Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mahakama iliyosikiliza hiyo kesi haikupaswa kusikiliza kesi inayozidi madai ya kiwango cha million 300 kisheria au haujapitia bandiko vyema mkuu !?
Nimesoma bandiko, sasa kama Mahakama iliyosikiliza hiyo kesi haikupaswa kufanya hivyo tena mpaka na hukumu ikatoa, hapo kosa ni la nani? Kwanini kina Mwana FA watishiwe kushikwa mali zao? Hapo ndipo nilipotaka ufafanuzi wa kina.
 
Mahakama Kuu, Dar es Salaam, imetengua hukumu iliyoiamuru kampuni ya simu za mkononi MIC (T) Limited, maarufu Tigo, kuwalipa wanamuziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma (MwanaFA) na Ambwene Yesaya (AY) Sh 2.1 bilioni kwa kukiuka sheria za hatimiliki.

Jaji Joacquine De-Mello amebatilisha uamuzi huo baada ya kukubaliana na rufaa ya Tigo kuwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Uamuzi huo unakuja huku tayari wanamuziki hao maarufu wa muziki wa Bongo Fleva wakiwa wametia fedha hizo kibindoni baada ya vita kali ya kisheria kati yao na Tigo ambayo ilipinga kwa nguvu zote kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo bila mafanikio.

Kampuni hiyo ililazimika kulipa pesa hizo baada ya wasanii hao kuikaba kooni kwa kukamata akaunti zake baada ya kupata amri ya Mahakama ya Ilala, kufuatia maombi yao ya utekelezaji wa hukumu hiyo baada ya kampuni hiyo kuchelewa kulipa.

Wakati ikiwalipa fedha hizo, kampuni hiyo tayari ilikuwa imeshafungua maombi mahakama, ikiomba kibali cha kukata rufaa nje ya muda na baada ya kufanikiwa kupata kibali hicho ndipo ikakata rufaa hiyo.

Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo ameliambia Mwananchi kuwa atawaandikia barua wasanii hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa na mteja wake.

“Kama hawatafanya hivyo, tutafungua maombi ya utekelezaji ili tupate amri ya mahakama ya kukamata mali zao,” alisema wakili Mbwambo na kuongeza, “ikilazimu tutaiomba mahakama pia iamuru wafungwe.”

Uamuzi huu wa mahakama unaweza kusababisha vita mpya ya kisheria kati ya wanamuziki hao wenye umaarufu mkubwa hapa nchini na kampuni hiyo ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa tatu zinazotoa huduma za simu za mkononi nchini.

Hukumu ilivyokuwa

Hukumu na amri ya kuwalipa MwanaFA na AY ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan, Aprili 11, 2016, kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya Tigo.

Hakimu Hassan aliridhika kuwa Tigo ilikiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa kutumia kibiashara nyimbo zao ambazo ni Usije Mjini na Dakika Moja kama miito ya simu bila ridhaa wala makubaliano nao.

Tigo haikuridhika na uamuzi huo na ilikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo.

Kampuni hiyo ya simu iliwasilisha sababu 11 za kupinga hukumu dhidi yake, lakini Jaji De-Mello, ametengua hukumu hiyo kwa kutumia sababu moja tu; kwamba mahakama hiyo haikuwa na mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Jaji De-Mello amekubaliana na hoja za Tigo iliyowakilishwa na wakili Rosan Mbwambo kuwa kiwango cha fidia cha Sh4.3 bilioni waliyokuwa wakiidai wasanii hao ni kikubwa kuliko uwezo wa kisheria wa mahakama hiyo.

Mahakama za wilaya zina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya madai yanayohusisha fedha kwa kiwango kisichozidi Sh300 milioni tu.

Katika hukumu hiyo ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, Jaji De-Mello Amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 40 (1) (b) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu, mahakama hizo zinapewa mamlaka yenye ukomo na hazipaswi kwenda zaidi ya mamlaka hayo.

Jaji De-Mello alisema kuwa kifungu cha 4 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kinatoa mamlaka ya masuala ya migogoro ya hakimiliki kwa mahakama za wilaya, lakini kwa kuzingatia ukomo mamlaka ya mahakama hizo kwa kiwango cha fedha katika shauri husika.

Pia alisema kwa kuangalia hoja na asili ya madai ya kesi hiyo, hakuna shaka kuwa huo ni mgogoro wa kibiashara ambao mahakama hiyo ya wilaya ilipaswa kuzingatia sheria zinazohusika kubaini kuwa haina mamlaka na kutoa maoni sawia.

Kesi ya msingi

Katika kesi ya msingi namba 17 ya mwaka 2012, wasanii hao waliiomba mahakama hiyo itamke kuwa MIC iliingilia haki zao kwa kutumia kibiashara kazi zao za kimuziki walizozitunga kwa pamoja na kuzisajili katika Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (Cosota), Septemba 24,2010.

Vilevile walikuwa wakiomba malipo ya fidia ya Sh4.3, Sh50 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya jumla na Sh4.32 bilioni zikiwa ni hasara maalumu, pamoja na riba ya asilimia 20.

Tigo katika utetezi wake kupitia kwa mkuu wa kitengo cha burudani na miradi David Zakaria, alidai kuwa MIC ilipelekewa nyimbo hizo na kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, waliyoingia nayo mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo na kwamba ndio inapaswa kuwalipa wasanii husika.

Hakimu Hassan katika uamuzi wake alikubaliana na madai na hoja za wasanii hao kuwa mdaiwa alitumia kazi zao bila ridhaa yao na kwamba alijipatia mapato, huku wasanii hao wakipata hasara kwa kutofanya biashara kwa kazi zao hizo. Hata hivyo, hakimu huyo alishusha kiwango cha fidia walichodai hadi Sh2.1 bilioni.
Ukisikia jela inakuita ghafla ndio hii
 
Upuuumbaaavuuuu....😲😲🤣🤣

Sasa ni kwanini WASIKATE rufaa kabla ya kuwalipa hizo PESA?!!

Huku mitaani kunatokea kesi za nyumba....mdai anashinda kesi MAHAKAMANI...na bado inachukua MUDA na MIAKA kupewa haki yake na MDAIWA...simply kwa kuwa MDAIWA amekata RUFAA MAHAKAMANI.....
 
Upuuumbaaavuuuu....[emoji44][emoji44][emoji1787][emoji1787]

Sasa ni kwanini WASIKATE rufaa kabla ya kuwalipa hizo PESA?!!

Huku mitaani kunatokea kesi za nyumba....mdai anashinda kesi MAHAKAMANI...na bado inachukua MUDA na MIAKA kupewa haki yake na MDAIWA...simply kwa kuwa MDAIWA amekata RUFAA MAHAKAMANI.....
Mbona article inajieleza vizuri ...Mwanasheria anasema wakati Wana hangaika na kukata rufaa mahama ikawa imetoa agizo la Tigo kuwalipa walalamikaji
 
Hawa tigo nao....bil2 tu $1million?? ndo wanazungushana Hivi court

Kampuni kubwa kama tigo?
Tena nyimbo walizitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu mkuu hapo issue haijakaa katika pesa tu peke yake.. issue imekaa katika pesa na Uchafuzi wa kuichafua taswira ya kampuni yaani Tigo wanaona kabisa kuwa wamechafuliwa na kama hukumu haikuwa ni ya haki kweli... Basi sote hapa hatuwezi kupinga kuwa tigo wamechafuliwa taswira yao kibiashara now wanaonekana Ni matapeli
 
Back
Top Bottom