tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,863
- 19,626
Mbwa kala mbwaAiseeee.... watu washanunua ma range na ma land rover,sa itakuwaje? Kwenye betting hii inaitwaje wakamalia?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbwa kala mbwaAiseeee.... watu washanunua ma range na ma land rover,sa itakuwaje? Kwenye betting hii inaitwaje wakamalia?
Msando aliwahi kukamata Ac za tigo kabla ya rufaa,hii case kuna rushwa na mikono ya wakubwa...hakuna case ambayo haina rufaa tena kwenye hukumu ya mwanzo tuUpuuumbaaavuuuu....[emoji44][emoji44][emoji1787][emoji1787]
Sasa ni kwanini WASIKATE rufaa kabla ya kuwalipa hizo PESA?!!
Huku mitaani kunatokea kesi za nyumba....mdai anashinda kesi MAHAKAMANI...na bado inachukua MUDA na MIAKA kupewa haki yake na MDAIWA...simply kwa kuwa MDAIWA amekata RUFAA MAHAKAMANI.....
Unatujazia pumba tuNajaribu kufikiria hivi;
NI KIASI GANI HAYA MAKAMPUNI YA SIMU HUPATA hata kule kuwachaji watumiaji wa mitandao yao kwa kuwaingizia hizo CALLER TUNE bila ya ruhusa(consent) ya mtumiaji?!!!
Halafu CALLER TUNE hizo wamezipata na wanaendelea kuzitumia bila ya KUWALIPA WENYE HATI MILIKI ZAO?!!!
Huu ni WIZI....
Huu ni UNYONYAJI...
Huu ni UKANDAMIZAJI...
Huku ni kutaka kuitia nchi na wananchi UMASKINI.....
Sheria ni msumeno bwashee!Tigo wanajidhalilisha tu, hawaoni aibu. Kwani hawakutumia kweli hizo nyimbo?
Au sababu wamezoea dhulumu wasanii?
Hapo Msando hana shida...hili alilifahamu litakuja...nawaonea huruma vijana waloingizwa mjini maana watalipa peke yao...migao mingine hairudi.Ulitegemea msando tapeli ashinde kesi bila kuhonga?hana historia ya kushinda kesi bila rushwa sasa mgao unamtokea puani chawa wa ccm.....yani lazima degedege limpate halafu mama DI melo hajui kuremba kesi wala kula rushwa yao
...nimezijaza mfukoni mwako?!!Unatujazia pumba tu
Hakimu hashitakiwi hata siku moja kwa maamuzi anoyatoa,hata yawe mabovu kiasi gani,labda kama unaweza kuprove rushwa.Exactly my point, aliyefanya kosa ni hakimu na mahakama yake, akamatwe na afungwe kwa kukiuka sheria, mwanaFa kapeleka malalamiko na wakamsikiliza, yeye MwanaFa agomee kwamba wasisikilize?
Kwanini hao TIGO wasingekwenda MAHAKAMANI kuzuia kukamatwa mali zao?!!!Msando aliwahi kukamata Ac za tigo kabla ya rufaa,hii case kuna rushwa na mikono ya wakubwa...hakuna case ambayo haina rufaa tena kwenye hukumu ya mwanzo tu
Dah, na jamaa walishapiga hela zote kwa safari za kuizunguka dunia kila wiki, kila mwezi, kila mwaka😀Mahakama Kuu, Dar es Salaam, imetengua hukumu iliyoiamuru kampuni ya simu za mkononi MIC (T) Limited, maarufu Tigo, kuwalipa wanamuziki wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma (MwanaFA) na Ambwene Yesaya (AY) Sh 2.1 bilioni kwa kukiuka sheria za hatimiliki.
Jaji Joacquine De-Mello amebatilisha uamuzi huo baada ya kukubaliana na rufaa ya Tigo kuwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.
Uamuzi huo unakuja huku tayari wanamuziki hao maarufu wa muziki wa Bongo Fleva wakiwa wametia fedha hizo kibindoni baada ya vita kali ya kisheria kati yao na Tigo ambayo ilipinga kwa nguvu zote kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo bila mafanikio.
