Mahakama yatoa hati ya kumkamata Zacharia Hans Poppe, kuunganishwa kesi ya utakatishaji fedha

Mahakama yatoa hati ya kumkamata Zacharia Hans Poppe, kuunganishwa kesi ya utakatishaji fedha

Unapata fedha Haramu (mfano za kupora benki, madawa ya kulevya, dili serikalini n.k) halafu unatumia Miradi halali (mfano unaanzisha biashara ya night club, kiwanda) kupumbaza Umma wasijue hela umetoa wapi.

Hiyo ndiyo kutakatisha fedha
Asante kwa ufafanuzi
 
Utakatishaji fedha au Money laundering kwa kifupi ni kuchukua mapato yatokanayo na biashara haramu kama uuzaji wa dawa za kulevya, Silaha ama kusafirisha binadamu nk na kuyaingiza mapato hayo kwenye mfumo halali wa uchumi wa nchi kwa kufanya biashara halali
Asante mkuu
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Hivi "utakatishaji fedha" ndio nini?wajuzi tusaidieni maana hata sielewi hawa jamaa walifanyeje?
Unapochukua hela ya wizi ama ela yoyote ambayo haina maelezo ya umeipataje ama ela yoyote ambayo ni nyingi kupita vyanzo vyako vya mapato na kuiingiza kwenye mzunguuko wa hela mfano kununua viwanja, ama kuziweka fedha bank n.k (hiyo ndio kutakatisha fedha na kiufupi kuifanya ela haramu kuwa halali).....kuhusu walifanyaje kwenye kutakatisha hizo fedha hapo sijui ngoja wajuzi wa mambo waje ila unaweza ukabofya kwenye link hapo chini;
Makosa 5 yanayowakabili Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake G.N. Kaburu
 
ULE MZIGOOO AWAKULA PEKEYAOOO INGAWA UJINGA WA KUPELEKA FEDHA ACC ZAO BINAFSI NDICHO KILIWAPONZA ..SASA INAPOELEKEAA WAMEANZA KUTAJANAA SO HUU MTAJOO AUTAISHIA HAPAA SUBIRINI

[HASHTAG]#YAKAYOOOYANAFURAHISHASANAAA[/HASHTAG]
 
Huu uonevu wa serkali
Aliwahi kumlipisha mkulu akiwa waziri wa usafirishaji

ilikuwa pale kibaha mizani kila magari yake yakipita yanaambiwa yamezidi mzigo mkubwa ikaenda hivyo miaka kibao siku moja wakacheza bonge la issue wakafunga vzr malori kama nane hivi na documents zikionyesha kuwa wamebeba mzigo yalipofika mizani wakaambiwa kama kawaida kuwa mzigo umezidi

Basi wakabiwa waache magari hapo atakuja mwenyewe kesho wakaacha document na funguo za magari yote

Oooooooh kesho kaenda pale mizani akasomewa mashitaka akalipa wakati wanamkabidhi akasema ngoja ahakikishe mzigo lallalallalaallalalalalala yeye akijua kabisa kuwa hakuna kitu alifungua na wao wakiwepo gari hazina kitu kesi yake ilikuwa si mchezo serikali ikalipa pakubwa sana
Jamaa aliyepata ukulu kwa shida anakisasi sio kidogo
 
Leo April 30, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwamba mwenyekiti wa usajili wa Simba SC, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Kaburu.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao toka mwezi wa tatu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ .
 
Hans Pope amekaa sana Ukonga nadhani mnamkumbusha machungu ya huko mahala tena kiasi cha kumfanya hata furaha na familia yake ikosekane sasa ...si mnaona wakina Kamishina mstaafu Tillya wa TRA na mkwe wa Lowassa na Mrembo wa TZ
 
Utakatishaji fedha au Money laundering kwa kifupi ni kuchukua mapato yatokanayo na biashara haramu kama uuzaji wa dawa za kulevya, Silaha ama kusafirisha binadamu nk na kuyaingiza mapato hayo kwenye mfumo halali wa uchumi wa nchi kwa kufanya biashara halali
Safi sana mkuu
 
Da! Jinsi ambavyo haivi na Mkuu tangu enzi za mgogoro wa Malori da! Imekula kwake. Kamanda wangu huyu da! Sijui!!
 
Hapo kuna mbumbumbu watasema viongozi wa Yanga wapo rumande wqnasahau viongozi wao wote ndio wapo uko.
Hakuna kiongozi wa Yanga yupo rumande ila kiongozi wa Tff iliopita ndio yupo rumande.
 
Huyu Hakimu na Swai wa TAKUKURU watakuwa mashabiki wa Yanga!!! Haiwezekani mechi imeisha jana eti leo ndo mseme Hans Poppe nae anatakiwa ashitakiwe wakati kesi hii imekuwepo kitambo pia huwezi kusema Hans pope ameshindwa kupatikana wakati kilasiku yupo ofisini na kuongea na media. Huu uonevu hautokubaliwa na wana Simba.
“Simba Nguvu Moja”
 
JAMANI JIRANIYANGUU TANKIBOVU NANI ATATUNULIA KAHAWA KWENYE KIJIWE CHETU DOH
 
Wamenunua sana mechi hawa kwa pesa za kutakatisha

Wafuaji wa pesa
 
Kuingizaa pesa zilizopatikana kwa njia isiyo halali katika matumizi ya kawaida ya pesa mfano,kutumia pesa ulizopata kwa kuuza madawa ya kulevya ukaziweka benki,ukanunulia gari ama nyumba au kulipa deni.Pia kulipia kitu chochote kwa kutumia pesa bandia.Hayo yoootee,ni kutakatisha pesa.Hawa walikuwa wanaiba pesa za Simba wanaingiza kwenye akaunti tofauti na ya Simba halafu wanazitoa wanazifanya kuwa zao binafsi.
 
Back
Top Bottom