Mahojiano na Shilole kwa kiingereza

Mahojiano na Shilole kwa kiingereza

Ngoja niishie njiani nadhani huko mbele sijui kukoje labda walioisikiliza yote wanaweza kujua, unajua inaweza ikawa anayeongea sio wewe lakini aibu utakayoipata ni ya wiki nzima.
 
Mbona hiyo ni kama utani...au ni masikio yangu tu?

Ingawa najua kinampiga chenga lakini hapo nadhani walikuwa wanafanya mzaha na utani kwa makusudi.

But what do I know...
Lakini yeye alikuwa serious
 
Mbona kajitshidi sana.Kikubwa umeelewa content.
 
Huyu dada anachonifurahisha alishadeclare kuwa hajui kiingereza ila haogopi kujaribu kuongea kisa watu watamcheka.
That is what we call CONFIDENCE. Big up Shilole
Mimi Mtanzania ambaye hajajinadi usomi wala kusema yeye mtaalamu wa lugha kukosea Kiingereza sishangai.

Ukianza kuongea Kiswahili, kujifunza Kiingereza ni kama vile uanze kujifunza lugha isiyo na mpangilio wala formula.

Hii ni kwa sababu Kiswahili kina mantiki zaidi ya Kiingereza.

Nina maana gani?

Kiswahili kipo "phonetic", maana yake ni lugha ambayo huhitaji kujifunza kutamka kila neno jipya unalokutana nalo.
Ukishajifunza misingi fulani ya kutamka maneno tu, unatumia misingi hiyo hiyo katika karibu maneno yote ya Kiswahili.

Kiingereza si phonetic, ni kama kila neno jipya inabidi ujifunze linatamkwa vipi upya.

Kiswahili kina mantiki sana katika kanuni za sarufi.

Ukijifunza kanuni fulani za sarufi katika Kiswahili, utaendelea kuzitumia hizo hizo karibu sehemu nyingine zote za Kiswahili.

Si Kiingereza.

Unaweza kuambiwa past tense ya rain ni rained, ya run ni ran, ya go ni went ya sink ni sunk.

Kiswahili karibu 100% kinafuata sheria moja. Kiingereza 50% kinafuata sheria, 50% nyingine ni exceptions.

Kama umezoea Kiswahili hapo lazima useme "huh"?

Ni kama unatoka lugha yenye mpangilio, unajifunza lugha isiyo na mpangilio.

Ndiyo maana Watanzania wengi Kiingereza kinawapa matatizo.

Si kwa sababu hawana akili, ni kwa sababu Kiingereza chenyewe ndiyo hakina akili.

Niachieni Shishi baby wangu.
 
I! I! I! I! I![emoji28] ya ya ya ya ya[emoji25] (in shishi's voice)
tusimlaumu shishi kwani wakati wazungu wanakuja na kiingereza tanzania walipokaribia na pwani yetu jahazi lilianza kuzama sasa ili kuokoa maisha yao ikabidi wachukue baadhi ya maneno ya kiingereza wakayatupa majini ili kupunguza uzito...kwa hiyo yalifika maneno machache mno huku kwetu [emoji3]🙄
 
Adam mchomvu mara nyingi hayuko serious ila hapo alikuwa anahojiwa serios

Alikuwa anahojiwa 'serious' kwenye kipindi gani? Hicho kipindi huwa wanafanya mahojiano kwa lugha ya Kiingereza hata kwa wasanii wa Kitanzania?
 
Alikuwa anahojiwa 'serious' kwenye kipindi gani? Hicho kipindi huwa wanafanya mahojiano kwa lugha ya Kiingereza hata kwa wasanii wa Kitanzania?
Kwani hizo sauti zinazosikika ni za kipindi gani nyani ngabu anyway kipindi chaitwa double xl wana utani na huenda waliamua kufanya hivyo makusudi coz wanamjua shilole sio mzuri kwenye hy lugha
Alikuwa anahojiwa 'serious' kwenye kipindi gani? Hicho kipindi huwa wanafanya mahojiano kwa lugha ya Kiingereza hata kwa wasanii wa Kitanzania?
 
Safiii... Ni Mara Miaa Ya Mswahil Anaeongea Kingereza Hivii... Kuliko Yule Ambae Ameenda Hadi Form 6 Afu Anajificha Ficha Na Ulimi Wake Mzito Kukitamka
 
alihojiwa kama sikosei clouds akasema anajua kiingereza Ila juzi hapa kwenye shiwaladu loohh!!
majanga matupu

Sent from my itel it1507 using JamiiForums mobile app
Hii lugha tunaipenda tu ila kwa wengi sio rafiki ila tutafanyaje ili uonekane umestaarabika na kuelimika lazima uiongee basi ndo hivyo tunajikongoja sentensi moja the kama kumi hivi hizo ni za kutafutia neno la mbele.
 
Hii lugha tunaipenda tu ila kwa wengi sio rafiki ila tutafanyaje ili uonekane umestaarabika na kuelimika lazima uiongee basi ndo hivyo tunajikongoja sentensi moja the kama kumi hivi hizo ni za kutafutia neno la mbele.
ila yeye anafanya makusudi tu,mana anajijua hajui so anaongea kufurahisha watu!
 
Back
Top Bottom