Maharage Chande: Hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta(Kununua umeme). TANESCO kuuza dhamana(Bonds)

Maharage Chande: Hatuogopi na tutafanya hiyo miradi na private sekta(Kununua umeme). TANESCO kuuza dhamana(Bonds)

Sasa huyo Chande kakuibia Nini? Bora useme mtu sio competent ila randomly kuita watu wezi sidhani kama ndio JF tunayoitaka.

Kibaya zaidi 90% hapo hamjasikiliza hata hiyo clip kabla ya comments, Sasa hamtaki wauze bonds Bado hamtaki wabinafsishe wakati huo huo hamuamini hao viongozi wa serikali Sasa mnataka Nini?

Mfano Mayor Quimby anakomaa kuwa hakuna mtu atanunua hisa or invest kisa TANESCO haipo competent. Muda huo huo hataki ibinafsishwe, muda huo huo Chande ni fisadi, muda huo huo anadai Zitto (mpinzani) anaandaa Dili la kifisadi hapo.

Sasa mnataka Nini kama sio chuki tu
Umeshanasa kwenye ulimbo wa defence, tatizo linaanzia hapo. Iruhusu akili yako ione kwa usahihi...

Hapo huyo mtu (Uliyemtaja kwa jina) kama yeye anahusikaje? Si ndiyo mnaonekana kama vile mnapigania maslahi bianfsi na siyo ya taifa na watu wake?
Yeye alikuwa MD IPTL ilipoingia mkataba? Lakini taasisi na cheo alichonacho kilikuwepo, so kama mkuu angetakiwa aelewe mazingira halisi anayo operate, asingeleta vitu vyenye sura na taswira ile ile kama ya MD wa wakati huo...Hiyo infact kama hampendi kuelewa ndiyo inayo provoke public...

Dhamira yake na wenzake kama individuals inashindwa kuji express katika namna na jinsi anayotaka kuitumia...Kuna tatizo la critical thinking kama taifa kwakua ubinafsi unaochagizwa na umasikini unatusumbua...Kila mtu ameshakata tamaa anatafuta jinsi ya ku escape poverty wakati mifumo inabana ndiyo sababu tunakuwa na shida ya fikra huru
 
Sasa angalia mtu kama huyu, anachoeleza hata hajui anaeleza nini; kwa hiyo hawa sasa ndio wanaoshikilia hatma yetu katika eneo hili!

Miaka zaidi ya 60, watu wetu wakienda shule, matunda yake ndiyo haya?
Tuhurumie mkuu, usiombe umasikini ukawa ndiyo background yako, unaathiri sana fikra na atttitudes
 
Nime'skim' harakaharaka kwenye majibu yako ya uteyezi humu, lakini sijaona maelezo ya huyo Maharage kuhusu uwezo wao, au kutokuwa na uwezo katika kuendesha Tanesco kwa ufanisi.
Ninachoona kwa wingi ni msisitizo tu wa watu wengine kuja kuwafanyia kazi.
Sijui kama ninakutwisha mzigo usiokuhusu kutoa maelezo juu ya jambo hilo kwa niaba yao(Tanesco).

Naelewa hizi ni enzi za 'fashion' ya PPP na matakataka mengine mengi tunayohimizwa tusiyafanye wenyewe kwa sababu tu ya hizo 'fashion' mpya zinazohimizwa. Hata mara moja sisikii kamwe, tukijiamini kwamba nasi tunaweza kufanya baadhi ya mambo muhimu yanayotuhusu sisi wenyewe.
Mjiamini? Si watu wanasema Makamba na Chande wanataka kufanya ufisadi means hamna Imani na serikali kusimamia sekta ya Nishati wakati huo huo PPP hamtaki wakati huo huo mikopo/bonds hamtaki. Kaongelea masuala ya umeme wa gesi kama suluhu ya mgao watu wanakomaa kuwa ni ufisadi!!

Sasa mnataka Nini? Ndio maana nikasema Kuna chuki bila sababu. The guy might not be competent ila sio fisadi at least for now.
 
Tunataka awe realistic kwenye hizo investment plans zake na umeme wa uhakika kwanza.

Umeme hakuna lakini kila siku wanatupigia tantalila tu za mambo ambayo sio priority zetu tushazichoka.
Realistic kivipi? Automation sio realistic? Si wamesema mgao itaisha before Christmas why usisubiri ndio umkaange kisawasawa?