Kampuni hiyo ililazimika kulipa pesa hizo baada ya wasanii hao kuikaba kooni kwa kukamata akaunti zake baada ya kupata amri ya Mahakama ya Ilala, kufuatia maombi yao ya utekelezaji wa hukumu hiyo baada ya kampuni hiyo kuchelewa kulipa.
Wakati ikiwalipa fedha hizo, kampuni hiyo tayari ilikuwa imeshafungua maombi mahakama, ikiomba kibali cha kukata rufaa nje ya muda na baada ya kufanikiwa kupata kibali hicho ndipo ikakata rufaa hiyo.
Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo ameliambia Mwananchi kuwa atawaandikia barua wasanii hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa na mteja wake.
“Kama hawatafanya hivyo, tutafungua maombi ya utekelezaji ili tupate amri ya mahakama ya kukamata mali zao,” alisema wakili Mbwambo na kuongeza, “ikilazimu tutaiomba mahakama pia iamuru wafungwe.”
Uamuzi huu wa mahakama unaweza kusababisha vita mpya ya kisheria kati ya wanamuziki hao wenye umaarufu mkubwa hapa nchini na kampuni hiyo ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa tatu zinazotoa huduma za simu za mkononi nchini.
Hukumu ilivyokuwa
Hukumu na amri ya kuwalipa MwanaFA na AY ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juma Hassan, Aprili 11, 2016, kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya Tigo.
Hakimu Hassan aliridhika kuwa Tigo ilikiuka Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa kutumia kibiashara nyimbo zao ambazo ni Usije Mjini na Dakika Moja kama miito ya simu bila ridhaa wala makubaliano nao.
Tigo haikuridhika na uamuzi huo na ilikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo.
Kampuni hiyo ya simu iliwasilisha sababu 11 za kupinga hukumu dhidi yake, lakini Jaji De-Mello, ametengua hukumu hiyo kwa kutumia sababu moja tu; kwamba mahakama hiyo haikuwa na mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.
Jaji De-Mello amekubaliana na hoja za Tigo iliyowakilishwa na wakili Rosan Mbwambo kuwa kiwango cha fidia cha Sh4.3 bilioni waliyokuwa wakiidai wasanii hao ni kikubwa kuliko uwezo wa kisheria wa mahakama hiyo.
Mahakama za wilaya zina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya madai yanayohusisha fedha kwa kiwango kisichozidi Sh300 milioni tu.
Katika hukumu hiyo ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, Jaji De-Mello Amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 40 (1) (b) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu, mahakama hizo zinapewa mamlaka yenye ukomo na hazipaswi kwenda zaidi ya mamlaka hayo.
Jaji De-Mello alisema kuwa kifungu cha 4 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kinatoa mamlaka ya masuala ya migogoro ya hakimiliki kwa mahakama za wilaya, lakini kwa kuzingatia ukomo mamlaka ya mahakama hizo kwa kiwango cha fedha katika shauri husika.
Pia alisema kwa kuangalia hoja na asili ya madai ya kesi hiyo, hakuna shaka kuwa huo ni mgogoro wa kibiashara ambao mahakama hiyo ya wilaya ilipaswa kuzingatia sheria zinazohusika kubaini kuwa haina mamlaka na kutoa maoni sawia.
Kesi ya msingi
Katika kesi ya msingi namba 17 ya mwaka 2012, wasanii hao waliiomba mahakama hiyo itamke kuwa MIC iliingilia haki zao kwa kutumia kibiashara kazi zao za kimuziki walizozitunga kwa pamoja na kuzisajili katika Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (Cosota), Septemba 24,2010.
Vilevile walikuwa wakiomba malipo ya fidia ya Sh4.3, Sh50 milioni zikiwa ni fidia ya hasara ya jumla na Sh4.32 bilioni zikiwa ni hasara maalumu, pamoja na riba ya asilimia 20.
