Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Sawa mkuu tupo pamoja
Paulo jacob kagame=Nelson jacob kagame!!?

We jamaa!!

Kuna move ya kuruhusu free movement kuingia Rwanda bila visa je mjomba amechoka anataka kuruhusu demokrasia ndani ya Rwanda au kwa move hii kaandaa ambush nyingine ambayo itakua na mwelekeo mpya wa Rwanda ijayo!?au ni mtego kwa maadui wake waone sasa Rwanda ni shwari Ili waje washughulikiwe!!?

Au ameshankula mkataba wa dp world hivyo ana uhakika wa ulaji wa ukoo wake hata akiwa nje ya madaraka!!?

Hebu nijibu we jamaa!!
 
INAENDELEA...........!!!!
Afande ""F""""anasema kua alikua anafikiria kujitoa jeshini either kwa kukimbilia nchi ya Zaire au Tanzania maana alikua anaona kabisa hali ilipokua inaelekea kutakua na uvunjikaji wa amani nchini mwake,ila kilichokua kinamzuia ni kiapo chake mbele ya kamandi kuu ya jeshi.
JANUARY 22 1988.....!!!!! KIGALI (CHIGALI) RWANDA.
Ilikua ni siku ya kawaida kama siku zingine na alikua anashuka anashuka kwenye gari lake la kijeshi ili kuingia ndani kwake kupumzika,ila aliyeanza kushuka ni mlinzi wake binafsi ambae aliambulia risasi za kichwani na kufa pale pale huku gari lake likishambuliwa na risasi za kutosha kabla ya wahusika kukimbia kwa gari nyingine.
Unajua afande""F"" alikua na utaratibu wa kutembea na walinzi tofauti na makanali wengine,na hili tukio kusema kweli lilimvunja moyo saana.Maana hata uchunguzi uliofanywa na jeshi kuhusu hili jaribio la kumuua ulikuawa juu juu tu usiokua na majibu ya kuridhisha.
Lakini alipofanya uchunguzi binafsi aligundua kua ule mpango ulisukwa na makanali wenzie ambao walikua na mipango yao kichwani na walimwona afande""F""kama tishio kwao,kwa msimamo wake wa kukataa kuchanganya jeshi na siasa sababu alijua litapoteza weledi wake wa kufanya kazi kwa ufanisi kama taaluma ya kijeshi inavyotaka.
TURUDI KWENYE MPAKA WA MJI WA GATUNA KATI YA RWANDA NA UGANDA 1988:
Toka yale mashambulio ya mwaka uliopita yaani 1987 hali ya pale mpakani ilikua tete na shughuli nyingi za kiraia kwa upande wa pande mbili zote zilisitishwa na kulikua na harakati tu za kijeshi za waziwazi hasa ule upande wa uganda.
Na ilikua wazi kabisa kua kuna vikundi vya waasi vinavyosaidiwa na serikali ya Uganda ili kuleta hali ya sintofahamu upande wa Rwanda.
Magari ya kivita na maroli ya kijeshi yaliyokua yanawasusha na kuwapakia watu wakiovalia sare za jeshi la Uganda ila walionekana kabisa waziwazi ni wanyarwanda wenye asili ya kitusi.
Hivyo kutokana na hali hiyo ya wasiwasi na taa nyekundu ya kivita na lile shambulio la kwanza lililoshindwa lilisababisha eneo lote la mpaka wa Rwanda na Uganda liwe chini ya kamandi kuu ya kijeshi ya jeshi la Rwanda chini ya Amri jeshi mkuu wa wakati huo Kanali Habiyarimana Juvenal.
Kambi mpya za kijeshi ziliongezwa na vikosi maalumu vya kamandi kuu kutoka kambi ya mafichoni isiyojulikana ya Ginene vikiongezwa mipakani kote upande ule wa Uganda.
Magari ya deraya yakiongezwa na vifaru vya kijeshi na mzinga na magari ya kubebea mzinga vilionekana wazi wazi pande zote mbili za mpaka,na ilikua inasubiriwa ni lini vita hivi vitajitokeza na hata uhusiano wa kidiplomasia wa pande hizi mbili ulikua unasua sua kutokana na mashambulio ya mwaka 1987 japo serikali ya Uganda ilikua inakana kuhusika na lolote lile.
Hali ilikua tete mpakani maana kulikua na matukio madogo madogo ya kurushiana risasi na kutukanana na kurushiana maguruneti ya kutupwa na mkono kwa pande mbili zote za wanajeshi wa mpakani na raia walikimbia kabisa maeneo yote ya mpakani mwa Uganda na Rwanda kuhofia usalama wao.
Afande ""F"" yeye akurudishwa tena mpakani bali alipewa jukumu lipya la kusimamia ulinzi binafsi wa ardhini wa raisi Juvenail na familia yake.
Na alikua na jukumu pia la kuhakikisha usalama wa viongozi waandamizi wa serikali na familia zao.
Kanali""F""au afande ""f"" sasa akawa na jukumu lipya la kuhakiki usalama wa raisi ndani ya nchi,pamoja na usalama wa viongozi waandamizi ndani ya serikali ya Kanali Juvenail Habiyarimana na alibakia na cheo hicho kama mlinzi binafsi wa raisi akiwa ardhini kuanzia mwaka 1988 mpaka mwaka 1994 alipokimbilia Bukavu nchini Zaire.
ITAENDELEA.............!!!!!!
 
