Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Kampuni huwa zinashtakiwa...kama TUSHTAKIWAVYO sisi....

Yaani umnyonge mtu haki yake...utumie JASHO LAKE...ufaidike kwa CALLER TUNE ZAKE....aende mahakamani kudai CHAKE useme anakuchafua?!!!

Sasa mahakama ziko kwa AJILI GANI?!!

Kama hutaki kuchafuliwa na KUCHAFUKA biashara zako basi USIINGILIE HAKI ZA WENGINE....
 
MIC wamefeli,hawakutakiwa kulipa kwanza wakati wameenda kukata rufaa higher court..

MIC huko ndani ni lazima kulikua na watu wamekula njama na hawa viazi akina AY walipwe fasta wagawane...

MIC hawakutakiwa kulipa chochote kabisa maana rufaa was on!

Plus,mtu fala ni mtu sio smart kwenye kitu fulani ila anaweza kua smart kwenye kitu kingine,nothing wrong with fala...

Na pia sio lazima niwapende FA na AY,silazimishwi kuwapenda...I can as well hate them!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Wyatt him self
 
Kampuni huwa zinashtakiwa...kama TUSHTAKIWAVYO sisi....

Yaani umnyonge mtu haki yake...utumie JASHO LAKE...ufaidike kwa CALLER TUNE ZAKE....aende mahakamani kudai CHAKE useme anakuchafua?!!!

Sasa mahakama ziko kwa AJILI GANI?!!

Kama hutaki kuchafuliwa na KUCHAFUKA biashara zako basi USIINGILIE HAKI ZA WENGINE....
Wajua haya makampuni huwa Yana nunua nyimbo kwa makampuni ambayo Ni dalali was kuuza hizo nyimbo kwa wasanii na kampuni hizo zipo kisheria na wasanii husika ndio huwa wanapeleka hizo nyimbo katika hayo makampuni kwa lengo la kufanya nahiyo kampuni biashara
 
Wajua haya makampuni huwa Yana nunua nyimbo kwa makampuni ambayo Ni dalali was kuuza hizo nyimbo kwa wasanii na kampuni hizo zipo kisheria na wasanii husika ndio huwa wanapeleka hizo nyimbo katika hayo makampuni kwa lengo la kufanya nahiyo kampuni biashara
Sure....

Ila akina mh.FA walilalamika kuwa hakukuwa na mkataba baina yao na hiyo kampuni iliyouza CALLER TUNER zao kwa kampuni inayolalamikiwa....
 
Mahakama Kuu, Dar es Salaam, imetengua hukumu iliyoiamuru kampuni ya simu za mkononi MIC (T) Limited, maarufu Tigo, kuwalipa wanamuziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma (MwanaFA) na Ambwene Yesaya (AY) Sh 2.1 bilioni kwa kukiuka sheria za hatimiliki.

Jaji Joacquine De-Mello amebatilisha uamuzi huo baada ya kukubaliana na rufaa ya Tigo kuwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Uamuzi huo unakuja huku tayari wanamuziki hao maarufu wa muziki wa Bongo Fleva wakiwa wametia fedha hizo kibindoni baada ya vita kali ya kisheria kati yao na Tigo ambayo ilipinga kwa nguvu zote kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo bila mafanikio.

Kampuni hiyo ililazimika kulipa pesa hizo baada ya wasanii hao kuikaba kooni kwa kukamata akaunti zake baada ya kupata amri ya Mahakama ya Ilala, kufuatia maombi yao ya utekelezaji wa hukumu hiyo baada ya kampuni hiyo kuchelewa kulipa.

Wakati ikiwalipa fedha hizo, kampuni hiyo tayari ilikuwa imeshafungua maombi mahakama, ikiomba kibali cha kukata rufaa nje ya muda na baada ya kufanikiwa kupata kibali hicho ndipo ikakata rufaa hiyo.

Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo ameliambia Mwananchi kuwa atawaandikia barua wasanii hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa na mteja wake.

“Kama hawatafanya hivyo, tutafungua maombi ya utekelezaji ili tupate amri ya mahakama ya kukamata mali zao,” alisema wakili Mbwambo na kuongeza, “ikilazimu tutaiomba mahakama pia iamuru wafungwe.”

Uamuzi huu wa mahakama unaweza kusababisha vita mpya ya kisheria kati ya wanamuziki hao wenye umaarufu mkubwa hapa nchini na kampuni hiyo ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa tatu zinazotoa huduma za simu za mkononi nchini.

Hukumu ilivyokuwa

Hukumu na amri ya kuwalipa MwanaFA na AY ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan, Aprili 11, 2016, kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya Tigo.

Hakimu Hassan aliridhika kuwa Tigo ilikiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa kutumia kibiashara nyimbo zao ambazo ni Usije Mjini na Dakika Moja kama miito ya simu bila ridhaa wala makubaliano nao.

Tigo haikuridhika na uamuzi huo na ilikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo.

Kampuni hiyo ya simu iliwasilisha sababu 11 za kupinga hukumu dhidi yake, lakini Jaji De-Mello, ametengua hukumu hiyo kwa kutumia sababu moja tu; kwamba mahakama hiyo haikuwa na mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Jaji De-Mello amekubaliana na hoja za Tigo iliyowakilishwa na wakili Rosan Mbwambo kuwa kiwango cha fidia cha Sh4.3 bilioni waliyokuwa wakiidai wasanii hao ni kikubwa kuliko uwezo wa kisheria wa mahakama hiyo.

Mahakama za wilaya zina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya madai yanayohusisha fedha kwa kiwango kisichozidi Sh300 milioni tu.

Katika hukumu hiyo ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, Jaji De-Mello Amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 40 (1) (b) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu, mahakama hizo zinapewa mamlaka yenye ukomo na hazipaswi kwenda zaidi ya mamlaka hayo.

Jaji De-Mello alisema kuwa kifungu cha 4 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kinatoa mamlaka ya masuala ya migogoro ya hakimiliki kwa mahakama za wilaya, lakini kwa kuzingatia ukomo mamlaka ya mahakama hizo kwa kiwango cha fedha katika shauri husika.

Pia alisema kwa kuangalia hoja na asili ya madai ya kesi hiyo, hakuna shaka kuwa huo ni mgogoro wa kibiashara ambao mahakama hiyo ya wilaya ilipaswa kuzingatia sheria zinazohusika kubaini kuwa haina mamlaka na kutoa maoni sawia.

Kesi ya msingi

Katika kesi ya msingi namba 17 ya mwaka 2012, wasanii hao waliiomba mahakama hiyo itamke kuwa MIC iliingilia haki zao kwa kutumia kibiashara kazi zao za kimuziki walizozitunga kwa pamoja na kuzisajili katika Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (Cosota), Septemba 24,2010.

Vilevile walikuwa wakiomba malipo ya fidia ya Sh4.3, Sh50 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya jumla na Sh4.32 bilioni zikiwa ni hasara maalumu, pamoja na riba ya asilimia 20.

Tigo katika utetezi wake kupitia kwa mkuu wa kitengo cha burudani na miradi David Zakaria, alidai kuwa MIC ilipelekewa nyimbo hizo na kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, waliyoingia nayo mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo na kwamba ndio inapaswa kuwalipa wasanii husika.

Hakimu Hassan katika uamuzi wake alikubaliana na madai na hoja za wasanii hao kuwa mdaiwa alitumia kazi zao bila ridhaa yao na kwamba alijipatia mapato, huku wasanii hao wakipata hasara kwa kutofanya biashara kwa kazi zao hizo. Hata hivyo, hakimu huyo alishusha kiwango cha fidia walichodai hadi Sh2.1 bilioni.
Duh
 
Back
Top Bottom