Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

..Rais Samia Suluhu ameshindwa kuwashawishi viongozi wenzake wampigie kura Raila Odinga.

..enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, mgombea aliyeungwa mkono na Tanzania ilikuwa lazima ashinde.

Yes, na kipindi kile mgombea lazima aje kuhiji Tanzania, ili kuweka mambo yake sawa. Tanzania ya sasa bado hrijajua jukumu ililo nalo kwenye uwanja wa kikanda, Afrika na nje yake
 
ni wazi hiyo ni miongoni mwa sababu muhimu zilizomkwamisha muungwana,

Mahamoud Yusuph anazungumza zaid ya lugha5 za kigeni ukilinganisha na Raila anaezungumza kiingereza na kiswahili pekee :NoGodNo:

Kama ni hivyo kuna shida mahali. Yaani lugha pekee ndiyo iwe sababu ya kumtupa nje Raila Odinga. Anawez asizungumza lugha nyingi, lkn akawa bora ktk mambo mengi tu
 
Mbona salim Ahmed hakuwa katibu wa UN licha ya kutakiwa na Hyyo unayemwita ana yshawishi lakini koffi Annan aliweza justify your comment
Issue ya Salim Ahmed ilikuwa ni kutokana na mvutano baina ya US na China, (western vs eastern blocks). US alipiga kura ya veto kwa Salim na China alipiga kwa Kurt Waldheim, matokeo wote waliondolewa na akawekwa de Cueller.

Baadae alikuja Boutrol Ghali (Egypt) lakini US hawakumtaka baada ya kipindi kimoja, ndipo Salim akapendekezwa tena kwa mara ya pili. France walimkataa kwa vile alikuwa haongei kifaransa ndiyo akawekwa Koffi Anan.

Salim alipigiwa debe sana na Nyerere na alipata support ya OAU na nchi nyingi za dunia ya tatu, lakini big boss US hakumtaka kwa sababu ya msimamo wake kuhusu China na support kwa Palestine.

Mara ya pili (1996) Mandela alimpigia chapuo sana lakini France ndiyo iligoma.
 
Kama ni hivyo kuna shida mahali. Yaani lugha pekee ndiyo iwe sababu ya kumtupa nje Raila Odinga. Anawez asizungumza lugha nyingi, lkn akawa bora ktk mambo mengi tu
ujuzi wa lugha mbili kuu ni muhimu sana kwa posts kama hizi - english na french.

Tatizo letu Tz hatuchukulii umuhimu wa kujua lugha hasa french na hapo ndipo tunapopigwa bao kirahisi.
 
Kama ni hivyo kuna shida mahali. Yaani lugha pekee ndiyo iwe sababu ya kumtupa nje Raila Odinga. Anawez asizungumza lugha nyingi, lkn akawa bora ktk mambo mengi tu
si hivyo tu,
bali pia kama nilivyoeleza kwenye reply ya kwanza kwamba,
blocks za Africa magharibi na baadhi ya miongoni mwa members wa blocks za kusini mwa Africa walijipanga vizuri zaidi kuhakikisha mtu kutoka pande hizo ndie anaendelea kuongoza taasisi hiyo nyeti Africa. ukilinganisha na Raila odinga ambae hakua na uhakika hata na baadhi ya members wa Africa Mashariki ikiwa waTamchagua :NoGodNo:
 
Huwezi kuwa inatokea Nchi ya wasakiti na vibaraka kama Kenya harafu ukashinda.

Odinga ni mgombea sahihi ilakutoka Nchi ya hovyo 🤣🤣🤣😬

Pole sana Mzee ndio hivyo tena maisha yaendelee.

View: https://x.com/TheCitizenTz/status/1890788433095770264?t=QRzw9yOabqLLKXXgzZhezA&s=19

My Take
Hii ni mara ya pili Kenya kuangukia pua,Tanzania hatujawahi shindwa popote.

View: https://www.instagram.com/p/DGGTdQ-oSgC/?igsh=emRtNDhycXcxcjNu

RAO ajiandae tu kupambana na Rutto uchaguzi wa 2027.
 
Wewe Huwa hufuatilii mambo hayo ndio maana hujui kitu.

RAU ni maarufu huku kwenu sio huko kwingine.

Na Kwa taarifa Yako tuu,pamoja na Rais Samia kumualika kwenye mkutano wa Nishati kama njia ya kumnadi ila mgombea wa Djibouti Ali tweet Kwa Samia akisema anapoteza mda,yeye Mahmood ndio atashinda hiyo nafasi 🤣🤣
Naiomɓa hiyo tweet as "evidence to proof " narration yako
 
Back
Top Bottom