Mahmoud Ahmadnejad: Rais aliyekataa mshahara mkubwa na kuendelea kupokea mshahara wa mwalimu na kurudi na kufundisha baada ya miaka 8 ya urais

Mwanaume Aliyeitawala Iran kwa Miaka 8 akiingia kwenye Basi kwenda Kazini kama mwalimu, kazi yake kabla hajawa rais.

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, ambaye aliongoza taifa la Iran kwa miaka 8, sasa anafanya kazi kama mwalimu.

Picha ya Ahmadinejad akitumia usafiri wa umma ilionekana kwenye mtandao wa kijamii. Rejea ilitolewa chini ya picha kwamba katika kipindi cha miaka 8 ya uongozi wake Ahmadinejad hakupokea hata mshahara wa rial kutoka kwa bajeti ya serikali, akiishi kwa mshahara wa mwalimu. Wakati wa urais wake, hakuanzisha sheria ya urais wa zamani ili kupokea pensheni kubwa. Alirudi kufundisha tena, na kama unavyoona, anapanda basi kwenda kazini.

Hebu fikiria Rais wa zamani kujiunga na usafiri wa uma, yani kupanda dala dala tena akikosa seat anasimama na wala haoni shida. Na je vipi kwetu Africa tunaweza kupata kiongozi wa namna hii ?! Africa yetu hii kwa kina Mobutu waliojichimbiaga mahandaki yenye azina ya mabillion ya fedha.

(inasemekana Mobutu alikua na hazina na Trillion 8 ndani acha fedha alizojiwekea kwenye mabenki ya nje kama Finland, Malaysia, Canada nk)

View attachment 2625170
Itashangaza kwa watu wenye poverty mentality iliyojengwa na wazungu ambao mnawasujudia.

Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye siasa na uongozi ktk mashariki ya kati na bara arabu.

Waliokwenda Qatar ni mashuhuda
 
Mkuu una ubishi usio kuwa na msingi wowote.
Kwahilo anabisha bure ila labda hajasikia tusimlaumu
Sijawahi sikia popote Iran imefika enrichment ya 90% ya Uranium. Ukifika enrichment hiyo unatengeneza nuclear warhead, sasa Iran ina nukes?
Vikwazo viliizidia nguvu kiuchumi ikapunguza enrichment ikafanya mazungumzo baadae taratibu ikaanza kuongeza na haijulikani imefikia hatua gani maana imefukuza wataalamu wa shirika la atomiki duniani, sijajua kama wamekwisharudi. Kwa sasa taarifa za nyuklia za Iran ni zile zinatolewa na serikali, au zile za kijasusi kutoka Israel ila sio shirika la atomiki.
Na inasemekana enrichment iliwahi fika about 80%.

Hakuna sababu ya kusema Ahmadinejad alifika 90% alafu hadi leo Iran haina nukes. Siku Iran ikifika hizo percentage inaunganisha moja kwa moja na kutengeneza warhead sio kusubiri kinu kishambuliwe au vikwazo maradufu viongezwe. Hiyo ni point of no return
MKUU hata IAEA kwenye ripoti zao walitangaza kama jamaa kafikia hizo 90 kwenye kurutibisha
Binafsi nitakua mtu wa mwisho kuamini kama IRAN [emoji1130] hawana nyuk maana Israel [emoji1134] wangekua washawafanyia ushenzi wao
 
  • Thanks
Reactions: ITR
Pole pole wakuu siku mtasikia jamaa huyo ni agent wa MOSSAD tena hizo allegations tusishangae zikitolewa na wa IRAN wenyewe. Sura na muonekana wa hawa wa IRAN ni copyright na wazayuni wa Islaer achilia mbali tamaduni nyingine nying wanafanana. Iran na wahayudi wengi sana
TOFAUTISHA wa i
Israel Na WAZAYUNI. UZAYUNI ni itikadi ya kisiasa haina tofauti na Colonialism na sio muonekana wa mtu.
 
Kwahilo anabisha bure ila labda hajasikia tusimlaumuMKUU hata IAEA kwenye ripoti zao walitangaza kama jamaa kafikia hizo 90 kwenye kurutibisha
Binafsi nitakua mtu wa mwisho kuamini kama IRAN [emoji1130] hawana nyuk maana Israel [emoji1134] wangekua washawafanyia ushenzi wao
Leta hiyo report ya IAEA inayosema Iran wamefanya enrichment ya 90%.
Huwezi fika 90% alafu ukakosa nukes, sasa Iran wamefika lini. Nasubiri source
 
Mkuu una ubishi usio kuwa na msingi wowote.
Msiwe mnajitungia maneno mkikataliwa mnakimbilia kuwaita watu wabishi. Wewe ambaye sio mbishi leta hapa IAEA, Mossad, CIA, Iran, Russia au trusted source yeyote yule lini kasema Iran imefika enrichment ya 90%.

