Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Itashangaza kwa watu wenye poverty mentality iliyojengwa na wazungu ambao mnawasujudia.Mwanaume Aliyeitawala Iran kwa Miaka 8 akiingia kwenye Basi kwenda Kazini kama mwalimu, kazi yake kabla hajawa rais.
Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, ambaye aliongoza taifa la Iran kwa miaka 8, sasa anafanya kazi kama mwalimu.
Picha ya Ahmadinejad akitumia usafiri wa umma ilionekana kwenye mtandao wa kijamii. Rejea ilitolewa chini ya picha kwamba katika kipindi cha miaka 8 ya uongozi wake Ahmadinejad hakupokea hata mshahara wa rial kutoka kwa bajeti ya serikali, akiishi kwa mshahara wa mwalimu. Wakati wa urais wake, hakuanzisha sheria ya urais wa zamani ili kupokea pensheni kubwa. Alirudi kufundisha tena, na kama unavyoona, anapanda basi kwenda kazini.
Hebu fikiria Rais wa zamani kujiunga na usafiri wa uma, yani kupanda dala dala tena akikosa seat anasimama na wala haoni shida. Na je vipi kwetu Africa tunaweza kupata kiongozi wa namna hii ?! Africa yetu hii kwa kina Mobutu waliojichimbiaga mahandaki yenye azina ya mabillion ya fedha.
(inasemekana Mobutu alikua na hazina na Trillion 8 ndani acha fedha alizojiwekea kwenye mabenki ya nje kama Finland, Malaysia, Canada nk)
View attachment 2625170
Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye siasa na uongozi ktk mashariki ya kati na bara arabu.
Waliokwenda Qatar ni mashuhuda