Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel.

Nikahama hotel nikahamia Nyumbani Hotel jamaa akanisaka sikuonana nae maana alitaka anipe hela na niliona kesi yake ipo straight Hana haki na procedure zilifuatwa sikuwa na namna ya kumsaidia .

Ile naingia mahakamani akaanza kunilaumu nikamwambia mie sio Wakili wake na asinipigie tena sababu Sina mpango wa kumsaidia kesi yake ni nyoofu ajiandae kusepa kwanza hakuwa na hela ya maana mteja wangu amenilipa vizuri sana na malazi na safari ananilipa hela nzuri sana .

Jamaa akasema tutaona mie mtoto wa kidigo mie nikamshangaa tu, nikamwambia ukiniroga mie utakuwa unapoteza muda maana Sina ugomvi nawe, kazi umeharibu mwenyewe, aliyekufukuza kazi ni HR na umeshindwa kumroga HR uniroge mie .

Babu Ile naingia kwa Jaji marehemu Lugaziya J sauti ikakata, nikaahirisha kutafuta dawa pharmacy, nikakimbia Bombo hospital pale nnje Kuna pharmacy nikapiga dawa naona naongea fresh kabisa.

Basi nikarudi nikamwambia Karani nipo tayari akitoka kusikiliza anipangie tuingie, Ile nimeingia tena sauti ikakata tena.

This time Jaji nae akaogopa anaongea mambo mengi kwa yule mshtakiwa akamwambia yeye amekaa mahakamani zaidi ya miaka 30 anaijua vizuri akasema aache uhuni wake.

Kesi iliahirishwa but ananiambia Kama unasafiri usiondoke leo 😃 nami nikaona heri nifuate maneno ya wazee.nikaondoka kesho yake. Jamaa siku kesi inaitwa tena anashangaa nipo akajisemea confession aliweka kitu barabarani nisingepona nikamwambia kesi hii nachoweza kukusaidia ni ulipwe kidogo sitabishia 😃😃😃😃 Ila hakurudi kazink.

Uchawi upo. Siku nyingine nitawasimulia yaliyonikuta Mahakama Kuu Tabora Kuna wachawi kule dah
Bora wahusika mkiri maana kuna wapuuzi wakiambiwa uchawi upo wanabishana!
 
Uchawi wa kuroga ATM ukipatikana mnistue
Uchawi una nguvu kwenye mazingira ya kuharibu na si ya kujenga! Ukitaka kufanya jambo lolote hasi uchawi unakuwa perfect yani iwe kukanusha, kukwamisha, kufelisha uchawi una nguvu!

Kwenye ATM haiwezi kufanya kazi sababu uchawi haurogi mashine unaroga nafsi😅
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea.

Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi.

Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani.

Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili

1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa

2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani

Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu

Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu.

Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza

Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.

Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi.

Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu.

Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho.

Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti.

Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi.

Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia

Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena

Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea

Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa,

Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu

Nitaendelea tena baadae kuelezea

Wale wapambanaji hawawezi kushangaa ninachokisema hapa, Hakuna maisha ya mteremko hapa duniani you have to fight
Mungu ajaalie usije ukauponza kwa kutaka vya bure
 
Unajua kumloga mtu lazima ujue majina yake Matatu ili ujue nyota yake, sehem kama hizo za watu wengi lazima tu uongee na mlinzi umpe hela ili akupe ruhusa ya kuweka madawa maana haya mambo yanaakiwa mfano ukaweke mahakamani Saa Saba usiku au umeambiwa ukaweke mlangon siku ya jumaosi saa kumi na mbili unafikil bila kuwaomba na kuwapa pesa walinz utafanikiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh mimi sijui ila kama ni mchawi kabisa, anaweza ingia sehemu yeyote muda wowote.
 
Kuna shahidi alikuwa kila akiulizwa lilipotokea tukio yeye anataja Chanika wakati tukio limetokea tegeta...kila akiulizwa dar es salama unaifahamu vizuri na vitongoji vyake hasa Tegeta na Chanika anaeleza vizuri kabisa lakini akiulizwa unakumbuka tukio lilipotoke yeye anasema Chanika...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
huyu tapeli anataka kuwatapeli hela. nimefanya kazi Mahakamani miaka mingi, hakuna uchawi unafanya kazi Mahakamani. utapoteza pesa zako tu. ingekuwa hivyo hakuna mtu angefungwa. kuna waganga wa kienyeji wamejaa magerezani huko. kitu pekee ambacho niliwahi shuhudia ni kuuliwa kwa hakimu na pp, na hata hivyo hao wanaokufa huwa wale ambao hawana Mungu. na hata ukiua mmoja, kesho mwingine anachukua jalada mambo yako palepale.
Acha ubishi.
 
Babu huwa anatuma joka siku ya hukum kama kesi ni ngumu kwake. Hakimu akikaa tu mezani cobra linamsimamia mbele tayari kumgonga akitaka kutamka neno tu. Mahakimu huwa wanatoka na kuita karani ataje siku nyingine mwisho kesi inafutwa.
Siku moja alikutana na hakimu anatokea usukumani
Kilichotokea ............
Nashindwa kusimulia ila ilikuwa ni Singida.
Babu bado yupo.

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea.

Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi.

Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani.

Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili

1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa

2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani

Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu

Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu.

Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza

Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.

Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi.

Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu.

Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho.

Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti.

Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi.

Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia

Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena

Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea

Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa,

Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu

Nitaendelea tena baadae kuelezea

Wale wapambanaji hawawezi kushangaa ninachokisema hapa, Hakuna maisha ya mteremko hapa duniani you have to fight
Umeharibu pale ulipoanza swaga za kutolipa nauli

Chai ya moto ktk bakuli la bati
 
Wakati nikiwa field, Hakimu Mkazi fulani alinisimulia namna ambavyo alikuwa analazimika kusimamisha shughuli za Mahakama na kuanza kukemea mapepo. Hii ni baada ya hali ya chumba cha Mahakama kubadilika na kuhisi harufu za ajabu na maruweruwe.

Pia msaidizi wake alinisimulia namna ambavyo alikuwa anaumwa kichwa na kushindwa kuandika hukumu ya kesi ambayo ilishaamuliwa.

Mahakamani kuna mengi; siyo kesi tu
Katika Mahakama naona Mahakimu ndio wana kazi ngumu sana kuliko Majaji.
Mahakimu ndio wanao fanya kazi kwenye mazingira magumu zaidi kuliko Majaji, lkn cha kushangaza eti Majaji ndio wanalipwa vizuri zaidi kuliko Mahkimu.

hivyo ni vyema Serikli ikwajali sana Mahakimu ktk masilahi yao kuliko Majaji.
Kutoa haki sio kazi ndogo.
 
Back
Top Bottom