Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Mpaka awahi! Na katiba inasema akivunja bunge uchaguzi unarudiwa. Kama alivyosema "Bwege" (mbunge mmoja wa awamu iliyopita), "ngoma inaanza upyaaaaa". Wasiyemtaka wanamshughulikia huko huko!
Uwezo wa kuwahi anao kwasababu wapo wanaompenda kwenye system na watampenyezea tu taarifa mapema. Anamvua uanachama spika [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Ngoma inaishia hapo.
 
Yaani kama katiba na sheria za bunge zina ruhusu, hata Ndugai ana takiwa aachie nafasi ya uspika aliyo nayo. Huyu spika amelinajisi bunge na sheria kwa maslahi yakena tumbo lake.
 
Mnadai katiba mpya wakati hii iliyopo hamuijui
Siyo kila anayehoji jambo ni mpinzani. Kwa taarifa yako sasa hivi wapinzani wamekaa pembeni kabisa waangalie hili tifu linaloendelea ndani ya CCM. Hii vita ya nafasi ya VP ni ya kwenu wenyewe CCM, wapinzani hawamo na hawawezi kuingilia mambo yenu ya ndani.
 
Ninachokisema vote of no confidence inawezekana na ikafanikiwa na raisi akaondolewa madarakani ilihali bunge likawa limoja raisi anaondolewa wala haihitaji sijui TISS wala sijui Nani nje ya bunge,bunge linadhamana kubwa na mamlaka hayo endapo tu wakiamua
 
Namsifu sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi aliofanya, amewazidi akili wabashiri wote! Dr Philip Mpango ni chaguo sahihi 100%, hayuko katika yale makundi, na zaidi sana ni mtu principled, mchapa kazi, mwenye hekima sana, mpole na mwadilifu. Wataendana vizuri sana na bosi wake. Kwa uteuzi huu, tumepata picha halisi ya mwelekeo anaoutaka Mama, ni mwelekeo mzuri kwa taifa.
Wale waliotaka kumvuruga Mama naamini somo limewaingia, sasa wajirekebishe, watulie, tuendelee kuijenga nchi.
 
Umewaza kiundani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…