Kwanini mnapenda tantalila nyingi wakati ni suala la kuleta evidence. Unapinga as if hapa tunabishana umri wako ambao wewe ndio unastahili uujue kuliko sisi.
 
Ila Iran iliharibiwa tu kuwekwa chini ya sheria za hovyo za kiislamu,

Isingekuwa hivyo ingekuwa nchi tamu sana
 
Ingekuwa kama Uturuki, ndio maana Waturuki ukitaka wakuchape makofi waambie hizo sheria
 
Unawaona hao wenye suti?
Mwanaume Aliyeitawala Iran kwa Miaka 8 akiingia kwenye Basi kwenda Kazini kama mwalimu, kazi yake kabla hajawa rais.

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, ambaye aliongoza taifa la Iran kwa miaka 8, sasa anafanya kazi kama mwalimu.

Picha ya Ahmadinejad akitumia usafiri wa umma ilionekana kwenye mtandao wa kijamii. Rejea ilitolewa chini ya picha kwamba katika kipindi cha miaka 8 ya uongozi wake Ahmadinejad hakupokea hata mshahara wa rial kutoka kwa bajeti ya serikali, akiishi kwa mshahara wa mwalimu. Wakati wa urais wake, hakuanzisha sheria ya urais wa zamani ili kupokea pensheni kubwa. Alirudi kufundisha tena, na kama unavyoona, anapanda basi kwenda kazini.

Hebu fikiria Rais wa zamani kujiunga na usafiri wa uma, yani kupanda dala dala tena akikosa seat anasimama na wala haoni shida. Na je vipi kwetu Africa tunaweza kupata kiongozi wa namna hii ?! Africa yetu hii kwa kina Mobutu waliojichimbiaga mahandaki yenye azina ya mabillion ya fedha.

(inasemekana Mobutu alikua na hazina na Trillion 8 ndani acha fedha alizojiwekea kwenye mabenki ya nje kama Finland, Malaysia, Canada nk)

View attachment 2625170
Hilo gari katika picha si basi la umma hilo ni bus linalotumika kusafirisha abiria airport, na hao waliomzunguka ni walinzi wake.
Hiyo picha ilipigwa mwaka 2014, mwaka mmoja tangu alipomaliza uongozi wake kwa nafasi ya urais. Ilipotolewa in public picha hii, ilitoka na habari hii hii uliyoileta na baadaye ikaja kuthibitika kuwa taarifa haikuwa na ukweli.
 
Asante kwa ufafanuzi mpya ndugu, binafsi nilisadiki taarifa uliosema ni ya awali sikujua kuhusu undani wa jambo hili. Lakini pia hata kama ni bus la aisort rais mstaafu kupanda na kusimama sio jambo la kamaida, vipi Kikwete anaweza pale JKN Airport kupanda basi la airport na akasimama ?

na je ni kweli kwamba bbda ya kustaafu uraisi huyu jamaa aliamua kurudi kua mwalimu wa chuo kazi yake ya awali ?
 
Mwanaume Aliyeitawala Iran kwa Miaka 8 akiingia kwenye Basi kwenda Kazini kama mwalimu, kazi yake kabla hajawa rais.

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, ambaye aliongoza taifa la Iran kwa miaka 8, sasa anafanya kazi kama mwalimu.

Picha ya Ahmadinejad akitumia usafiri wa umma ilionekana kwenye mtandao wa kijamii. Rejea ilitolewa chini ya picha kwamba katika kipindi cha miaka 8 ya uongozi wake Ahmadinejad hakupokea hata mshahara wa rial kutoka kwa bajeti ya serikali, akiishi kwa mshahara wa mwalimu. Wakati wa urais wake, hakuanzisha sheria ya urais wa zamani ili kupokea pensheni kubwa. Alirudi kufundisha tena, na kama unavyoona, anapanda basi kwenda kazini.

Hebu fikiria Rais wa zamani kujiunga na usafiri wa uma, yani kupanda dala dala tena akikosa seat anasimama na wala haoni shida. Na je vipi kwetu Africa tunaweza kupata kiongozi wa namna hii ?! Africa yetu hii kwa kina Mobutu waliojichimbiaga mahandaki yenye azina ya mabillion ya fedha.

(inasemekana Mobutu alikua na hazina na Trillion 8 ndani acha fedha alizojiwekea kwenye mabenki ya nje kama Finland, Malaysia, Canada nk)

View attachment 2625170
Nasikiaga eti baadhi ya nchi za waafrika wenzetu (majirani) mpaka ufikie kuupata urais ushajijengea maadui kibao, mikono yako imelowa damu ya wapinzani wako sasa unaanzaje kutembea peke yako bila ulinzi na mabunduki ?
 
Enzi za urais wake alitoa kauli kuifuta israel kwenye ramani ya dunia
 
Back
Top Bottom