Mahakama yawarudisha Askari Polisi waliotimuliwa kazi

Mahakama yawarudisha Askari Polisi waliotimuliwa kazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mahakama Kuu Tanzania imewarudisha kazini askari polisi watatu waliokuwa wakifanya kazi uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo namba 9432 ya mwaka 2024 iliyokuwa mbele ya Jaji Mtembwa, Mahakama Kuu Tanzania masijala ndogo ya Dar es Salaam ambayo inahusisha maaskari polisi watatu wanaofanyakazi katika uwanja huo.

Kurudishwa kazini kwa askari hao kumetokana na taarifa ya hukumu hiyo iliyowekwa mtandaoni leo kufuatiwa maamuzi yaliyotolewa Septemba 10 mwaka huu.

Askari hao waliorudishwa kazini ni Rabson Mosha (EX G4350 CPL), Amelda Honga (EX. WP 7845 CPL) na Denice Kasimbazi (EX, H5338 D/C).

Maaskari hao walitaka kutengua uamuzi wa inspeka jenerali wa polisi wa kuwafukuza kazini mnamo tarehe 5 Oktoba mwaka 2023. Walishitakiwa Mahakama ya kijeshi kwa makosa ya kufanya kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi kwa kumuhoji abiria kwa dakika 51 na kushawishi na kuchukua pesa za rushwa kutoka kwa abiria huyo.

Waleta maombi waliwakilishwa na wakili Peter Majanjara wakati upande wa Inspekta Jenerali wa Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwakilishwa na Wakili wa Serikali Doreen Muhina.

Wakili Majanjara alisema kulikuwa na ukiukwaji wa utaratibu kwa kutozingatia upelelezi wa awali wa makosa yaliyowakabili waleta maombi huku kwa upande wa wajibu maombi walishindwa kuzuia adhabu ya kuwafukuza kazi wakati wamekata rufaa, kwamba kosa la kufanya kitendo kibaya kunyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi kwa kuhoji abiria kwa dakika 51 halikuwa kosa kwenye sheria yoyote na lilitengenezwa ili kuwaondoa waleta maombi kazini, makosa dhidi ya waleta maombi hayakuthibitishwa kwa mkanganyiko kwenye ushahidi na kukosa ushahidi.

Pia, wajibu maombi waliwanyima ripoti ya uchunguzi na mwenendo wa kesi dhidi yao. Upande wa wajibu maombi walijibu kwamba waleta maombi walileta maombi mapya ambayo hayakuwepo kwenye kiapo chao ikiwemo kutosimamisha adhabu ya kufukuzwa kazi wakati wamekata rufaa na kwamba upelelezi wa awali dhidi ya waleta maombi ulifanyika.

Waliongeza na kudai kwamba makosa dhidi ya waleta maombi kutothibitika, Mahakama haina mamlaka kuingilia ushahidi bali kuangalia uhalali wa maamuzi ya chombo cha umma.

Mahakama iliamua kwamba kisheria, wajibu maombi walipaswa kuweka mwenendo wa shauri dhidi ya waleta maombi na kuwapatia nakala lakini hawakufanya hivyo.

Julai 31, 2024 mahakama iliwaamuru wajibu maombi kuweka mwenendo huo kwenye mtandao wa kesi wa Mahakama, lakini mwenendo huo waleta maombi hawakupewa kwa waleta maombi kabla ya kufanya maombi yao na hata wakati wa kufanya mawasilisho yao.

Chombo chochote cha umma kinacholalamikiwa kuhusu maamuzi yake kinawajibika kuleta nyaraka zote zinazohusiana na malalamiko kwa sababu wao ndio wana nyaraka zote za kuisaidia Mahakama kwenye kuamua kuhusu malalamiko yaliyopo mbele yake. Na hata kwenye kesi tofauti tofauti mahakama zimekuwa zikitengua maamuzi ya vyombo vya umma pale ambapo vinashindwa au kukataa kuwapatia waleta maombi mwenendo.

Mahakama pia iliona kwamba wajibu maombi waliamua kutengeneza muhtasari wa mwenendo wa shauri dhidi ya waleta maombi bila uwepo wao.

