Mahitaji ya watu wa mikoa ya kaskazini ni barabara za lami, reli na mipango miji na sio umeme kutoka Ethiopia!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Mikoa ya kaskazini imekuwa na umeme tangu zamani. Kwa mfano Kilimanjaro kila kijiji kimeunganishwa na gridi ya Taifa.

Kama rais Samia anatafuta kitu cha kuwafanyia watu wa mikoa ya kaskazini basi afanye haya:
1. Barabara za lami
2. Reli ya mpya (SGR)
3. Mipango miji
4. Viwanda
Kusema ataleta umeme maalumu kwa watu wa kaskazini ni hadaa tupu.
 
tuna vyanzo vingi vya kufua umeme sehemu ambazo kuna upepo mwingi.

Ila kwa vile ccm bado inafanya yale kila ikifika uchaguzi ndio inaleta jambo wakati haya mambo tulitakiwa tusiwe tunajadili shida ya umeme,barabara na mengine tuwe tunajadili kwa nini Thamani yetu ya pesa inashuka wakati bidhaa tunazo au maendeleo na kukabiliana na dunia
IMG_0816.jpeg
 
Umeme hauji na label.., watawapa wa Rufiji halafu watasema umetoka Ethiopia wapige pesa
 
Pesa za mauzo ziko wapi?
Siri ya kambi umeambiwa wanafanya biashara ya kanisa kila baada ya misa wanatangaza wamekusanya sadaka kiasi gani, hizo Siri ndio maana wanaapa mbele alichokiita kijitabu kwamba watatunza Siri ila ni ngumu sana kwa mwmke kutunza Siri lazima zivuje
 
Duuh…, hata sina la kusema aisee.., mbona nchi itakuja kupinduliwa hii, kwamba Kauza bwawa?! Nakataa hili..
 
Defence mechanism unaelewa maana yake? Rejea kauli za Mawaziri akiwemo PM kuhusu umeme wa lile Bwawa kisha fanya calculation
 
Mikoa ya kaskazini imekuwa na umeme tangu zamani. Kwa mfano Kilimanjaro kila kijiji kimeunganishwa na gridi ya Taifa.

Kama rais Samia anatafuta kitu cha kuwafanyia watu wa mikoa ya kaskazini basi afanye haya:
1. Barabara za lami
2. Reli ya mpya (SGR)
3. Mipango miji
4. Viwanda
Kusema ataleta umeme maalumu kwa watu wa kaskazini ni hadaa tupu.
Kwani lami hazipo?
Viwanda havipo?

Utampangaje Masai na mang'ati?

Reli Iko mbioni
 
Back
Top Bottom