Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mimi nilishauri tangu mwanzo wa kesi kuwa hizo pesa ni nyingi sana....wangekula milioni mia kila mmoja wapite hivi.

Ila hata hivyo kwa huo muda ulivyopita hizo pesa watazikuta wapi?.
 
Najaribu kufikiria hivi;

NI KIASI GANI HAYA MAKAMPUNI YA SIMU HUPATA hata kule kuwachaji watumiaji wa mitandao yao kwa kuwaingizia hizo CALLER TUNE bila ya ruhusa(consent) ya mtumiaji?!!!

Halafu CALLER TUNE hizo wamezipata na wanaendelea kuzitumia bila ya KUWALIPA WENYE HATI MILIKI ZAO?!!!

Huu ni WIZI....
Huu ni UNYONYAJI...
Huu ni UKANDAMIZAJI...
Huku ni kutaka kuitia nchi na wananchi UMASKINI.....
 
Sawa ..ila deep inside kuna ka wivu flan kwa kina FA kwamba ya wapate wao hzo pesa vijana wa kibongo tunajuana.mwenzao akipata kiroho kinaruka hiv..mbaya snaa...yaan kiufup hauhitaj kuwa upande wa tigo hata kama wamekosea
Ahaghh aghh sasa huko Ni kulazimishana kihisia boss huo Ni ukoloni mambo leo

Sio lazima kile unacho kipenda wewe ninacho kipenda mie Basi mtu mwingine nae akipende vivyo hivyo ' Tigo Ni kampuni Ay na FA ni wasanii kwanamna moja ama nyingine kampuni ya Tigo na hao wasanii wote Ni lazima watakuwa na mashabiki zao kwa sababu wote kwa pamoja Huduma wanazo zitoa zina gusa maisha ya watanzania directly

So kwa mantiki hiyo Tigo hawawezi kukosa mashabiki na kina AY na FA Hawawezi kukosa mashabiki pia

Kutaka watu wote washabikie upande Mmoja tu As if wote tuna moyo Mmoja unatoa tafasiri 1 ya kichocheo cha hisia huo sasa Ni ubinafsi na kutaka kuchaguliana maamuzi
 
Kusema mliletewa kazi na Cellulant bila ufhibitisho kuwa wanamiliki kazi hizo ni sawa na kununua gari ya wizi halafu uje useme ulikuwa hujui.

Bado utawajibika kulilipia gari hilo kisha uanze kumtafuta aliye kutapeli (Cellulant). Hao mahakama ya wilaya ndio walipe hizo fedha kwa kusikiliza kesi wasio na uwezo nayo, period.
 
Kazi wanayo

Waweza kukuta huyo hakimu aliyepitisha hiyo hukumu Alifanya hivyo ili nayeye apige mpunga. Sasa mpunga unakwenda kuwatokea puani [emoji849][emoji849]
Watazitapika in jiwe voice
 
Huyo Hakimu ndiye aliyekiuka sheria na huku akijua ni kosa, akamatwe yeye na afungwe ili iwe fundisho.

Hao wengine wana kosa gani wakati wamepewa haki mahakamani?
Exactly my point, aliyefanya kosa ni hakimu na mahakama yake, akamatwe na afungwe kwa kukiuka sheria, mwanaFa kapeleka malalamiko na wakamsikiliza, yeye MwanaFa agomee kwamba wasisikilize?
 
Back
Top Bottom