Wakuu Lissu ameenda Uganda na nimeona hii Taarifa hapa je ina uhalisia wowote?
- Tunachokijua
- Deogratias Mahinyila ni Mwenyekiti wa baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (BAVICHA) Taifa. Machi 4, 2025 akiwa na viongozi wengine wa baraza hilo alifanya mkutano na waandishi wa habari ukiwa na lengo la kuongelea hali ya usalama kwa vijana Tanzania, ikiwemo kwa katibu mkuu wa BAVICHA mkoa wa Mwanza Amani Manengelo, Februari 14, 2025.
Madai
Kumekuwapo na grafiki ikieleza kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA amesema kuwa fedha alizozifuata Uganda wao kama vijana hawazitaki kwa kuwa hawataki kuwa sehemu ya hiyo dhambi.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayona kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na mkutano aliofanya Mahinyila na waanidshi wa habari umebaini kuwa hakuna mahali ambap mahinyila alimtaja Mwenyekiti wa chama hiko, Tundu Lissu wala safari yake ya kwenda Uganda.
Katika mkutano huo Mahinyila alizunguzmia hali ya usalama wa vijana wa Tanzania, tukio la kutekwa kwa Amani Manengelo pamoja na mapendekezo yao juu ya kile kinachotakiwa kufanyika dhidi ya suala la utekaji hususan kwa vijana.
Aidha kuhusu safari ya Lissu, Chama kilitoa barua Machi 3, 2025 na kueleza kuwa Mwenyekiti wa Chama hiko ameeleka Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na akiwa huko atashiriki kongamano litakalowashirikisha vyama rafiki vya demokrasia kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na barua hakuna mahali ilielekeza kuwa Lissu anaenda kuchukua hela akiwa huko.
Pia grafiki na taarifa hiyo haijachapishwa na Jambo TV kama inavyoonekana