Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,877
- 2,314
Kwani mahari ni kuwauza? Mbona basi hela ndogo sana. Mwanadamu anauzwa kwa thamani ya hizi mahari tunazotoa kweli?Uzuri hailazimishwi, ukishindwa unaachana nayo.
Sina hakika sana kama mwanaume aliyetimia sawasawa akishindwa kutimiza utaratibu wa kuoa anawezaje kuwajibika kwa familia?
Kuoa sio kuwa na uwezo wa kudindisha. Kuoa ni zaidi ya majukumu ya kifamilia.
Mwenyezi Mungu akujaalie watoto wa kike uwakuze wakifika wakati wa kuolewa wagawe bure bure tu.
Kwanza imekaa kitamaduni zaidi. Kuna baadhi anaelipa mahari ni familia ya kikeni. Wengine anaetamka mahari ni mtoto wa kike mwenyewe. Anatamka chochote atakacho, hata smart kitochi akiamua.
Watu tu siku hizi wanakiuka maadili, wanamtajia kijana pesa au vitu visivyoendana na uwezo wa kijana au familia ya kijana.