Mahojiano ya Diamond katika kipindi cha leo tena, amkubali mtoto wa Hamisa kuwa wake

Mahojiano ya Diamond katika kipindi cha leo tena, amkubali mtoto wa Hamisa kuwa wake

Ila Zari jamani anajionaga mzuri na Diamond hawezi tongoza mwanamke mwingine apa dunia...ila yamemkuta kiumbe mwenzangu mungu ampe uvumilivu nahisi leo atazidi kumkumbuka [HASHTAG]#IVAN[/HASHTAG] the DONE
 
Watu wanampongeza Diamond kwa sababu alikuwa anampa Hamisa 70k kwa siku ni kama alikuwa anamlipa hela ili akae kimya.

Kwenye interview kuna wakati anasema eti kuna siku alikuwa anaenda kumuona mtoto ila akaahirisha kwa sababu aliambiwa kategeshewa shilawadu wampige picha,baba wa namna gani unaogopa kuonana na mwanao kisa wambea!!?
 
We una akili sana!! Yaani huyu Hamisa angekuwa mjanja, angeendelea kuzitafuna za Chibu kwa miaka kadhaa ijayo! Na kwavile wanawake hupenda kutegeshea mimba penye pesa, am sure na mvuto ule alionao angetandikwa mimba ya pili very soon na hivyo kuendelea kula maisha bila stress kwa gia za watoto!!!

Na kama ulivyosema, there's no way mtoto wa Diamond na Hamisa anaweza kuwa siri kwa 3+ years, no way! Hata Diamond mwenyewe alifahamu kwamba it's just a matter of time lazima ingefahamika tu!!! Na huku mitaani wanaume ndivyo tunavyofanya! Unapiga mimba mchangani; unakubaliana na uliyempiga mimba kwamba "tufanye siri ili mama nanii asijue lakini na-take responsibility!"

Kwa mwanamke mjanja, anapiga kimya provided mwanaume anatimiza wajibu wake! Ukikutana na hawa akina dada zetu tuliokua nao huku Mbagala, hata kama mlikubaliana lazima atafute njia ya kufikisha ujumbe kwa wife!!

Kilichotokea kwa Hamisa ndo kile Waswahili wanasema "Mtaka yote kwa pupa, huko yote!"
Tatizo ni kushikiwa akili na mitandao ya kijamii badala ya kutumia akili... makosa yametokea tayari basi rekebisha kwa kutumia akili na kuhakikisha wewe na mwanao ni priority.
 
Hawa wanawake balaa, mtu anataka upendo na recognition ya aina gani? Mtoto asimamie show toka mimba mpaka labour kisha una option ya kutoa wazo la biashara uwe funded. Ombi ni moja tu mambo yawe low profile kisha unang'ang'ania kupeleka stories kwenye media?
Wewe uoni kwamba dai huyo mtoto angemfanya kama mtu ambae anamke alafu pembeni anamchepuko
 
Ila Zari jamani anajionaga mzuri na Diamond hawezi tongoza mwanamke mwingine apa dunia...ila yamemkuta kiumbe mwenzangu mungu ampe uvumilivu nahisi leo atazidi kumkumbuka [HASHTAG]#IVAN[/HASHTAG] the DONE

Kama umeumbwa kutokujiamini na kujikubali basi unatia huruma zari anajiamini na kujikubali ndo mana diamond kasema atatambaa had south anajua msimamo wa baby mama wake
 
Tusi judge sana kwa kusikiliza stori upande mmoja ngoja Hamisa aitwe tubalance story tuone Nani mjinga kati Yao usikute ahadi zilikuwa hewa hazikutimilizwa je
Au aliahidiwa makubwa zaidi je tuliza munkari
Yule demu story zilizopo aliaidiwa ndoa
 
Kapoteza kipi kwenye makubaliano yao? Mnawaza tu mali, tena angekuwa privately ndo angezidi kujazwa material things ili asiseme, ila utu ni bora kuliko kosa. Afu washakuwa wazazi, mwisho wa siku watakaa chini watapatana just for the sake of their child na maisha yataendelea (sijasema kurudiana), huyu jini mkata kamba ataondoka tu kati yao. Afu ni vyema wamlee mtoto wao kwa uhuru
Kwahiyo ww unaamini hamisa alibeba mimba ya diamond kwakuwa anampenda sana?!...je kwa majizo napo ilikuwa ni kwa mapenzi?!
 
