Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Nimeona Kama Tigo Wana hoja ya msingi mwanasheria wao anasema kwamba wao walipelekewa hizo nyimbo na kampuni ya Celullant LTD ambayo kimsingi Ni Kama dalali wa kuuza hizo nyimbo za wasanii kwa makampuni ya simu nchini .so kimsingi Mwanasheria wa Tigo anadai kwamba kampuni ambayo inapaswa kushtakiwa Ni hiyo cuz wao walimalizana na kampuni hiyo kisheria

Ngoja kwanza tuone hili saga litakavyo kwisha
mkuu ukimkamata mtu kauziwa gari lako kwa wizi utamtafuta aliyemuuzia ukamdai au utamdai yule uliyemkamata na gari yako
 
mkuu ukimkamata mtu kauziwa gari lako kwa wizi utamtafuta aliyemuuzia ukamdai au utamdai yule uliyemkamata na gari yako
Nitamtafuta niliyemkamata na gari ... Then what if kukiwa na uthibitisho wa kisheria kwamba Tigo walinunua kisheria hizo nyimbo toka katika hiyo kampuni na kampuni hiyo iliuziwa kisheria hizo nyimbo na wasanii husika !??
 
Ndio tunajua umefurah kina FA kuporwa pesa zao si ndo vijana wa bongo mlivyo hampend mafanikio ya wenzenu.wivu mbaya sana aisee
Tanzania sasa hivi kila mtu anajipambania ajuavyo. Ndio maana leo FA anakula mezani pa wauaji.

Kuna siku jamaa fulani Twitter alimwambia AY, Kaka naomba unisaidie hata 2M ninunue bodaboda hata kwa mkataba nitakurudishia.

Akamjibu kwa kuandika" Download hapa: Milioni2.com.

Tafsiri yake ni kwamba, celebrities siyo ndugu yako, Jali maisha yako.
 
-Hyo cellulant Tanzania ipo na inafanya Kaz kwasasa?

-mahakama inawajibika wap ikikosea kutoa haki?

-kama ndivyo sheria za kimahakama zilivyo basi hukumu ilikosa weledi wa kutafsir sheria na kampuni za kusikiliza na kuamua shauri.

- Kama ilkua ndo Ile inshu za zile aisee hii inshu ikitiki basi utakula miatatu Sasa ugumu inakuja hapa unazirudishaje jamaa wakishinda rufaa waliokata?

Lile tangazo la tunalongalonga nawatu wa #### bana, tunalongalonga sijui Kama bado lipo kwenye kumbukumbu za Hawa jamaa
 
Mahakama kuu imekubali rufaa ya kampuni ya Tigo na kutengua hukumu ya awali iliyowataka Tigo wawalipe Mh Mwinjuma aka mwanaFA na Yesaya Ambwene kiasi cha tsh 2.1 bilioni.

Mahakama kuu imekubaliana na Tigo kwamba mahakama ya Ilala haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Wakili wa mwanaFA ni Dr Albert Msando.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kusema mliletewa kazi na Cellulant bila ufhibitisho kuwa wanamiliki kazi hizo ni sawa na kununua gari ya wizi halafu uje useme ulikuwa hujui. Bado utawajibika kulilipia gari hilo kisha uanze kumtafuta aliye kutapeli (Cellulant). Hao mahakama ya wilaya ndio walipe hizo fedha kwa kusikiliza kesi wasio na uwezo nayo, period.
Huo mfano sidhani kama ni relevant mkuu...

Hivi kama Duka limesajiliwa kwa ajili ya kuuza TV,kisha mimi nikauziwa TV ya wizi kwenye hilo duka halali..ni mimi nitashtakiwa? na kuna remedy yeyote ya kulipa,je ni mimi ndo nitatakiwa kulipa?
Je mimi kama mteja nina wajibu wa kujiridhisha kuwa mali ninayouziwa kwenye duka lililosajilwa kama ni ya wizi au la zaidi ya kudai risiti?
Naona kama wako ni kwa mali mlizouziana kiholela huko mitaani.
 
Kazi wanayo

Waweza kukuta huyo hakimu aliyepitisha hiyo hukumu Alifanya hivyo ili nayeye apige mpunga. Sasa mpunga unakwenda kuwatokea puani [emoji849][emoji849]
Ulitegemea msando tapeli ashinde kesi bila kuhonga?hana historia ya kushinda kesi bila rushwa sasa mgao unamtokea puani chawa wa ccm.....yani lazima degedege limpate halafu mama Di melo hajui kuremba kesi wala kula rushwa yao
 
Kwenye hii kesi kulikua na janjajanja pamoja na vitisho vingi sana.
Msando ni bushlawyer tunamjua,hajawahi shinda kesi bila kuhonga....alikua mwanasheria wa exim bank arusha akawa anakula pesa za washtakiwa tu exim wakasanuka na kumtimulia mbali....baada ya kumtimua wakashinda kesi na wafanyakazi wezi wakahukumiwa miaka 30
 
Mwana FA hawezi kufanya huo uchizi hapo tigo wahesabu maumivu
 
Sasa hapo hasara itakuwa Kwa hao vijana,maana waliopewa mgao kama mawakili na wadau hawawawezi kurudisha pesa.Hapo mwana fa na Ay inabidi wahangaike wenyewe ikiwemo kuwalipa mawakili upya.Nilichogundua mawakili wengi ni watoto WA mjini
Si ndo hapo sasa...kwa sababu kesi kama ina wakili ina maana walianza kuandika "Demand note" kwenda Tigo na hiyo huonyesha kiasi ambacho watamuomba wanayetaka kumshtaki kiasi anachotakiwa kulipa kwa ukiukaji wa haki aliofanya au la watu waende Mahakamani.

Sasa huwezi kuniambia Mawakili wasishtuke,hakimu asishtuke ishu ndogo ya Pecuniary Jurisdiction kwenye kesi inayohusisha Billions of money?

Hapa kuna mchezo hapa...nahisi watoto wa mjini washachukua chao wanawaachia saga vijana...hata hakimu huwenda yumo humu.
 
Back
Top Bottom