Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Sequence of events:
  1. Suppose Kundi mojawapo katika wanaotaka nafasi hiyo wana mshikamano na Spika.
  2. Halafu mtu wao anateuliwa kuwa makamu wa rais.
  3. Bunge linampitisha kwa kauli moja, anaapishwa kuwa makamu wa rais
  4. Baada ya miezi michache wabunge wanaanza kuhoji ufanisi wa rais.
  5. Hoja ya kutokuwa na imani na rais inaletwa kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba, spika anakubali ijadiliwe, na inapita kwa kauli moja na azimio la bunge kuwa limekosa imani na rais.
  6. Katiba inafuatwa tena, makamu huyo anakuwa rais, anaapishwa, duara linarudi lilipoanzia.
Nyie bisheni.
Kwani nchi si iko mikononi mwao. Shida iko wapi?
 
Shikamoo mzee. Kwahiyo unamaanisha mhimili wa rais ni mtu mmoja tu mzee.
Wewe ndio unadhani urais ni mtu mmoja maana unataka kutuonyesha kwamba hayo yote yakifanyika Rais kalala tu he knows nothing kinachoendelea kule bungeni.
 
Watajuana acha wakatane mapanga sisi tutazika tu.
Mungu atuepushie. Hatutaziweza hizo gharama za misiba ikiwemo kuzungusha maiti mikoa kadhaa, siku mbili za mapumziko, maombolezo siku 21, magwaride ya kurudiarudia, vyombo vyote vya habari kutumia airtime yote kwenye msiba (sijui wanafidiaje lost revenue), vifo vya waombolezaji wanaokanyagana wakigombea fursa ya kuona maiti nk. Hapana, Mungu awajaalie waishi tu.
 
Ile siku wanakaa kikao, wanapelekewa wajeda ili kulinda usalama wao.
Na wengine wanawekwa ndani kwa tuhuma za uhujumu uchumi
Usicheze na mtu aitwaye Amiri jeshi mkuu
Kile kiti cha amiri jeshi ni dhaifu tu endapo jeshi halikutii. Kinyume na hapo hakuna mbunge wala waziri anayeweza kumtoa Rais madarakani kwa mtindo wowote ule ukiondoa kifo au umaututi. Labda raia tena kwa maandamano makubwa sana yanayoambatana na vifo ndio wenye uwezo huo.
 
Mungu atuepushie. Hatutaziweza hizo gharama za misiba ikiwemo kuzungusha maiti mikoa kadhaa, siku mbili za mapumziko, maombolezo siku 21, magwaride ya kurudiarudia, vyombo vyote vya habari kutumia airtime yote kwenye msiba (sijui wanafidiaje lost revenue), vifo vya waombolezaji wanaokanyagana wakigombea fursa ya kuona maiti nk. Hapana, Mungu awajaalie waishi tu.
Sawa tu. Sisi wanyonge hatupungukiwi wala kuongezewa kitu.
 
Marhaba. Isingekuwa hivyo, msingehangaishwa na itakuwaje baada ya Magufuli.
Lazima mahangaiko yawepo kwa sababu hao wengi wakishagongana kimaslahi ni tabu. Na masnitch yanakuwemo humohumo miongoni mwao.
 
Kile kiti cha amiri jeshi ni dhaifu tu endapo jeshi halikutii. Kinyume na hapo hakuna mbunge wala waziri anayeweza kumtoa raisi madarakani kwa mtindo wowote ule ukiondoa kifo au umaututi. Labda raia tena kwa maandamano makubwa sana yanayoambatana na vifo ndo wenye uwezo huo.
Genge la ccm hulijui. Liko backed na wahuni wengine humohumo.kwenye vyombo vinavyoitwa vya dola.
 
Back
Top Bottom