Mahekalu ya maaskofu kufuru

Mahekalu ya maaskofu kufuru

Sema wewe Mzizimkuu ulichopost sio ulichotaka una kitu cha ziada kimnakukereketa na kita kuuawa usipokitoa nimeshaangalia post zako inapokuja suala la religion.
 
Kama wana Devote their life time.. entire day kuhudumia kanisa kupunguza vibaka,wazinzi na kufundisha watu kumjua Mungu, they Deserve More than that...

Anayeona ni rahisi kukusanya sadaka za waumini aanzishe kanisa lake aone kama atafikisha hata waumini kumi.

Asante mama

Tell them
 
Hawa jamaa unafikiri wanaelewa wao wanamjua Yesu ni yule wa kwenye picha ya maigizo tehetehe Yesu Kristo wa Nazarethi hakuhitaji cash maana alikuwa akiita chochote akitakacho kinatokea kwenye njaa akaomba samaki na mikate wakala maelfu mpaka kusaza,hakuhitaji meli maana juu ya maji alitembea,hakuhitaji ndege wala gari ndo maana ilipofika saa ya kwenda Mbinguni alipaa tu.
na ndiyo mwanaume pekee aliyekufa akafufuka na atarudi tena wengine wote udongo umeshawatafuna na hata mimi utanitafuna ila huyu mwanaume udongo wenyewe ulimtapika.

Asante
U made my day mr
 
...LOOOH..!! nimeipenda sana hii, hakika Mungu wetu anabariki, hongereni maaskofu kwa kuonyesha kwa vitendo kazi za Mungu aliye hai...

Amen
We a leading
Na.ndo kanisa linavyotakiw liwe
 
Asante
U made my day mr

pamoja christine hata hivyo jamaa wamizimika kama mshumaa ghafla.

kama Yesu wa Nazarethi hangekuwa tajiri asingesema tuombe lolote atatupa maana angefafanua isipokuwa fedha,lakini Nchi na vyoote viijazavyo ni mali ya Bwana,ndiyo maana tunakuja uchi tukifa tunamuachia Mungu mali zake tunarudi tena mikono mitupu.
 
Kupata mali siyo dhambi maana neno lanena Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na mengine yote mtazidishiwa.
Na wala umaskini siyo utakatifu.Vipi hebu tupe na data za Mashehe.
Masheikh hawana utajiri kabisa hakuna Sheikh Tajiri katika Uislam ni Dini kutafuta kesho pepo kwa wenzetu wakristo Pepo yao ipo hapa hapa Duniani. Kama alivyosema Bwana Yesu

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
 
Hapa Yesu Kristo wa Nazarethi Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme alimaanisha ni vigumu sana wenye kutegemea mali kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.Mbona Ibrahimua likuwa tajiri wa fedha,dhahabu nk.,Mfalme Suelemani aliyekuwa tajiri na hatatokea tajiri kama huyo yeye hata vyombo vya kulia ilikuwa dhahabu.
Nenda tena kaisome Biblia tena inaonyesha wewe huijuwi kuisoma vizuri Biblia Nabii Ibrahimu hakuwa ni Myahudi wala Nabii Suleyman hakuwa Myahudi wala Mkristo hawa wawili walikuwepo kabla ya kuja Bwana Yesu. Kaisome vizuri Biblia usikurupe kusema maneno huna uhakika nayo.
 
Sema wewe Mzizimkuu ulichopost sio ulichotaka una kitu cha ziada kimnakukereketa na kita kuuawa usipokitoa nimeshaangalia post zako inapokuja suala la religion.
Huwa ninapenda kusema ukweli ingawa wewe utachukia lakini ukweli nitasema mpaka siku yangu ya mwisho.

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
 
Masheikh hawana utajiri kabisa hakuna Sheikh Tajiri katika Uislam ni Dini kutafuta kesho pepo kwa wenzetu wakristo Pepo yao ipo hapa hapa Duniani. Kama alivyosema Bwana Yesu

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."

Maandiko kuyaelewa ni vigumu ndiyo maana anahitajika Roho mtakatifu kufundisha wanafunzi wa Yesu walimwendea wakamwambia tazama tumeacha ndugu na jamaa tutapata nini? akawambia mtazidishiwa mara mia katika ulimwengu huu na baadaye kurithi uzima wa milele.

