, yaamuru arudishe milioni 15 alizotaka kumtapeli muumini wake kwa kusingizia zaka

Hapo mahali sahihi ambapo watu wote tunakubaliana kwamba hapa ndio sahihi ni wapi?
mahali ambapo wamwabuduo halisi wanaabudu. Yohana 4:23 imeandikwa, "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu". tafuta watu wanaomwabudu Mungu katika Roho na kweli jiunge nao, hao ndio wanaabudu na hawapotezi muda. kuabudu katiak Roho na Kweli sio tu kunyenyekea toka moyoni, ni pale Roho Mtakatifu anapohusika kwenye ibada zenu. kwanza uokoke, pili jiunge na waliookoka kama wewe, na kama kuimba imba katika uwepo wa Roho, kama kuabudu hivyo hivyo na kama ni kuhubiri ni kwa Roho Mtakatifu, yaani Roho Mtakatifu awe kiongozi sio tu kwenye maisha yako bali kweney abudu yako.

Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. duniani kuna umwengu wa mwili na ulimwengu wa Roho, Mungu yupo rohoni hayupo mwilini, hii inamaana kwamba, ili umpate lazima uende rohoni. na mashetani pia hivyo hivyo, ili uyapate yanapatikana rohoni, huo ndio ulimwengu wa roho, watu wapo tayari wamfuate shetani rohoni ila Mungu wasimfuate rohoni wakati Mungu anapatikana rohoni pia. shida ya watu wengi, madhehebu mengi ya kikristo, yanamwabudu Mungu kimwili, na hawatamwona Mungu kimwili bali kiroho, katika Roho Mtakatifu na katika kweli ya Mungu.
 
Ukristo biashara
 
Kuna watu ni wajinga sana kwenye hii nchi. Wacha waendelee tu kutapeliwa. Kirahisi tu nimpe mtu hela yangu kama fungu la 10!!!

Si bora hiyo hela nikawasaidie watu wenye mahitaji maalum!!
 
Analo kanisa na ndilo Neema analosali.
Ni kweli. Nijuavyo mimi kanisa analoabudu ni hilo la huyo Mchungaji. Mara nyingi utawasikia wakitaja kwamba wao wanaabudu kwa Mchungaji fulani ambaye anakuwa ndiye aliyeanzisha Ujenzi wa kanisa hilo. Jambo hili huleta utata mara Mchungaji husika anapopata faradhi na kufa. Inafikia wakati Mama Mchungaji anarithi hilo kanisa na mifano ipo mingi hadi huko Nigeria. Wengi huishia kujiuliza je, kanisa ni la waumini kwani wao ndio walichangia katika kujenga au ni mali ya Mchungaji?
 
Kimsingi mtu hawezi toa sadaka kwa hiari yake halafu tena akaidai mahakamani!

Mchungaji alipata wapi ujasiri mpaka mahakamani!
Ona sasa! Kampoteza kondoo alienona na lazima kuna kondoo wengi tu wamepata shock huenda atawapoteza pia
 
Kuna kanisa moja hivi hapa arusha nilitonywa na wajanja wa mjini,hapo kila ukiingia hutoki kapa! Pastor wetu ni kibopa flani kwenye taasisi moja ya serikali yenye ukwasi mrefu,hapo church kuna ibada inayoanza saa 3 hadi 5 asubuhi,halafu kuna break,tunaenda hotelini tunakula na kunywa tunachotaka kwa bill ya pastor,baadaye saa saba tunarudi church session nyingine ambayo ni ya online,tunatoka saa tisa au kumi jioni,hapo kila muumini anakamatishwa 10,000 ya nauli kurudia home, na pastor ametuambia kabisa,kama kuna mtu ana changamoto yoyote inayohitaji fedha tusisite kumwambia,kila mwisho wa ibada utakuta waumini kama wote wamejibanza kwenye vikona wanamsubiria pastor wampige kucha,siku kadhaa sijaenda hapo,ni uvivu wangu tu,ila hapo nipo nipo sana.karibuni
 
Ni kama tu ile dini inayoua watu kila siku kwa kujivika mabomu na kujilipua.
hata hueleweki kabisa
pitia kwanza aya hii


Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na watawa(wa kikristo na kiyahudi) wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia [watu] njia ya Allaah. Na wale wanaorundika [hazina za] dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. Siku [mali zao] zitakapopashwa katika Moto wa Jahannam, kisha kwa hayo vikachomwa Moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao [huku wakiambiwa]: “Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika.” (09:34-35)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…