Kuongeza capacity ya umeme wa gesi Kinyerezi sio realistic? Naelewa watu mna hasira ila tuwe optimistic, kama gesi itachangia gridi ya taifa by 70% unadhani tutakua tunalia Lia Tena mgao mvua zikikwama? Hakuoni ni sustainable zaidi?!
 
Ndugu hivi karibuni tu tumetoka kuambiwa TANESCO wamefutiwa deni la TPDC lenye thamani ya trillion or two (if I remember correctly more on the latter).

Msingi wa ilo deni ni malimbikizo ya gas purchase, na hiyo ni bidhaa muhimu kwenye uzalishaji wao wa umeme.

Thanks god lilikuwa ni deni la serikali rahisi kulifuta, vinginevyo ingekuwa ni deni la private sasa hivi hiyo mitambo ya umeme ingeshafungwa au serikali ingekuwa itoe hela za kodi kulipa hilo deni na kuwanunulia gas juu ili kinyerezi izalishe.

Sasa mtu ambae ajaonyesha ata uwezo wa ku-manage finance za shirika , kuonyesha uwezo wa kutengeneza sustainable business, kutengeneza net profit, improvements on important ratio kwenye balance and so forth.

Leo mtu wa aina hii ambae ajatuonyesha ata uwezo wa kumudu gharama za gas wanayotumia kuzalishia umeme mnataka tuanze kumu encourage aingie kwenye commitment za kununua umeme wa makampuni binafsi akishindwa kulipa serikali itoe hela za walipa kodi kugharamia hayo madeni na gas wanunuliwe tena.

Listen huyo mtu ajaonyesha uwezo wa kuendesha hilo shirika kwa faida bado, acheni kumu encourage kujiingiza katika commitment zingine zitakaloliongezea shirika pressure za financial burden.

Watanzania tunapenda mambo makuu makuu wakati basic hatuja master bado.
 
Historia huwa inatabia ya kujirudia. Maharage Chande asije akatufanyia kama yale aliyotufanyia Dr Idris Rashid kwenye awamu ya nne ya Jakaya Kikwete. Idris alikuwa gavana wa benki kuu akapelekwa kuwa Managing Director wa tanesco. Akatuletea makampuni binafsi ya nje kutuzalishia umeme kwa mitambo ya kukodi. Makampuni hayo ni pamoja na Dowans, Richmond, Symbion na IPTL. Tukawa watumwa wa capacity charges za mabilioni ya pesa kila siku. Mafuta ya kuwasha mitambo hiyo tunaweka sisi kwa gharama ya tanesco lakini umeme unaozalishwa tanesco wanaununua kwa bei kubwa sana. Hata kama mitambo yake imezimwa tunalipa mabillioni kila siku. Maji ya bwawa la Kidato na Mtera yakawa yanafunguliwa. Sakata la Richmond likamng'oa Waziri mkuu (Lowassa) na waziri wake wa nishati (Dr Rashid Msabaha). Ufisadi mwingi ulifanyika tanesco wakati Dr Idris Rashid akiwa ndiye MD wake.

Tatizo linaweza kuanzia hapo ulipoandika SIKUTAKA HATA KUSIKILIZA....

Hapo pana tatizo kubwa sana, kubwa mno.

Inawezekana kabisa kwamba "sisi" tuna uelewa mkubwa na maarifa mengi zaidi kuliko watu wengine. Hili ni jambo jema sana na ni jambo la asili (ni majaaliwa).

Lakini hii haitoi haki wala uhalali wa kutokuwasikiliza wengine tunaodhani wana uwezo mdogo kuliko "sisi".

Masikilizano ni nyenzo muhimu sana katika kujenga kwa pamoja.

Hii nchi ni yetu sote, angalau tuanze kwa kuwa tayari kusikilizana.
Moderators nashauri hii comment iwe comment bora ya mwaka 2022 halafu uzi ufungwe watu wakaufanyie kazi ushauri uliotolewa.
 