Na akawambia utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo yote mtazidishiwa,neno halipingani ila wewe unatafsiri tofauti.
na sehemu nyingine inasema Vinavyotamaniwa na mataifa vitawaijia.

Kusema mashehe hawana utajiri basi mungu wenu habariki sasa huyu wa Wakristo anabariki poleni sana maana umaskini siyo tiketi ya kumuona Mungu bali utakatifu.
 
Nenda tena kaisome Biblia tena inaonyesha wewe huijuwi kuisoma vizuri Biblia Nabii Ibrahimu hakuwa ni Myahudi wala Nabii Suleyman hakuwa Myahudi wala Mkristo hawa wawili walikuwepo kabla ya kuja Bwana Yesu. Kaisome vizuri Biblia usikurupe kusema maneno huna uhakika nayo.

Hata mimi sijasema walikuwepo kabla ya Yesu duniani nilitaka kukuonyesha jinsi Mungu wa Mbingu na Nchi anabariki,nani alikuambia Yesu ni kwa wayahudi hujasoma alikuja kuchukua dhambi za ulimwengu siyo? na neema kuwageukia mataifa hujasoma?
 
Watanzania wana safari ndefu.Hizo nyumba za kawaida kabisaaa
Nyie ni wadaku kweli,
mnashangaa hivyo vijumba vidogo vidogo hii inaonyesha kuwa Watanzania
wengi wana fikra za kimaskini na wivu. Mbona hamshangai maghorofa
yaliyojengwa MASAKI, MIKOCHENI, MBEZI BEACH nk, tafuteni pesa nanyi
mkajenge kama hizo au nanyi kaanzishe makanisa mpate sadaka
hizo.
 
Mbona nyumba za kawaida sana?? Ipi hapo inakaribia sifa ya kuitwa hekalu???

Au wanaficha sadaka Uswizi??
 
Hata mimi sijasema walikuwepo kabla ya Yesu duniani nilitaka kukuonyesha jinsi Mungu wa Mbingu na Nchi anabariki,nani alikuambia Yesu ni kwa wayahudi hujasoma alikuja kuchukua dhambi za ulimwengu siyo? na neema kuwageukia mataifa hujasoma?


YESU KRISTO HAKUTUMWA KWA WATU WOTE

Yesu Kristo anasema; "Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua Torati au Manabii, la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana nawaambieni, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja na nukta moja ya Torati haitaondoka mpaka yote yatimie (Mathayo 5:18-18)"

Ni dhahiri kuwa Nabii Musa na manabii wengine watiotangulia walkuja kuwafundisha na kuwaongoza Waisraeli tu. Yesu Kristo amekwisha kubali katika maneno ya juu ya kuwa amekuja kulitimiza kusudi lile ile ya Musa na Manabii wengine waliotangulia.


Lakini tunaona mapadri wamekwisha fika katika kila sehemu ya dunia hata Afrika ijapokuwa Yesu Kristo mwenyewe hakuwa na nia na kusudi ya namna hii kabisa. Sasa swali hasa linalotakiwa kufikiriwa, si Wakristo wanafanya nini, bali ni, "Je, Yesu Kristo alikuwa na nia na azimio gani?" Mwenyezi Mungu alikuwa na kusudi gani alipomtuma Yesu Kristo? Jambo hili haliwezekani kuelezwa kwa njia nzuri na yeyote isipokuwa lielezwe na Yesu Kristo mwenyewe. Na Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24). Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoka kilichopotea (Matt. 18:11)."


Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa. Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa, Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia. "Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"


Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa. Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:

"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19). ‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24). "Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26) "Sio haya tu bali pia tunasoma, "Hawa thenashara Yesu

aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""

Kutoka kwa mafungu ya maneno haya ni kuwa wafuasi wake wameamrishwa naye kupeleka ujumbe wake kwa mataifa yote ya Israeli si mataifa yote ya ulimwenguni. Mtu asidhani ya kwamba mawazo ya maneno yajuuni kuwa waende kwanza miji ya Waisraeli na baadaye kwenye miji mingine. La, maana kwenda kwa kondoo waliopotea wa Israeli si maana yake kuvitazama vijiji tu, bali ni kuwaingiza katika dini ya Ukristo. Basi kwa hakika maana hasa ya maneno haya ni kuwa Waisraeli wote waingie katika Ukristo, Mkristo na padri ye yote asijielekeze kabisa kwenye mataifa mengine.

