Mama pretty
JF-Expert Member
- May 1, 2020
- 2,082
- 4,103
Amen. Hakuna gumu ukimtegemea Mungu.Naogopa kweli...hapa nilipo nasubiriwa na kesi kama hii basi naogopa mnoo maana complications ni nyingi mnoo. Mirathi ni mbaya sana.
Mungu atutetee.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amen. Hakuna gumu ukimtegemea Mungu.Naogopa kweli...hapa nilipo nasubiriwa na kesi kama hii basi naogopa mnoo maana complications ni nyingi mnoo. Mirathi ni mbaya sana.
Mungu atutetee.
AmenAmen. Hakuna gumu ukimtegemea Mungu.
Kila la kheri Mheshimiwa.Amen
Me sio mheshimiwa hakimu ila ni mmoja wa beneficiary wa mirathi..Kila la kheri Mheshimiwa.
We uoni kuwa ni tangazo la biashara kwa story za kusadikika hizi.Usije huko mwisho ukaharibu kwa kuweka namba ya mtaalam tu maana hapo tutakushtukia kuwa nia yako ni kutangaza biashara.
Japo mpaka mwisho wa siku leo Inbox yako itajaa msgs hasa toka kwa kina dada wakiomba contacts za mganga.
True ,Wengi wasingefungwa jela.Uongo wa kiwango cha Juu, hawakukumbuki wewe kabisa, Ila kuna records, kuna arrest order Na wewe ulichagua option two!
Uongo narudia tena uongo! Kuna watu Wenye fedha nyingi wamefungwa life time and mganga angekuwa an easy option!
Hakuna Mganga anayeweza kufuta Kesi, simply hayupo, Na hawa Ma police Nina uhakika wana fungu la kujiweka Sawa!
Uongo uongo uongo Na uzandiki
Yote kwa yote iwe kheri kwako. Naelewa changamoto ya kesi za namna hii..Me sio mheshimiwa hakimu ila ni mmoja wa beneficiary wa mirathi..
Mganga alimpeleka sehemu ya ajabu sana.
Sehemu gani mkuu?! Eleza tu usiwe na shaka, anonymity inatulinda humuMganga alimpeleka sehemu ya ajabu sana.
🤭🤭🤭🤭🤭 duh wengine unakuta hakimu hawezi kusoma hukumuNyie haya mambo yapo sana tu ila watu wanabisha.
Balaa jingine lipo kwenye kesi za mirathi, kuna wilaya moja kwenye mahakama fulani ya mwanzo kulikua na kesi ya mirathi ambayo kila ikikaribia siku ya hukumu inaondoka na hakimu mkazi anaehusika na hiyo kesi. Wakaamua waifute tu maana iligharimu sana maisha ya watu.
Kesi za mirathi zinaogopwa sana na mahakimu.
Makaburini walipita msituni.kinacho muuma zaidi alimwambiaga mmewe kuwa rafiki yake ni mwathirika afu still akawafumania ndo maana aliamua kumwacha akaondoka na watoto.Sehemu gani mkuu?! Eleza tu usiwe na shaka, anonymity inatulinda humu
Na ameiandika mwenyewe...🙌🤭🤭🤭🤭🤭 duh wengine unakuta hakimu hawezi kusoma hukumu
huyu tapeli anataka kuwatapeli hela. nimefanya kazi Mahakamani miaka mingi, hakuna uchawi unafanya kazi Mahakamani. utapoteza pesa zako tu. ingekuwa hivyo hakuna mtu angefungwa. kuna waganga wa kienyeji wamejaa magerezani huko. kitu pekee ambacho niliwahi shuhudia ni kuuliwa kwa hakimu na pp, na hata hivyo hao wanaokufa huwa wale ambao hawana Mungu. na hata ukiua mmoja, kesho mwingine anachukua jalada mambo yako palepale.Wanabodi,
Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea
Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi
Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani,
Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili
1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa
2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani
Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu
Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu
Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza
Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.
Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi
Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu
Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho
Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti
Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi
Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia
Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena
Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea
Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa, Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu
Nitaendelea tena baadae kuelezea
Kumbuka sitatoa namba za hao waganga hapa JF. mnivumilie.
Baadhi ya dawa kuna Dada wanazitumia kuvuta wanaume hasa ile ya mafuta inawapa mng'ao na mvuto huwa wanaomba nawapa bure tu kidogo kwa kuwamininia. Mimi situmii haya madawa kwa sasa wala siwezi toa kwa mtu hapa JF