Mjiamini? Si watu wanasema Makamba na Chande wanataka kufanya ufisadi means hamna Imani na serikali kusimamia sekta ya Nishati wakati huo huo PPP hamtaki wakati huo huo mikopo/bonds hamtaki. Kaongelea masuala ya umeme wa gesi kama suluhu ya mgao watu wanakomaa kuwa ni ufisadi!!

Sasa mnataka Nini? Ndio maana nikasema Kuna chuki bila sababu. The guy might not be competent ila sio fisadi at least for now.
Hukujibu kitu kabisa.
Nadhani katika kuufahamu umakini wako ulionao kupitia humu JF, haya uliyoandika hapa yanatofautiana kabisa na mategemeo niliyonayo juu ya uwezo wako wa kujibu hoja.

Mi nadhani hukuwa na jibu.
 
Sasa mnataka Nini? Ndio maana nikasema Kuna chuki bila sababu. The guy might not be competent ila sio fisadi at least for now.
Wewe umeyajuaje haya kuwa na hakika kiasi hiki juu yake.
Na wala hilo halikuwa lengo langu katika andiko ulilojibu hapa.
 
Halafu huyu mama ni potential wa mlipuko tena si bomu la kawaida ni nuclear hizo story zote za kina zito ni introductory
Yeah wanaandaa mazingira rafiki ya kulipua bomu.

Ila nahisi wizara ya Nishati huenda linaandaliwa bomu kubwa sana.

Bodi ya Tanesco kwa sasa imeundwa na wafanyabiashara watupu.
 
Tunataka awe realistic kwenye hizo investment plans zake na umeme wa uhakika kwanza.

Umeme hakuna lakini kila siku wanatupigia tantalila tu za mambo ambayo sio priority zetu tushazichoka.
Una maoni Gani kwa Sasa. Si walisema mwaka mpya mgao umeisha!! And they delivered. Next time msipende kuandika tu for the sake
 
Hapa kwanza linatengenezwa tatizo ambalo ni huu mgao ili ipatikane justification ya kutafuta wawekezaji Kisha from there Kuna ufisadi takatifu unakuja kupitia hayo makampuni

Kama hamuelewi mashirika ya umma ni sehem ambazo ufisadi mkubwa hufanyika na yanahujumiwa sana ni swala la muda ila CCM kama wanawapenda watanzania wamtoe huyu mama waweke mtu mwingine yaani tumekwisha deni la Taifa ni Trillion 70+ mfumoko wa Bei, ufisadi Kila Kona kidaraja Cha milioni 500 unaambiaa 7 billion yaani Kuna watu wanakula Kwa hasira maana walibanwa muda mrefu kiukweli ngoja tuone ni swala la muda ila TANESCO ni kichaka Cha kufanyia fraud
Mna maoni Gani kwa Sasa tokea mvua zianze kuonyesha, mgao feki Bado unaendelea?
 
Niliwahi Sema humu ndani.. Huu mgao wa Tanesco ni njia moja wapo ya kubinafsisha iliionekane Tanesco imeshindwa kujiendesha..

Kama ilivyofanyika kwa TTCL tutarajie the same kwamba Tanesco itakuja kuwa kama Shule ya kata.. Na mashirikia binafsi kama vile international school of Tanganyika [emoji23][emoji23]

Bila maneno mengi.. Mikataba watakayoingia Hawa watu ndio utakayo amua hatma ya nchi yetu kwenye swala Zima la nishati..

Magufuli aliyasema haya.. Atakayekosea asiseme tu hakujua anachofanya huko mbele ya safari
Wazee wa speculations mna maoni Gani kwa Sasa.
 
Haya ni "MakambaMahaharage"

Majizi tupu! Hakuna lolote hapo!

Huyo Zitto mzee wa fursa, hapo ameuliza Swali elekezi!

Tayari na yeye ni sehemu ya mpango Wizi.

Ina maana kuna Deal Na "Mazda" na sasa linakolezwa taratibu.

Hawa tutakuja kuwanyonga hadharani, kama sio sisi basi watoto wetu watawanyonga watoto wao.
Wivu utakuua kaka, umekariri zile siasa za kuwa huyo ni mtu wa JK na JK ni msimamizi wa wapigaji!.

Badili hiyo thinking itakuacha na maumivu na kununa hovyo bila ya sababu za msingi. Epuka siasa za makundi.
 