Huyo mtoto asiye na hatia mama ake tu akili hana unadhani wapambe wa insta na jf tutaweza kumfanya awe na akili?
Mwanamke mwenye akili hata akitereza akazaa na mtu mwenye mahusiano yake atafanya namna mwanae asikose mahitaji ya msingi, atatumia akili nyingi kuzuia uadui kati ya baba na mtoto na mtoto na nduguze akikua huko mbele then ataangalia maisha yake anatokaje bila kufungwa na kurudishwa nyuma na makosa aliyofanya.
Mwisho wa siku kama huna namna utaharibu mahusiano yale mengine sababu mwanaume kashasema msijuane na huleti chokochoko ni rahisi mtoto wako kukubalika bila kinyongo na familia ya upande wa pili. Kukiwa na chokochoko nyingi hata mtoto atachukiwa.
For as long as ulianza kama main chick kuwa na mtoto sio guarantee wewe kuwa main.... watu wapambane na hali na kuacha kuparamia wanaume wakware
Maneno yako mazuri unajua wengine hayajawafika haya ndo maana wanachukulia kirahisirahisi ...inahitaji sana hekima kwa ku-handle haya mambo maana siku zote malezi ya mtoto yanatakiwa yaende sambamba mahusiano mema ya wazazi hata kama wameachana ama mmoja yupo kwenye mahusiano yake
 
Kwahiyo ww unaamini hamisa alibeba mimba ya diamond kwakuwa anampenda sana?!...je kwa majizo napo ilikuwa ni kwa mapenzi?!
Anajua mwenyewe moyoni mwake coz kila aliyezaa ndo anajua kwa nini ameamua kuzaa.
 
Anajua mwenyewe moyoni mwake coz kila aliyezaa ndo anajua kwa nini ameamua kuzaa.
Basi tuache kusema kama hakufuata umaarufu na hela za diamond kama kweli tunaamini ukweli anao mwnyw moyoni
 
haya maisha ya mastaa ovyo tu,hivi mfano mimi nina mtoto wa mchepuko mama anajua ndg zangu wote wanajua ,mke wangu nishamwambia,sasa jamii inataka nini sasa ,haya mambo mengine ni vihelele vya watanzania kukosa kazi kuanza kujadili maisha ya watu,haya naona saivi kila mtu aliyempa mimba mchepuko ili mtoto akubalike muwe mnatoa matangazo kwenye gazeti au TV,kweli inchiii ya viwanda ni ndoto
Familia nzima wenyewe wanajuana eti hadi ampost kwenye page yake ndo anakua baba kamili
 
Yule demu story zilizopo aliaidiwa ndoa
Atakuwa mpumbavu kama aliamini! Na hata kama kweli, ndo hapo alipotakiwa kupeleka mambo kimya kimya! There's no way mwanaume mwenye familia anaweza kutangaza hadharani kirahisi rahisi tu kwamba kapiga mimba kwenye mechi za mchangani!!

Nadhani alipobugi Hamisa ni ile kuona Zari sio mke wa ndoa kumbe ndoa sio makaratasi wala kiapo mbele ya sheikh au padri bali ni commitment! Hata kama ndo imefungwa kanisani au msikitini jana; kama haina commitment, hiyo sio ndoa compared na maisha ya uhawara yenye commitment ndani yake!
 
Maneno yako mazuri unajua wengine hayajawafika haya ndo maana wanachukulia kirahisirahisi ...inahitaji sana hekima kwa ku-handle haya mambo maana siku zote malezi ya mtoto yanatakiwa yaende sambamba mahusiano mema ya wazazi hata kama wameachana ama mmoja yupo kwenye mahusiano yake
Ubinafsi na kukomoana ni ugonjwa mbaya sana.... Mama inabidi uwe makini sana katika maamuzi sababu mtoto wewe ndio unashinda nae na kadiri anavyozidi kukua unazidi kumuelewesha situation kulingana na umri wake.
Uadui ukiwepo ni bora ukaishia kuwa uadui wa kawaida lakini sometimes mara kurogana, mara kuwekeana vikwazo katika maisha ya kila siku, kuuana, kujeruhi.... etc. Why kufika huko while kila mtu akikubali makosa yake na kufikia muafaka kusimamia njia sahihi maisha yanaendelea?
 
Back
Top Bottom