Mkuu umeuliza maswali matano kwa wakati mmmoja 🤣🤣🤣 afu yamekaaa kijasusi kweli kweli z🤣🤣
 
Nasubiria kwa hamu!!
 
INAENDELEA............!!!
Afande ""F"" anasema uhasama dhidi ya makundi hayo mawili ya kinyarwanda yalianzia toka mwaka 1948 wakati wa ukoloni wa wabeligiji na ulichangiwa na matabaka ya kwenye jamii ya kinyarwanda.
Ulikua unaridhishwa kutoka kizazi mpaka kizazi na ulikita mizizi pale wanyarwanda waliokua uhamishoni walipoamua kuanza harakati za kurudi ngumbani.Ikumbukwe mwanzo tatizo halikua ukabila bali nafasi za utawala na madaraka kati ya jamii za wafanya biashara na wanasiasa ambao waligeuza ukabila kwa manufaa yao.
Ilikua lazima kundi moja litoke au lipotezwe ili kundi lingine litawale na kuhodhi madaraka ya nchi.
Uhasama huu ulianzia kwenye koo mpaka ukapanda ngazi ya kitaifa na ukaja kusababisha mauaji ya kimbali ya mwaka 1958 na 1972 na 1994 na mara zote hizo jamii ya kitusi wakiwa wahanga kwa asilimia kubwa kwa sababu hawakua kwenye utawala.
Na kupinduliwa kwa serikali ya wahutu walio wengi na mauaji ya kimbari ya watusi walio wengi ndio yaliendelea kuchochea uhasama huu.
TURUDI KWA AFANDE""F"" 1993 CHIGALI (KIGALI) RWANDA
Anasema na yeye pia alikua amekulia mazingira hayo hayo ya chuki toka akiwa mdogo ila tokea alipojiunga na jeshi alianza kutazama vitu kwa mtindo tofauti na hakukubaliana na baadhi ya mambo jeshini,kama lile la kuchanganya taaluma ya kijeshi na siasa za ukabila.
Toka mwanzo alikataa kushiriki mauaji ya kikabila na kupanga njama za mauaji ya kimbari ambayo yalikua yanaasisiwa na pande zote mbili za kwenye mgogoro wa kuwania madaraka ya nchi ya Rwanda.
Na uhasama huu uliongezeka baada ya waliokua madarakani kukimbizwa uhamishoni nchini Zaire.
Baada ya usalama kua unasuasua ns kila dalili zinaonyesha serikali kushindwa kwa matukio ambayo ni mengi ukijumuisha na lile la raisi kuuawa akiwa angani,basi kanali""F"" aliamua kuchukua jukumu la kuondoka kigali,,baada kutolewa uongozi wa vikosi vyote vya kijeshi kwa lawama za kushindwa kumlinda raisi na akapewa lawama zote za kifo cha raisi na akakataliwa kua mstari wa mbele wa mapigano,kitu ambacho anadai kiliokoa maisha yake na hakufia kwenye uwanja wa mapambano kama wenzake.
Afande""F""alishuhudia mauaji ya raia na anakiri wazi kua haya mauaji yalikua mauaji ya kupangwa na hayakua mauaji ya bahati mbaya,bali makusudi na ya kulipiza kisasi kati ya pande hizi mbili zenye uhasama.
Hata raisi anasema kua alimwambia
"""""""Namnukuu"""""""""""""
Raisi amesikitika sana na mpango wa kuwauwa watu wenye jamii ya kitusi na hana uwezo wa kuuzuia sababu anahofia wanajeshi wake watampindua au kumuua yeye.
"""""""""Mwisho wa kunukuu"""""""""""""""""
SASA TURUDI KWENYE SAFARI YANGU MJINI BUKAVU KUWAHOJI WATU NILIOWATAJA HAPO JUU KUHUSU UHASAMA WAO WA JADI.
Lakini kabla ya hapo nitamzungumzia PAULO JACOB KAGAME na influence yake kubwa toka miaka ya themanini mpaka alipokorofishana na serikali ya Rwanda mnamo mwaka 1990.
ITAENDELEA KIDOGO KIDOGO ILI ISIPOTEZE MAANA NA IKUMBUKWE HII SIO HADITHI BALI NI INTERVIEW...................!!!!!!
 
