Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake

Mahakama yatupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake

Zipo huru? zingekuwa huru polisi wangekuwa wanazichezea hivyo?
Polisi gani wanaozichezea mahakama? Shida nyie watu mkishajazwa upepo na Mawakili wenu basi mnaamini kuwa their applications will simply be granted. Hivi unadhani ukiambiwa kuwa Kibatala ameweka pingamizi basi unajua it's automatically granted? Acheni ujinga huo, na hawa Mawakili wenu wameshajua kuwa wengi wenu ni maamuma, wanachoamua kukifanya ni kucheza tu na akili zenu na nyie mnatoka mnaimba kama kasuku
 
Polisi gani wanaozichezea mahakama? Shida nyie watu mkishajazwa upepo na Mawakili wenu basi mnaamini kuwa their applications will simply be granted. Hivi unadhani ukiambiwa kuwa Kibatala ameweka pingamizi basi unajua it's automatically granted? Acheni ujinga huo, na hawa Mawakili wenu wameshajua kuwa wengi wenu ni maamuma, wanachoamua kukifanya ni kucheza tu na akili zenu na nyie mnatoka mnaimba kama kasuku
Katawaze
 
Ulikuwa upuuzi mtupu.
ujuwaji mwingiiii!!
mnawachosha mabalozi wa watu bureee mwisho wapate korona!!!
Mbowe anavuna alicho kipanda.
eti anachagua Mahakama ya kusikiliza kesi yake!!
mwishowe atachagua na gereza la kutumikia kifungo chake!!
Akili kisoda mwili jumba
 
Mahakama Kuu Division ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa Leo Septemba Mosi, 2021 imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mawakili wa upande wa utetezi, juu ya Mahakama hiyo kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya Ugaidi.

Usikilizwaji wa kesi hiyo unaendelea.

=====

View attachment 1919552

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imetupilia mbali pingamizi ililowasilisha na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu la kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi zenye mashtaka ya Ugaidi.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Septemba Mosi, 2021 na Jaji Elinazer Luvanda, baada ya kupitia hoja za pande mbili.

Jaji Luvanda amesema mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ugaidi na kwamba pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi halina mashiko na hakubaliani nalo.

"Kwa maoni yangu, sitaweza kukubaliana na hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi," amesema Jaji Luvanda na kuongeza

"Baada ya kupitia hoja za pande zote, mahakama hii inayo mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ugaidi na hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi hazina mashiko," amesema Jaji Luvanda.

Jana Agosti 31, 2021 Mbowe na wenzake waliwasilisha pingamizi mahakamani hapo wakipinga mahakama hiyo kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao kwa mashtaka ya ugaidi na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia Ugaidi kesi yao inapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu ya kawaida na si hiyo ambayo ni Divisheni Maalum.

Baada ya washtakiwa hao kuwasilisha pingamizi hilo, Serikali imepinga hoja hizo ikidai kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya mwaka 2016 makosa yaliyoko kwenye Sheria ya Ugaidi yaliwekwa kwenye Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba kwa hali hiyo mahakama hiyo ya ufisadi ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yao.

Baada ya Jaji Luvanda kutoa uamuzi huo, upande wa mashtaka waliomba kuwasomea maelezo ya awali (PH) washtakiwa hao.

Hata hivyo kabla ya kuwasomea maelezo kufanya, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando anayewasilisha jopo la mawakili watano wa upande wa mashtaka, ameniomba mahakama hiyo, kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa Hoteli ya Aishi ipo wilayani Hai na sio wilayani Moshi kama ilivyoandika katika hati ya mahstaka.

Wakili Kadando baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala amewasilisha pingamizi mahakamani hapo akipinga hati ya mashtaka ina makosa.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Luvanda aliahirisha kesi hiyo kwa dakika 15 ili upande wa utetezi uweze kuja kuwasilisha hoja kuhusu pingamizi hilo huku upande wa mashtaka nao watatakiwa kujibu hoja hizo.

Chanzo: Mwananchi
Walipa kodi kuweni makini, gharama zote za kuendesha mashtaka upande wa serekali unatumia fedha zenu. Jaribu kudadisi au kwenda kumuajiri mwanasheria ujue gharama zikoje. Huduma ya sheria ni moja ya vitu ghali sana huwezi fananisha gharama zake na kumuona daktari.

Wengi watadharau kwa kueka siasa mbele, lakini ni ukweli usiopingika fedha hizi zinazotumika kufanya sarakasi ya kesi zaweza tumika kutatua kero halisi za maisha ya mtu wa kawaida mnyonge. Haipendezi kuona fedha zikitumika kufanya show ya namna hii. Ni majuzi tuu tuliona kesi za ugaidi zikitupiliwa mbali, na hii sioni tofauti.
 
Ulikuwa upuuzi mtupu.
ujuwaji mwingiiii!!
mnawachosha mabalozi wa watu bureee mwisho wapate korona!!!
Mbowe anavuna alicho kipanda.
eti anachagua Mahakama ya kusikiliza kesi yake!!
mwishowe atachagua na gereza la kutumikia kifungo chake!!

Ila huruma mnazo.

Kwamba mabalozi wanachoshwa? Na eti mwisho wapate Corona?

Kwani Tanzania kuna Corona? Kwani mahakamani wamelazimishwa kuja?

Hiiiiii bagosha!
 
Unaonaje bibi anavyowakomesha mataga, sukumagang na kufuta legacy?
Wapinzani kwa upofu wao waliaminishana eti adui yao alikua magufuli leo magufuli hayupo your tanayotokea Kila mtu anaona lakini bado Wala hawajifunzi na kubadilika.
 
Huo ukatili wa Sabaya aliokuwa anafanya Sabaya kwa backup ya Magufuli uko wazi. Na Mbowe anakomolewa na serikali kutokana na kudai katiba mpya. Haya mambo yako wazi.
Acha uongo wewe!
.
Unaweza kuthibitisha madai yako?

Kwanini hizo mahakama zikiwa kwa wanaccm zinatenda haki ila kwa chadema hazitendi haki?
 
Ushahidi wake wala sio wa kutafuta upo wazi.
ha uongo wewe!
.
Unaweza kuthibitisha madai yako?

Kwanini hizo mahakama zikiwa kwa wanaccm zinatenda haki ila kwa chadema hazitendi haki?
 
Back
Top Bottom