GE2025 Mahakama yatupilia mbali maombi ya bodi ya wadhamini CHADEMA. Kesi yapigwa tena Kalenda hadi Agosti 28

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndiyo maana tunasema mahakama hizi ziko mfukoni mwa watawala. Upumbavu huu utaendelea milele bila umma kuamua kufanya kitu.
Ndio madhara ya kuwa na viongozi failures. System nzima, matatizo chungu nzima.
 
Tunaongozwa na watu wenye elimu za kuungaunga. Hawana vision ni mipasho na hasira tu. Kichwa nazi
 
Huu ni mpango wa jamaa aliyepigwa Live pale Mlimani City kuhakikisha kwamba CDM inakufa wakose wote.
Muasisi wa ajabu ambaye anakubali kazi yake yote ya uasisi iishie hapo hapo kisa tu kapigwa kwa kura, - Kwetu buza inaita KIJIBA CHA ROHO

CDM mtashinda hii vita , wala msiwe na hofu.
 
Mwamba kawatumia Wapemba kuuwa chama cha Ukweni 😂😂
Jamaa kumbe ni wa hovyo namna hii, aliifanya taasisi ya CDM kama mali yake. CDM mmechelewa sana kumjua rangi zake huyu jamaa.
CDM mtashinda vita hii msiogope.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, ya kuomba mahakama hiyo kutengua uamuzi wake ulioutoa Juni 10, 2025 wa kuzuia Bodi hiyo na Katibu Mkuu wa chama kutoendelea na shughuli za kisiasa kwa kutumia mali za chama.

Uamuzi huo mdogo umetolewa leo Agosti 18, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema kuhusu mgawanyo wa rasilimali kati ya Chama hicho Bara na Upande wa Zanazibar.

Akitoa uamuzi huo Jaji Mwanga amesema maombi ya Bodi na Katibu Mkuu wa Chadema hayana sababu za msingi za kumfanya atengue uamuzi wake, huku akizibainisha hoja kadhaa ambazo ziliwasilishwa kupitia maombi hayo, ikiwa ni pamoja na madai ya kuwa mahakama haina mamlaka ya kutoa amri ya kuzuia shughuli za kisiasa, mahakama ilisikiliza upande mmoja wakati inatoa amri hiyo na kuwa amri hiyo imesababisha mali za chama kukosa waangalizi, huku upande wa waleta maombi ukidai kuwa utaratibu ulifuatwa na upande wa wajibu maombi ulipewa fursa ya kushiriki kwenye uamuzi huo lakini hawakutaka kuitumia.

Baada ya uamuzi huo kutolewa na Jaji Mwanga, pande zote mbili zimekubaliana kuendelea na hatua inayofuata ambapo Mahakama iliahirisha shauri hilo hadi Agosti 28, 2025 kwa ajili ya mapitio ya hoja mbalimbali zinazobishaniwa na kuweka utaratibu wa kuendelea na shauri la msingi, ambalo msingi wake ni kuwa Said Issa Mohammed na wenzake wanadai kuwa Chadema imekua ikiitenga upande wa Zanzibar katika mgawanyo wa rasilimali hususani fedha.

Chadema/lisu, anapambana, na, ccm kila Kona, akiwa, polisi,ni, ccm wamevaa Magwanda, akiwa, mahakamani, ni, mahakimu waliopakatwa na ccm,
 
ilikuwa lazima hio rufaa itupwe mbali..hapa Chadema walikosea unakataje rufaa kwa yule aliyekuhukumu kwani huyu jaji mwanga ndie aliyehukumu Chadema wasifanye shughuli zozote za siasa na bado Chadema walitegemea huyo jaji eti ajipinge mwenyewe kwenye hukumu aliyotoa mwanzo.ubaya wa hizi kesi za mchongo kila kitu kishapangwa kwamba kesi iende vipi na hukumu iweje..wala hawatazami sheria inasemaje bali waliofungua na kuisimamia hio kesi wanatakaje...nyie hata mkijitetea ni kazi bure mnajisumbua tu
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, ya kuomba mahakama hiyo kutengua uamuzi wake ulioutoa Juni 10, 2025 wa kuzuia Bodi hiyo na Katibu Mkuu wa chama kutoendelea na shughuli za kisiasa kwa kutumia mali za chama.

Uamuzi huo mdogo umetolewa leo Agosti 18, 2025 na Jaji Hamidu Mwanga katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema kuhusu mgawanyo wa rasilimali kati ya Chama hicho Bara na Upande wa Zanazibar.

Akitoa uamuzi huo Jaji Mwanga amesema maombi ya Bodi na Katibu Mkuu wa Chadema hayana sababu za msingi za kumfanya atengue uamuzi wake, huku akizibainisha hoja kadhaa ambazo ziliwasilishwa kupitia maombi hayo, ikiwa ni pamoja na madai ya kuwa mahakama haina mamlaka ya kutoa amri ya kuzuia shughuli za kisiasa, mahakama ilisikiliza upande mmoja wakati inatoa amri hiyo na kuwa amri hiyo imesababisha mali za chama kukosa waangalizi, huku upande wa waleta maombi ukidai kuwa utaratibu ulifuatwa na upande wa wajibu maombi ulipewa fursa ya kushiriki kwenye uamuzi huo lakini hawakutaka kuitumia.

Baada ya uamuzi huo kutolewa na Jaji Mwanga, pande zote mbili zimekubaliana kuendelea na hatua inayofuata ambapo Mahakama iliahirisha shauri hilo hadi Agosti 28, 2025 kwa ajili ya mapitio ya hoja mbalimbali zinazobishaniwa na kuweka utaratibu wa kuendelea na shauri la msingi, ambalo msingi wake ni kuwa Said Issa Mohammed na wenzake wanadai kuwa Chadema imekua ikiitenga upande wa Zanzibar katika mgawanyo wa rasilimali hususani fedha.

Kangaroo courts!
 
Chadema/lisu, anapambana, na, ccm kila Kona, akiwa, polisi,ni, ccm wamevaa Magwanda, akiwa, mahakamani, ni, mahakimu waliopakatwa na ccm,
Tatizo watesi wa TAL hawatumii akili! Atawashinda mapema sana!
Yaani clip moja inatolewa ushahidi na watu zaidi ya 30 wote wakirudia maneno yake yale!
 
Back
Top Bottom