Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,434
- 27,177
Katika hali ya kufurahisha, mawakili wamefurahia sana kwa kitendo cha Mahakama zilizokosa weledi hupenda kufurahisha anayewateua majaji na si kufurahisha sheria. Kanuni hiyo inakiuka ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano Watanzania.
Hivyo kanuni hiyo haina uhalali wowote wakuendelea kutumia. Uhuru ulioelezwa ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano Watanzania, haujawekewa mipaka ya kupata, kupokea na kusambaza taarifa. Kwa kuwa mahakama ina jurisdiction katika premises zake, mbona wakati mwingine polisi huwa wanakiuka utaratibu wakiwa maeneo ya mahakama na bado mahakama hazikemei.
Kwahiyo mahakama zimeamua kufyata mkia kwa polisi wanaovunja sheria kwa vitendo vyao wanavyovifanya wawapo mahakamani, ikiwemo kuwapiga watu, kuwadhalilisha. Ikumbukwe polisi wetu wengi elimu ya kutosha juu ya sheria hawana kabisa, badala yake wanafanya kazi bila weledi na hutumia nguvu zaidi mahali ambapo palipaswa kutumia akili tu.
Mahakama si chombo cha kutoa haki pekee bali pia ni chombo cha kuelemisha jamii kuhusu Sheria na kurithisha Sheria na maienedo ya kisheria kizazi hadi kizazi. Hivyo kuwazuia wanasheria kuongerea masahuri yanayoendelea ni kuipofusha jamii kwa maswala ya kisheria.
Pia mahakama mtandao ni nzuri lakini kwa baadhi ya kesi hasa zenye maslai mapana ya umma ladha na uimara wa mahakama uwa sawa inapokuwa ukumbini badala ya mitandaoni. Teknolojia ni nzuri lakini asili sharti ilindwe.
Kama dunavyo fatilia Bunge la Tanzania live na wabunge kuojiwa baada ya vikao vya bunge, Mahakama ya Tanzania hili hamwezi kulikwepa, acheni kuinyima jamii haki ya kuijua Sheria na urithi wa Sheria unaopatikana kwa miendo ya kesi mahakamani na nje ya mahakama.
MWABUKUSI AMEPOST HIVI:
WAKILI HAKATAZWI KUZUNGUMZIA KESI ILIYOKO MAHAKAMANI ANAKATAZWA KUZUNGUMZIA KWA NAMNA YA KUINGILIA UENDESHAJI SHAURI KWA NAMNA INAYOATHIRI NA KUTWAA MAJUKUMU YA HAKIMU AU JAJI.
English: The same Lord Denning was to later pronounce with great erudition that, “Justice has no place in darkness and in secrecy. When a judge sits on a case, he himself is on trial if there is any misconduct on his part, any bias or prejudice, there is a reporter to keep an eye on him.” Lord Denning (Address before the High Court Journalists Association, December 3, 1964).
Kiswahili: Huyo huyo Lord Denning baadaye alitamka kwa ufasaha na hekima kubwa kwamba, “Haki haina nafasi katika giza wala usiri.
Jaji anapoketi kusikiliza shauri, yeye mwenyewe huwa yuko kwenye hukumu... iwapo kuna mwenendo mbaya kwa upande wake, upendeleo au chuki yoyote, kuna mwandishi wa habari anayemwangalia na kufuatilia mwenendo wake.” Lord Denning (Hotuba mbele ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Mahakama Kuu, Desemba 3, 1964).
BAK Mwabukusi