Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Huo ndio ukweli japokuwa unauma. Na ni lazima usemwe ili usikike. TANESCO ni shirika ambalo kila mtu anataka limhudumie bila ya kuangalia lenyewe nani analihudumia.
Wanataka vya bure,sijui at expenses za nani,hakuna kitu kama hicho.

Ndio maana namkubali Samia, amesema wamachinga wapangwe Ili wachangie uchumi wa Nchi,hakuna kupepesa macho kutafutwa kupendwa kinafiki..
 
Tanesco hawajawahi eleweka wanataka Nn nchi hii... kiangazi kwao tatizo... masika kwa tatizo... gas kwao tatizo... hydropower tatizo... mnataka nini enyi kizazi cha michongo ? 10%

Leo 27,000
Kesho 27,000 sio mchongo ...

Why huyu Mtanzania mnambebesha tu mizigo
Akigeuka Tozo ,bei za vitu kupanda,Petrol juu vyakula juu vifaa vya ujenzi juu

Duh wabongo hii nchi Mna hakika ni yetu ?🤣
Ni yetu mkuu, ndio ukubwa huo. Utotoni ulikuwa unachagua sana chakula Baba yako anakuangaliaaa hakumalizi. Moyoni mwake anakwambia ngoja huyu akue aje ayaone mwenyewe.

Sasa umekuwa mtu mzima, ndio maana ya lile jicho la mzazi wako pale mezani miaka ile wakati wa chakula.
 
Wanataka vya bure,sijui at expenses za nani,hakuna kitu kama hicho.

Ndio maana namkubali Samia, amesema wamachinga wapangwe Ili wachangie uchumi wa Nchi,hakuna kupepesa macho kutafutwa kupendwa kinafiki..
SSH anao mtazamo wa kibiashara tofauti na hayati JPM. Anajua kuwa mwenye duka anapata hasara kwa mmachinga kusimama mbele ya duka lake.

Hiyo ndio faida ya maamuzi ambayo msingi wake ni kumsikiliza kila mtu.
 
Vya bure at expenses za nani?
Kodi tunayolipa, REA tunayokatwa kwenye mafuta na tozo kedekede.
Na miundombinu husika sio ya mwananchi ni ya shirika ila shirika halitaki kugharamia miundombinu yake inayomiliki.

Sisi wananchi tunalihudumia shirika la TANESCO kwa Kodi zetu na haliwezi kujiendesha kwasababu haliwezi kufanya biashara bado liko kutoa huduma.

Sisi wananchi tunajenga bwawa la Nyerere na baadae TANESCO watachukua umeme pale.

Yafaa kuunganishiwa umeme bure kabisa la sihivyo wananchi wapewe uhuru wa kununua nguzo na nyaya zenye ubora na vifaa vingine TANESCO wafike kukagua ubora wa vifaa na kumfungia mteja, akichoka kutumia umeme awaite TANESCO wamsaidie kutoa vifaa vyake akauze.

Sasa hivi hata wasema mteja analipa milioni tano bado kuunganishiwa umeme itapaswa ufuatilie mpaka uchoke na utajibiwa hakuna vifaa jibu rahisi kabisa.

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
Watanzania walilishwa matango, huwezi kupata umeme wa 27000! Hiyo ni bei ya bati Moja
 
Umeme uingie bure ndani ya nyumba, yaani wiring nyaya zangu Alafu nguzo ipo uwanjani kwangu kuingiza ndani kwa wire wa TANESCO kama mita 5,tu wanataka nilipe laki 5 ya nn? Hivi shirika la umeme linapata hasara kivipi? Yaani waibe wao alafu wasingizie bei ya 27,000 ndio chanzo. Mama Amina sana Tanesco hawa
Ndio ujinga ww viojgozi wetu kufikiria 27000 kama ada eti ni ndogo .wakati hata wakifunga bure ndani ya miezi 6 na wakakata hata shilingi 5/ unit wwnawezakukusanya fedha ya maana kabisa wasubiri 24

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikiliza huyu mkurugenzi nikabaki nimeduwaa. Hivi concept ya serikali kusambaza umeme ikoje? Nilidhani kwamba gharama za kuunganisha zingekuwa as minimum as possible ili waunganishe wateja wengi halafu fedha zirudi kwa kuuza units za umeme. Ndiyo maana makampuni ya simu yanatafuta yenyewe fedha kwa ajili ya infrastructure installation (kuweka minara na vituo kadhaa then returns zao wanazipata kutoka kwa wateja kupitia airtime, msg na miamala.
Viongozi wetu kichwani wanamakamasi nakuhakikishia eti huyo ni mkurugunzi wa shirika kubwa la umeme anatefemea 27000 badlala ya kutegemea mauzo ya unit za umeme ambazo ndo kwenye faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kiuhalisia hiyo bei ni hasara kwa shirika
Nimefuatilia huo mjadala, jamaa ni mzuri asipoingiliwa na siasa.
Kwa namna moja ama nyingine tena kwa akili sana amewananga wanasiasa.
Akipewa miaka 3 shirika litakuwa bora sana.
Jamaa ni mzuri kiliko Makamba mara 100
 
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
Nchi ngumu sana hii. Jamaa nae anahisi alivumilia sana lawama sasa ndio kaamua kujotokeza kuusema anaohisi ni ukweli!!

