Unamaanisha nini kusema "ualisia" wa kibinadamu?
Mimi nasema katika Uislam, mahari ukiangalia maana yake na mafundisho kuhusiana nayo kisha ukaangalia mafundisho na Sharia kuhusu Ibada nzima ya ndoa, mahari sio biashara ya utumwa.
Sijui kwenu mahari ni nini. Lakini katika Uislam mahari ni zawadi anayopewa mwanamke na mwanaume anayetaka kumuoa ili kuonesha ukweli wa kutaka kwake kumuoa na ni jambo la wajibu lililowekwa na Allah katika Qur'an kama haki ya mwanamke. Na haisihi ndoa katika Uislam bila ya mahari.
وآ توا النساء صدقاتهن نحلة
“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)
يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن
“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)
فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة
“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)
Na mahari haina kiwango maalum ni makubaliano ya wao wawili (akitaja mwanamke au mwanaume aki offer kisha mwanamke akakubali kwa hiyari yake) na ni haki ya mwanamke mwenyewe sio wazazi au walezi. Inaweza kuwa Mali au jambo jengine. Sio pesa tu na ng'ombe. Inaweza kuwa ni vitu mbali mbali kulingana na ada na makubaliano. Na ni mwanamke mwenyewe ndie anataja na kuridhia. Na ikapendekezwa mahari iwe ndogo
Kuna ambao wanatoa Pete kama mahari, kuna ambao walioa na mahari yao ilikuwa ni kile walichokihifadhi katika Qur'an (yaani kiwango walichohifadhi katika Qur'an ) ndio ilikuwa mahari nk.
Ngoja nikupe mfano mmoja tu kutoka zama za Mtume kukuonesha; wakati wa Mtume(SwallaAllahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) kulikuwa na Swahaba anaitwa Abu Talha (Radhwiya Allahu 'Anhu), Abu Talha alitaka kumuoa Umm Sulaym (Radhwiya Allahu 'Anha), lakini wakati Abu Talha anamposa Umm Sulaym, alikuwa sio Muislam. Umm Sulaym akamuambia Abu Talha; "Wa Allahi, mtu mfano wako harejeshwi, ila wewe sio muislam na mimi ni muislam, na haiwi halali kwangu kuolewa nawe, ukisilimu hiyo ndio mahari yangu na sitotaka kengine zaidi ya hilo". Abu Talha akasilimu na kule kusilimu kwake ndio ikawa ni mahari ya Umm Sulaym (Allah awe radhi nao wote wawili).
Kuna ambao mahari waliyoiridhia ilikuwa ni viatu (ndala mbili) kama yule mwanamke kutoka kabila la Bani Fazara na Mtume akamuuliza kama ameridhia hilo, akamjibu kuwa karidhia.
Sijui nikufafanulieje mimi sio fasaha sana, ila elewa kuwa katika Uislam mahari ni tofauti na unavyoelewa wewe.
Kazakh destroyer
Allah anajua zaidi.