Maharage Chande: Si busara kushusha bei ya umeme

Maharage Chande: Si busara kushusha bei ya umeme

Tatizo ni ujinga wa Watanzania na uongo wa wanasiasa. Hili tulishaliona na kulijadili zamani tu.

Wanasiasa wakitaka kuanzisha mradi basi wanawadanganya wananchi kwamba mradi ukiisha mambo yatakuwa mazuri na gharama zitashuka, wakati si kweli kwa sababu wanakuwa wameanzisha huo mradi kwa kukopa pesa.

Hapo na bado SGR ikikamilika ni lazima bei ya nauli ipande.

Wanasiasa wajifunze kuwaambia ukweli wananchi.

Kwa Tanzania hii, Serikali ikikopa pesa na kuyapeleka maji ya ziwa Viktoria Dodoma, lazima yatapanda

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Haya mawazo yanakuwa vipi hoja ni ipi lengo la mkopo wowote ule ni kuwafikia watu wengi katika kutoa huduma kwamba ata mimi nikienda bank nikachukua mkopo niungize kwenye duka langu lazima bidhaa nipandishe bei sababu nimekopa
 
Wataalam wetu wa chuo cha kijeshi na uchumi pale arusha wakikuwa watatuletea maendeleo kwa sasa tuwaache hawa wataalam wasio wazalendo wapite tu.maswali ni mengi sana .
 
Huyo Maharage anaijua kanuni ya demand and supply na price inavyokuwa affected?

Huyo Maharage anataka tuendelee kukata misitu ili tupate kuni za kupikia na nchi igeuke jangwa?

Huyo maharage hataki cost of production zipungue ili kuvutia wawekezaji nchi isonge mbele?

Magufuli alisema anajenga bwawa ili umeme uwe nafuu, sasa huyu Maharage ni nani hata atake bei ya umeme isishuke?
 
Watu kama Chande huwa hawafurahii NAFUU ya maisha kwa binadamu wenngine! Hapo utakuta yeye anapewa pesa hadi ya mafuta ya Gari lake achilia mbali huduma ya Bure ya umeme nyumbani kwake ila bado anaona sisi wengine bei ya umeme ibaki hiihii 300++ kwa unit ili hali Kuna uwezekano wa kushusha bei

je mnajua wafanyakazi wote wa tanesco wao hununua umeme ofisini kwao kwa bei ya cheee kabisa kila mwezi au hamjui
 
Tanzania ina Viongozi Ambao Hawajui kabisa hali za Watu wake. Viongozi wana wafananisha wananchi na hali zao wanadhani wananchi ni vigogo kama wao.
 
Sasa mtu kama yule mtoto wa Mwananyamala kupewa kitengo hujui nini kinaendelea? Yule hana final decision yoyote. Hawezi kutoa jibu kamili kwasababu ni sellout kitambo.
 
Haya mawazo yanakuwa vipi hoja ni ipi lengo la mkopo wowote ule ni kuwafikia watu wengi katika kutoa huduma kwamba ata mimi nikienda bank nikachukua mkopo niungize kwenye duka langu lazima bidhaa nipandishe bei sababu nimekopa
Huo ndio ukweli. Lakini wanasiasa huwa hawawambii ukweli wananchi kabla mradi haujanza kujengwa. Mradi ukikamilika bei ya huduma inapanda zinaanza kelele.

Yaani huwa serikali inawavizia wananchi pale inapotaka baraka za wananchi kuhusu mradi fulani, lakini viongozi wanajuwa wazi mradi ukikamilika ni lazima wapandishe bei ili wapate marejesho ya mkopo huko walipokopa.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Angalia Nauli zilipanda kwa kigezo cha bei ya mafuta ila mafuta yameshuka ziko pale pale Sasa yatakuwa kupanda kufikia bei ile ile iliyosababisha kupanda Nauli na Nauli zitapanda tena.
Hii ndiyo Afrika mkuu, ukiweza kufanya lako ukatoboa basi simamia hapo hapo na upande juu, usisahau kuwaonyesha njia uliyopitia wanao.

Look at the politician child's.
 
kutoka katika gazeti la mwananchi:

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema hadhani kama ni busara kushusha bei ya umeme baada ya mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) kuanza uzalishaji.

Chande amebainisha hayo leo Mei 26, 2023 wakati akijibu swali na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Beatrice Bandawe aliyetaka kujua kama bei ya umeme itashuka baada ya mradi huo kuanza uzalishaji.
Amesema huwezi kushusha bei ya umeme baada ya kuanza kuzalisha JNHPP wakati hata miundombinu inayojengwa kwa kutumia mapato yanayotokana na uuzwaji wa umeme haijakamilika.

"Mimi sidhani kama ni busara kushusha bei ya umeme ili fedha tutakayobaki nayo ibaki kuhudumia umeme. Hapa ni vizuri kutofautisha bei na gharama, ni vitu viwili tofauti," amesema Chande.

Mkurugenzi huyo ameongeza kwamba ukitaka kukua, usishushe bei ya umeme, bali ubaki vile vile ili yale mapato yatumike kujenga miundombinu na kuendelea kuzalisha umeme

NIONAVYO MIMI:
maharage ametuchukulia sisi watanzania watu wa kupandishiwa tu bei! ni mtu asiyejali hali ya wananchi! hajui kama hilo Bwawa litashusha gharama za uendeshaji kwenye mafuta huko na SONGAS then ndio itumike kufanya mambo mengine:

Watanzania wanataka unafuu wa maisha halafu huyu mpuuzi aliyenogewa hela za walala hoi anakula na kuvimbiwa maharage yake analeta ujinga huu! Sijui ndio akili ya makamba?

No wonder wanatamani kupunguza wafanyakaz wakati Tanesco yenyewe haina watu wa kutosha
Naunga mkono hoja ya Chande,ila wajinga sawa na yule Rais wao asiyejielewa watabisha na mara zote hubisha bila hoja
 
Jiwe alivyowaambia mtamkumbuka wengi hamkumuelewa. Sasa tutaelewana tu.
 
Back
Top Bottom