Una maoni Gani kwa Sasa. Si walisema mwaka mpya mgao umeisha!! And they delivered. Next time msipende kuandika tu for the sake
Shida ya watu kama nyie ni kujibu hoja at your suitable time, whereby the matter of concern requiring immediate innovation to reduce the negative impact is longer relevant.

Unakuja kujibu hoja later under the environment which favours your viewpoint. Kama uongozi ungekuwa rahisi hivyo huko duniani kwengine wangesubiri mpaka mwezi wa sita bei za nishati zishuke kama wanavyotabiri ndio waanze kujibu kuhusu inflation huko kwao.

That’s not how leadership works unatakiwa kuonyesha mitigation strategy zako za kukabiliana na unplanned diversity soon as they happen mbinu ambazo hazikuwepo wakati nchi ipo gizani.

Isitoshe msingi wa hii mada ilikuwa kwenye kuvutia uwekezaji. Hasa kwenye greener technologies sitegemei huyo Chande wako wala Makamba kuelewa how carbon trading works na trust me; ndio kitu pekee kinachowafanya wageni kuja kuwekeza Africa kwenye sector ya umeme.

With that knowledge at times inabidi sisi wa vijijini tukubali maisha na mipango ya watu mjini sio yetu, maana akili zenu zinawatosha nyie wenyewe kwenye kupanga mipango yenu ya muda mrefu.

Huko kwenye kuuza bonds sijui kutafuta hela kwenye capital markets ndio kabisa wanaongea ujinga mtupu; vinginevyo wangeshafanya.Hizo hela za sijui kuimarisha grid zitatoka mfukoni kwa walipa kodi tu awawezi pata kwenye soko la hela kama walivyodao.

Sasa kwanini mie niumie kama Bashe kapewa na atapewa karibu kiasi cha hela hizo TANESCO wanazotaka wafanye huo mradi, wakati yeye anapewa kila mwaka kwenye mbolea na upigaji wake umemfanya awe filthy rich kwanini niumie kwa TANESCO.

I am beginning to accept these are not my problems hayo ni matatizo ya watu wa mjini, sie tunaoishi vijijini sasa kwanini tuumie vichwa.
 
Kwanini unasema hawawezi? Why mnapenda zero sum games? Why usishauri namna Gani wapate hizo fedha ila unasema tu HAWAWEZI shows chuki ulizonazo Tu.

2. Wala sio nmechagua convenient time ila waliahidi kuwa umeme utaacha kukatika January and they delivered wakati majority yenu humu mlidai mgao ni sababu hawako competent.

3. Kingine long term wamesema ni gesi na inajengwa pale Kinyerezi 2 extension na Kinyerezi 3 Sasa kivipi unasema sio long term!! Wenzio wanaacha Maji waende kwenye gesi alafu unasema sio sustainable?

4. Unadai mbolea Kuna ufisadi which is pure speculation na inaonyesha how unapenda kuchafua watu out of mere hearsay. Tujitahidi kuwa supportive and optimistic hii kukosoa tu na kuamini hakuna anayeweza ni mindset mbaya sana.

Eti hawawezi!! Kwani wamejaribu wameshindwa? Hivi realistically serikali hata ikisema inauza TANESCO itakosa mteja?? They can restructure the company ama kufungua jipya likiwa fully branded unadhani litakosa wawekezaji?
 
Jamaa anaeleza mambo yake vizuri sana. Tumpe muda na nafasi atatusaidia kuibadilisha TANESCO kutoka kwenye hii ya sasa kwenda kwenye iliyo bora zaidi.
TANESCO ni taasisi nyeti, it is not quite subject to standard business-school or activist modes of evaluation. Kuna wakati fulani kulitoka dhana ya unbundling (generation, transmission, distribution) with fancy ecometric models. It it was tried here and there tulipojaribu TANESCO ikashindikana Wanasiasa hawakuielewa, and rightly so because you cannot unbundle a son from its father. Hizi piecemeal solutions zitazaa matunda in isolated cases lakini the underlying principle haijabadilika - focused management geared toward IPTIMISING the situation, with lots and lots of Government support same way as you support Msonganzila or a national airline. Hii ya bonds za DSE inahitaji discipline ya securitisation ambayo ni ngumu kisiasa. Tumtakie heri Ndg Maharage, he will need it.
 
Back
Top Bottom