Tigo katika utetezi wake kupitia kwa mkuu wa kitengo cha burudani na miradi David Zakaria, alidai kuwa MIC ilipelekewa nyimbo hizo na kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, waliyoingia nayo mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo na kwamba ndio inapaswa kuwalipa wasanii husika.
Hakimu Hassan katika uamuzi wake alikubaliana na madai na hoja za wasanii hao kuwa mdaiwa alitumia kazi zao bila ridhaa yao na kwamba alijipatia mapato, huku wasanii hao wakipata hasara kwa kutofanya biashara kwa kazi zao hizo. Hata hivyo, hakimu huyo alishusha kiwango cha fidia walichodai hadi Sh2.1 bilioni.
Basi hakimu alivuta mpungaTigo hawaja badilisha Mawakili.
Umeambiwa wakati wakikata rufaa Mahakama ilizuia akaunti za Kampuni ya Tigo, huelewi kusoma?MIC wamefeli,hawakutakiwa kulipa kwanza wakati wameenda kukata rufaa higher court..
MIC huko ndani ni lazima kulikua na watu wamekula njama na hawa viazi akina AY walipwe fasta wagawane...
MIC hawakutakiwa kulipa chochote kabisa maana rufaa was on!
Plus,mtu fala ni mtu sio smart kwenye kitu fulani ila anaweza kua smart kwenye kitu kingine,nothing wrong with fala...
Na pia sio lazima niwapende FA na AY,silazimishwi kuwapenda...I can as well hate them!
Anapenda kutumia short cut....Msando ni bushlawyer tunamjua,hajawahi shinda kesi bila kuhongwa....alikua mwanasheria wa exim bank arusha akawa anakula pesa za washtakiwa tu exim wakasanuka na kumtimulia mbali
Huyo jamaa nae ndio miyayusho,unaanzaje kutaka kumuazima mtu hela na hakujua? Huko ni kutafutia watu lawama tu.Tanzania sasa hivi kila mtu anajipambania ajuavyo. Ndio maana leo FA anakula mezani pa wauaji.
Kuna siku jamaa fulani Twitter alimwambia AY, Kaka naomba unisaidie hata 2M ninunue bodaboda hata kwa mkataba nitakurudishia.
Akamjibu kwa kuandika ..........." Download hapa: Milioni2.com.
Tafsiri yake ni kwamba, celebrities siyo ndugu yako, Jali maisha yako.
Ushaligeuza kuwa suala la kishabiki tena?Ahaghh aghh sasa huko Ni kulazimishana kihisia boss huo Ni ukoloni mambo leo
Sio lazima kile unacho kipenda wewe ninacho kipenda mie Basi mtu mwingine nae akipende vivyo hivyo ' Tigo Ni kampuni Ay na FA ni wasanii kwanamna moja ama nyingine kampuni ya Tigo na hao wasanii wote Ni lazima watakuwa na mashabiki zao kwa sababu wote kwa pamoja Huduma wanazo zitoa zina gusa maisha ya watanzania directly
So kwa mantiki hiyo Tigo hawawezi kukosa mashabiki na kina AY na FA Hawawezi kukosa mashabiki pia
Kutaka watu wote washabikie upande Mmoja tu As if wote tuna moyo Mmoja unatoa tafasiri 1 ya kichocheo cha hisia huo sasa Ni ubinafsi na kutaka kuchaguliana maamuzi
Ndio maana mimi naonaga Mahakamani hakunaga haki kama inavyosemwa.Hakimu hashitakiwi hata siku moja kwa maamuzi anoyatoa,hata yawe mabovu kiasi gani,labda kama unaweza kuprove rushwa.
Maisha siyo vitabu ndugu yangu kama wengi wanavyodhani....haki mbinguni tu,duniani humu unaweza tamani kufa, kama huna pesa unaona kabisa haki yako ikinyang'anywa na huna pakwenda.Ndio maana mimi naonaga Mahakamani hakunaga kama haki kama inavyosemwa.