Uchaguzi 2020 Mahera (NEC) na Nyahoza (Naibu Msajili wa Vyama), kwanini hamkujipanga kabla ya kuonesha sinema yenu?

Uchaguzi 2020 Mahera (NEC) na Nyahoza (Naibu Msajili wa Vyama), kwanini hamkujipanga kabla ya kuonesha sinema yenu?

Mahera na nyahoza walishapanga mshindi wao mfukoni shida Ni nyomi la Lisu limewasambaratisha kabisa, watamtangaza vipi mgombea wao? Huku Kuna macho ya watz kule Robert Amsterdam anaangalia kila kitu. Lisu sio Lowasa tendeni haki ili msiende the Hague
 
Yaani huyu jamaa JIWE ananisikitisha sana,juu ya kupiga magoti kwa ajili ya kuomba kura..vipaumbele vyake bado ni vile vile habadiriki...atleast ange change gear angani kwa kuacha kunadi mambo ya madege sijui viwanja vya ndege n.k

Angejikita kwenye Afya
Maslai ya wafanyakazi
Mafao- ikiwemo kurudisha fao la kujitoa
Kuwajali wakulima na wavuvi
Kuondoa tozo za hovyo hovyo n.k

Hivi ile sera ya viwanda imekufia wapi?? Yaani nikikumbuka wakina mwijage walifikia kusema cherehani 4 ni kiwanda [emoji3][emoji3][emoji3] asee Viongozi wa Tanzania hawapo serious kwenye kuendesha nchi.
Umewahi ona wapi duniani dikteta anashughulika na maendeleo ya watu
 
Wadogo zangu Dr.Mahera na Nyahoza mmeniangusha sana. Nia ya kukisaidia chama chetu cha CCM mnayo. Uwezo mnao. Nguvu mnazo. Kwanini hamna maarifa? Dr. Mahera umejitokeza mbele ya watanzania na kuhabarisha kuwa mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu amekiuka Kanuni za Maadili ya Uchaguzi. Ukasema kuwa una nguvu na mamlaka ya kushughulika na hilo. Ukatamba kuwa tayari 'umeshamlima' Lissu barua ajitokeze mbele ya Kamati ya Taifa ya Maadili ya Uchaguzi.

Dr. Mahera ukada wa CCM na 'ushushushu' ukakuumbua. Ukakusukuma kusema visivyotakiwa kusemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC inayosimamia uchaguzi husika. Ukamwaga sera za CCM na kuzikosoa waziwazi sera za Lissu. Ukakosoa na kuonesha Lissu anakosea bila ushahidi wowote wa maana zaidi ya kufokafoka. Ukashindwa kujizuia kabisa. Ukashindwa kuficha hisia zako dhidi ya Lissu huku ukimuunga mkono Dkt. Magufuli. Umeshindwa kabla ya kuanza!

Ndugu Nyahoza nawe umeningusha. Baada ya mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza kumwandikia barua Lissu, nawe jana ukapeleka barua kwa bodaboda CHADEMA. Ni barua ile ile ya Mkurugenzi au nawe umepandishia barua juu ya barua ili kumtinga Lissu na barua? Nawaambia ukweli, Dr. Mahera na Nyahoza hamkujipanga na kupangika. Muda huu wa kampeni, mbinu zinapaswa kuwa zilizopangika kimyakimya. Si hila za wazi kama zenu.

Hivi, Dkt. Magufuli wa CCM, tangu kuanza kwa kampeni zake, hakuwahi kuvunja Maadili ya Uchaguzi au yale ya vyama vya siasa? Mnatazamwa, mnafikiriwa. Watanzania si wajinga, nao wanaweza kutafakari na kung'amua. Kwa maneno na matendo yenu: Dr. Mahera na Nyahoza, jambo lolote dhidi ya Lissu ni batili kwakuwa mmeshaamua kabla ya kuitisha hivyo vikao vyenu.

Acheni demokrasia ichukue mkondo wake!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mbeya, Tanzania).
Kisu kimechoma mpaka kwenye mfupa , Hawa watu wawili Mahera na Nyahoza wamedhalilisha sana ofisi za umma , pia wanajidhalilisha Sana wso binafsi .
Screenshot_20200928-121229.png
Screenshot_20200928-221139.png
Screenshot_20200929-105200.png
Screenshot_20200929-105600.png
Screenshot_20200928-153704.png
 
Mahera pamoja na familia yake apigwe ban ya kupewa viza nchi yeyeto duniani, ndie anaekwenda vunja amani yetu.
 
Mahare na nyahoza hata sheria tu za tume awazijui, ndo wataweza mhoji Lisu.
 
Back
Top Bottom