Kupanga ni kuchagua na bwana maharage anapaswa kujua umeme ni sawa na huduma nyingine za jamii km ilivyo maji,barabara,afya,elimu n.k.Public goods...

Sio 27,000 tu inaweza kuwa bila malipo ya moja kwa moja toka kwa mteja(wao huita bure) ni sehemu ya majukumu na wajibu wa serikali ya kufanya mgao wa keki ya taifa kwa wananchi wake.

Maharage anasahau mchango wa nishati ya umeme ktk mawndeleo ya jamii/taifa? Maharage anaangalia pato moja kwa moja wanalotakiwa kupata toka kwa walaji wa huduma. Hii sio sahihii.

Ushauri kwa maharage:
Aishauri serikali iondokane na Shana ya kuendesha ahirika kwa hasara Bali ajenge hoja ya serikali kutoa ruzuku stahili iatakayokidhi mahitaji ya shirika katika kuwapatia wananchi wake bila kupata kipato cha moja kwa moja.

Kwani serikalili inawezaje kwenye elimu na inashindwaje kwenye umeme na huduma nyingine nafuu kwa umma..!??? Serikali napata shilingi ngapi inapotoa huduma ya elimu ya msingi,swkondari na vyuo vya kati kwa wanachoita BUREE(KODI ZETU)??!!

MAHARAGE.. Jenga hoja kuliko kukariri kwamba lazima iwe hivyo. Mafuta ya taa yalipandishwa bei kuepuka uchakachuaji wa mafuta,watumiaji wa mafuta yabtaa ni watanzania halisi, Mlipolazimisha wapinzani akiwemo Zito kabwe wakajenga hoja km mkipitisha kupandisha bei ya mafuta ya taa basi kiasi cha ziada kiende REA....ili hiki unachokiita 27,000/ kisitokee....Leo Maharage unataka kutuambia nini? daahh kanchi kagumu sana sana haka
 
Bila mchanganuo wala maneno ya lugha ya kigeni, inawezekana! Haya tuanze na REA, wanapata wapi pesa za kulipana mishahara na gharama za uendeshaji wa hilo lishirika?

Kila mtumiaji wa umeme, anaichangia REA 1% ya manunuzi yake ya umeme, ni kiasi gani kinakusanywa kwa mwezi?

Znz wao wanaweza vipi kushusha gharama hizo? Wanaweza vipi kutumia umeme wasiolipia hata sumni?

Anzia generation mpaka distribution kunielewesha mkuu!
Tanesco haijapata MTU au ni mradi wa watu flani,au imeachiwa iendeshwe kisiasa....ila hili LA hujuma laweza kuwa sahihi..haiwezeiani kila kukicha tanesco ni majanga.

Kwani walimu,madaktari,vifaa tiba,vifaa vya kufundishaia n.k. vinagaramiwa na nani?

Nafikiri ni wakati muafaka sasa Siri-kali ituambie vizuri nini kipo nyuma ya swala la nishati ya umeme.

Lakini wanazuoni ni wakati wetu pia kufukunyua zaidi kwa kuitazama historia ya sekta hii ya nishati ya umeme kwa hapa Tanzania,Afrika na duniani kote, tuitazame miradi na huduma hii kwa mapana yake ili kubaini mchawi na tatizo lilipo
 
Haina kuremba, asante Kwa kutokubali kupelekeshwa na wanasiasa!
Nguzo 1 shilling ngapi??
Mita 1 ya waya shilling ngapi??
Mita ya LUKU shilling ngapi??

Leo wadanganyika tunaamini tunaweza kuunganishwa Kwa 27,000??

Hili halipingiki, gharama lazima zibalansi ili kupunguza mzigo serikali WA kuliendesha shirika.
 
Kama ndio hivyo ziruhusiwe kampuni binafsi kushindana kusambaza nguzo, waya na Luku, TANESCO kazi yao iwe ukaguzi, kuwasha na kuzima umeme.
 
Back
Top Bottom