Jibu maswali mkuu!!

Nataka kujua usalama wa wanyambo waishio huko Rwanda!!
Wanyambo nadhani wapo salama kabisa huko rwanda sababu kihistoria eneo la rwanda karibia asilimia 20% na asilimia 20% ya eneo la Uganda ilikua miliki ya wanyambo kabla ya wakoloni kuja na kuweka mipaka.
 
Mkuu umeuliza maswali matano kwa wakati mmmoja 🤣🤣🤣 afu yamekaaa kijasusi kweli kweli z🤣🤣
Kweli ila ni vema kudadavua kidogo. Binafsi naona mantiki ktk jitihada za Kagame ktk kujaribu kuneutralize social composition ya wanyarwanda. Wakati sasa wengi wanaona Watutsi wako wengi na salama ndani ya Rwanda, iwapo wageni na wahutu wanao ogopa wakirudi Rwanda itakua rahisi Kubadilisha mitazamo yao hasi juu ya umoja wa nchi.
Mtakumbuka kuwa Mwaka jana kama sikosei, Kagame aliomba wahamiaji haramu kutoka nchi ya Ueingereza kuja na kufanya Makao Rwanda, ukiangalia kwa nje huelewi nia halisi... Ila nia kuu hapo ni kuneutralize kabila... Awepo watu mchanganyiko na hapo itakua rahisi kuondoa dominance ya makabila mawili ambayo ni Pinzani na Yana kisasi juu kati yao.

Binafsi naona kwa namna wanyarwanda walio nje ya nchi wanavyozidi kuwa huko wanajitengeneza kama Hamas... Wanajifunza na kujipanga ili waje kukilipua kwa madai ya kudai Uhuru na nchi yao.... Kama jirani si pendi hata kidogo kuona genocide ya 94.Natamani wote wabadilishe mitazamo juu ya ubaguzi na wajione wa moja. Mungu awasaidie Wanyarwanda🙏
 
Tatizo la wanyarwanda ni ubaguzi wa kila jamii kujiona bora kuliko nyenzake.
Nakumbuka hata Habiyarimana alikua anakataa kwa Banyarwanda waliopo nje ya nchi hiyo kurudi nyumbani.
Rejea hotuba yake ya bunge mwaka 1987 baada ya lile shambulizi la kule Gatuna.
NB: NA HAO WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA UINGEREZA WENGI WALIKUA WAHABESHI NA WASOMALI KWA ASILIMIA 90%
NADHANI HAPO UMESHAELEWA KWANINI WALIPELEKWA RWANDA NA SERIKALI YA KAGAME IKAWAPOKEA.
 
Ni kama Rwanda ijayo inaandaliwa Marais wasio na nasaba ya makabila hayo mawili!yaani makabila madogo ya kigeni ndio yatawale kuua uhasama kati yao!!

Ni kama huku kwetu pale tunapopenyeza warundi hadi ikulu Ili kuondoa dhana ya upendeleo wa kikabila kwenye keki ya taifa!!

Nadhani mjomba kaona mbali sana!

Kama an akili angenitimka hata mtanzania akawe kiongozi pale kama mhamiaji kutoka tz Ii kuua ukabila pale Rwanda!!
 
Ni kama Rwanda ijayo inaandaliwa Marais wasio na nasaba ya makabila hayo mawili!yaani makabila madogo ya kigeni ndio yatawale kuua uhasama kati yao!!

Ni kama huku kwetu pale tunapopenyeza warundi hadi ikulu Ili kuondoa dhana ya upendeleo wa kikabila kwenye keki ya taifa!!

Nadhani mjomba kaona mbali sana!

Kama an akili angenitimka hata mimi nikawe kiongozi pale kama mhamiaji kutoka tz Ii kuua ukabila pale Rwanda!!
Ubaguzi wa kinyarwanda ni kwenye koo,,sababu hakuna kabila pale.
Wote ni wanyarwanda na wanaongea kinyarwanda.
NB: NI KAMA UHASAMA WA WASOMALI
 