Mahakama ya kijeshi ilipowakuta waleta maombi na hatia ya makosa dhidi yao, walimuachia Kamanda wa viwanja vya ndege (ASP Geremia Shila) ambaye haonekani akitoa adhabu yoyote kwa waleta maombi lakini akaendelea kuwafukuza kazini. Kwa wajibu maombi kushindwa kuleta mwenendo kamili na kuonesha adhabu iliyotolewa, inaonesha kwamba hakukuwa na adhabu yoyote dhidi ya waleta maombi. Inspekta Jenerali wa Polisi hakutakiwa kutoa maamuzi kwenye rufaa ambayo haikuwahi kutolewa maamuzi ya awali, ni sawa na kusema kwamba Jeshi la Polisi halikuwahi kuwaadhibu waleta maombi, mpaka sasa wametiwa tu hatiani kwa makosa dhidi yao.

Hivyo maamuzi ya Inspekta Jenerali wa Polisi ni kinyume na sheria, maamuzi ya kuwafukuza kazi waleta maombi yametenguliwa.
 
Askari hana ajira.
Askari ameandikishwa Jeshini.

Askari hakufuzwi kazi.
Askari anafutwa Jeshini. Wameshafutwa hiyo ya kurudishwa itabaki stori tu.
Ndio PGO Yao inavyosema ama ni mawazo yako tu mkuu!? Kama wamefutwa kama unavyosema je hawawezi kumlalamikia IGP kufutwa kazi kiuonezi na wakamfungulia kesi ya madai??
 
Warudishwe tu nguvu kazi inahitajika sana kipindi hiki.
 
Askari hana ajira.
Askari ameandikishwa Jeshini.

Askari hakufuzwi kazi.
Askari anafutwa Jeshini. Wameshafutwa hiyo ya kurudishwa itabaki stori tu.
Askari kibao wamefukuzwa kazi na wamerudishwa na mahakama kazini, kinacho wafukuzisha kazi ni makosa ya jinai mahakama ikiwakuta hawana hatia huwa wanarudi kazini nipo mahakamani na nimehudhuria hizo sessions nyingi
 
Ndio PGO Yao inavyosema ama ni mawazo yako tu mkuu!? Kama wamefutwa kama unavyosema je hawawezi kumlalamikia IGP kufutwa kazi kiuonezi na wakamfungulia kesi ya madai??
Wanaweza kufungua kesi ya madai ndo maana wengi wanabembelezwa kurudi kazini ili wasifungue madai ila wapo wanaofungua madai
 
Wanaweza kufungua kesi ya madai ndo maana wengi wanabembelezwa kurudi kazini ili wasifungue madai ila wapo wanaofungua madai
Ni kweli, kuna mmoja alishinda kesi na akakataa kurudi kazini, alifungua kesi ya madai
 
Askari kibao wamefukuzwa kazi na wamerudishwa na mahakama kazini, kinacho wafukuzisha kazi ni makosa ya jinai mahakama ikiwakuta hawana hatia huwa wanarudi kazini nipo mahakamani na nimehudhuria hizo sessions nyingi
Naomba msaada wa sheria je polisi ni mtumishi wa umma ama si mtumishi wa umma!?


Nauliza hivi kwakuwa mtumishi wa umma akifukuzwa kazi kesi yake ya kudai haki mwamuzi mkuu ni Rais ikiwa ataonekana kushindwa Kwa huku ngazi za chini,je ni Kwa vipi polisi kesi yao imefika Mahakamani!?
 
Naomba msaada wa sheria je polisi ni mtumishi wa umma ama si mtumishi wa umma!?


Nauliza hivi kwakuwa mtumishi wa umma akifukuzwa kazi kesi yake ya kudai haki mwamuzi mkuu ni Rais ikiwa ataonekana kushindwa Kwa huku ngazi za chini,je ni Kwa vipi polisi kesi yao imefika Mahakamani!?
Utaratibu wa askari na watumishi wengine ni tofauti Askari wa majeshi yote wana mahakama zao pia ukiona kapelekwa mahakama za kiraia ujue tayari kwenye mahakama zao za kijeshi alishapatikana na hatia na kahukumiwa kufukuzwa kazi ndo anapelekwa kwenye mahakama zetu kwaajili ya makosa ya jinai anayotuhumiwa nayo kama yapo, asipopatikana na hatia haki ya kwanza anayopata ni mahakama kutoa maelekezo ya yeye kurudishwa kazini lakini inategemea na utayari wa askari huyo anaweza kusema anataka kulipwa fidia na siyo kurudi kazini au akakubali kurudi kazini.

Pia wanaweza kukata rufaa kwa IGP au katibu mkuu lakini njia ya ndani huwa wengi hawatumii wanatumia mahakama
 
Back
Top Bottom