Yesu Kristo amehakikisha wazi wazi ya kuwa kazi ya kuwahubiria dini Waisraeli na kuwaingiza katika njia yake haitamalizika mpaka kufika kwake mara ya pili, kama ilivyosema:

"Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza mji yote ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu (Matt.10:23). "Katika maneno haya inajulikana wazi ya kuwa yaliyosemwa katika Mathayo (28:19) makusudio yake ni kwamba wahubiri Wakristo wasimamishe Ukristo katika miji ya Israeli na waingize kabila la Israeli katika dini yao si kuvitembelea tu na kuvitazama vijiji vya Waisraeli. Na pia ni wazi ya kuwa kazi hii ya

kuhubiri na kuwaingizia haitamalizika mpaka Yesu Kristo aje mara ya pili. Kwa hiyo kuwahubiri watu wengine wasio katika mataifa ya Israeli ni kinyume kabisa na mafundisho na maagizo ya Yesu Kristo. Hata mitume wa Yesu pia walifahamu kuwa ni kosa kuwahubiri watu wengine wasio Waisraeli. Tunasoma:


Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu.

"Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shida iliyotokea kwa habari ya Stefano wakasafiri hata Foiniki na Kupro na Antiokia. Wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao!! (matendo11:19)." Hivyo, mitume wa Yesu waliposikia ya kuwa Petro aliwahubiri watu wasio Israeli pahali fulani, wakakasirikia nawakashindana naye:
"Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakishindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao" (Matendo 11:2-3)",

Kwa neno zima kabla ya Mtume wetu Muhammad (saw) hakuna nabii au mtume ye yote aliyeamrishwa na Mwenyezi Mungu kuwahubiri watu wote wa ulimwengu mafundisho yake. Wao walikuwa wanatumwa kwa makabila maalumu na miji kadha wa kadha. Wala hakuna dalili yoyote ihakikishayo ya kuwa Yesu Kristo alitumwa kwa makabila yote ya dunia nzima wala hakuna ishara idhihirishayo ya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wanafunzi wake kuwahubiri watu wa ulimwengu mzima isipokuwa alisema:


"Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt.15:24)," Mapadri wanaofanya kazi ya kuhubiri dini ya Ukristo katika Waafrika na watu wengine wasio Israeli kwa hakika wanafanya kinyume cha maagizo ya Yesu Kristo ? Naam, Mtume Muhammad (saw) kwa amri ya Mwenyezi Mungu alisema: "Enyi watu wote! Kwa hakika mimi ni Mjumbe wa haki niliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwenu nyote" (Kurani 7:159).
 
Masheikh hawana utajiri kabisa hakuna Sheikh Tajiri katika Uislam ni Dini kutafuta kesho pepo kwa wenzetu wakristo Pepo yao ipo hapa hapa Duniani. Kama alivyosema Bwana Yesu

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, “Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.”

utajiri wa mashehe unajurikana ni kununu majini mengi na kuyafuga ndio furaha yao,wakati hawa maaskofu ni matajiri wa magari na majengo,so mashehe wana utajiri usoonekana kwa macho haya ya kawaida
 
mungu si wa watu masikini. mungu ni wamatajiri pekee
 
Kondoo wanachunwa hela hatari hata hawastuki,,,,mtu kaanza na kupanda daladala after 1year anaPush Range Rover na Hummer3 teh teh teh teh


Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
Huwa ninapenda kusema ukweli ingawa wewe utachukia lakini ukweli nitasema mpaka siku yangu ya mwisho.

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, "Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni."
Hapo umechukua mstari 1 na biblia haina mstari mmoja wa ufalme wa mbingu na utajiri wa dunia.Sababu mbinguni hawataingia maskini tuu bwana Mzizimkavu.Utateseka duniani na mbinguni pia huendendi.Ndiyo hivyo hivyo hayo mahekalu ya maaskofu sio kigezo cha kuwa watenda dhambi.Hapo unahukumu.
 
Back
Top Bottom