Huyu dada anachonifurahisha alishadeclare kuwa hajui kiingereza ila haogopi kujaribu kuongea kisa watu watamcheka.
That is what we call CONFIDENCE. Big up Shilole
Mimi Mtanzania ambaye hajajinadi usomi wala kusema yeye mtaalamu wa lugha kukosea Kiingereza sishangai.
Ukianza kuongea Kiswahili, kujifunza Kiingereza ni kama vile uanze kujifunza lugha isiyo na mpangilio wala formula.
Hii ni kwa sababu Kiswahili kina mantiki zaidi ya Kiingereza.
Nina maana gani?
Kiswahili kipo "phonetic", maana yake ni lugha ambayo huhitaji kujifunza kutamka kila neno jipya unalokutana nalo.
Ukishajifunza misingi fulani ya kutamka maneno tu, unatumia misingi hiyo hiyo katika karibu maneno yote ya Kiswahili.
Kiingereza si phonetic, ni kama kila neno jipya inabidi ujifunze linatamkwa vipi upya.
Kiswahili kina mantiki sana katika kanuni za sarufi.
Ukijifunza kanuni fulani za sarufi katika Kiswahili, utaendelea kuzitumia hizo hizo karibu sehemu nyingine zote za Kiswahili.
Si Kiingereza.
Unaweza kuambiwa past tense ya rain ni rained, ya run ni ran, ya go ni went ya sink ni sunk.
Kiswahili karibu 100% kinafuata sheria moja. Kiingereza 50% kinafuata sheria, 50% nyingine ni exceptions.
Kama umezoea Kiswahili hapo lazima useme "huh"?
Ni kama unatoka lugha yenye mpangilio, unajifunza lugha isiyo na mpangilio.
Ndiyo maana Watanzania wengi Kiingereza kinawapa matatizo.
Si kwa sababu hawana akili, ni kwa sababu Kiingereza chenyewe ndiyo hakina akili.
Niachieni Shishi baby wangu.