INAENDELEA,,,,,,,,,,,!!!!
Afande ""f"" anasema namnuku:
Askari wa RPF walikua wanazidi kusonga mbele na hali ilikua tete upande wa majeshi ya serikali sababu walikua hawana wanajeshi wa akiba na hata waliokua wanajeshi wa akiba,,,namaanisha vijana wa intarehamwe walikua hawana nidhamu na taaluma ya kijeshi.
Anasema na mauaji ya kimbari na ubakaji wa raia ulikua unafanywa na pande zote mbili wakati wa vita na kuongeza uhasama kati yao.
Majeshi ya serikali ya wahutu walio wengi jeshini waliendekeza uhasama kwa kuua raia na kupandikiza chuki kwa raia wawaue watusi.
Na kwa upande wa watusi walio wengi RPF walikua pia wanaendekeza chuki baina ya Watusi na Wahutu,,,,na pia walikua wanaua Wahutu na kusababisha uhasama.
Afande""f""" anasema uhasama huu ulichochewa na mauaji ya pande zote mbili mwaka 1993 na 1994 ila mauaji ya wahutu yaliyofanywa na RPF waga hayazungumzwi na jambo hilo limeendelea kuweka uhasama baina ya jamii hizi mbili.
Anasema wakati vikosi vya serikali vinarudi nyuma mpaka mji wa Gitarama,yeye ndipo alipewa tena jukumu la kuvizuia vikosi vya RPF kwa mda ili aweze kusaidia majeruhi waliotolewa Kigali baada ya kuzidiwa na vikosi vya RPF na kurudishwa kutokea mjini Kigali.
Na pia alipewa jukumu la kuandaa mashambulizi ya kuvizia kutokea njia ya Runda ili kuzuia kwa haraka vikosi vya RPF visiuzingire mji wa Gitarama.
Anasema afande""f"" alikua na idadi ya wanajeshi 4000 na alikataa usaidizi wa vikosi vya intarehamwe zaidi ya 6000 ambao kazi yao kubwa ilikua kubaka na kuua Watusi tu na Wakongomani.
Anasema afande""f""jeshi la serikali lilikua limepoteza wanajeshi wengi na lilikua na majeruhi wengi na kulikua na malalamiko toka kwa wanajeshi wa ngazi za chini kua,,walikua wanalazimishwa kuua na kubaka na kupora na makamanda wao walikua wamekataa kwenda msitari wa mbele,,wote walikua wanakimbilia miji ya mpakani na Zaire na Tanzania.
Alichokifanya afande""f"" anasema alichokifanya ni kuwasiliana kwa simu ya upepo na rafiki yake PAULO na kumwambia haya yafuatayo
"""""""""""""""""Namnukuuu""""""""""""
Nilichukua simu ya upepo na kumpigia ndugu yangu PAULO ambae toka mwaka 1990 tumekua maadui wa kisiasa ila sio kiundugu.
AFANDE: Paulo naona mmetunyanganya Kigali na mumemuua ""KINANI""
PAULO: Sio mimi niliyetoa amri ya kumuua ""KINANI"" ila ni vijana wangu walikua wanajihami sababu walijua ni ndege ya mzigo ya kivita ya ufaransa ilikua inashusha silaha na Kigali hatujawanyanganya bali wamekimbia wenyewe.
AFANDE:Nikuombe kitu Paulo?
PAULO :Yeah go ahead ila mimi nipo Byumba mda huu kanali.
Na siwezi kukusaidia lolote sababu upo upande wa adui,hivyo watu wangu hawatonielewa.
AFANDE: Ni kitu cha mwisho kati yangu mimi na wewe.Maana vikosi vyote vinarudi nyuma na wafaransa hawatusaidii tena kwa lolote na wewe mwenyewe unajua sijawahi kukutana na wewe kwenye uwanja wa vita tokea mwaka 1987 so kiasilia mimi sio adui yako.
PAULO: Ooh oky proceed ( Go ahead)
AFANDE: Naomba uwazuie vijana wako wasivuke Rundwa na Butamwa ili niondoe majeruhi wote mpaka Gitarama.Nimepewa amri ya kukushambulia ila sitofanya hivyo bali tufanye cease fire ya siku tano.
Hii vita sisi tunaelekea kushindwa na hii nchi tayari imeshakua tayari yenu.
PAULO: Wewe una nafasi gani sasa jeshini maana najua kila kitu kuhusu wewe na cha kukushauri ni kwamba uende Bukavu ukae huko maana ndani ya mwezi nchi nzima itakua chini yetu na napenda ujue kua sikukusaliti bali kila mtu anapenda madaraka hivyo sikua na jinsi.
Wewe mwenyewe unajua ilibidi wengine wafe ili sisi tuwepo hapa tulipo leo.Hata wewe ulitusaliti kwa kukataa kutupatia taarifa nyeti za mtu uliyekua unamlinda"""KINANI"""
AFANDE: Nitapata cease fire au???
PAULO: Ya siku tatu sababu sisi ni maadui na wewe unajua hilo.
AFANDE: Sawa Paulo nashukuru ila kumbuka tukikutana uwanja wa vita sitokuonea huruma.
PAULO:Risasi haina macho sitokulaumu tupo vitani.
AFANDE: Najisikia vibaya kuikimbia nchi niliyozaliwa niwe mkweli tu.
PAULO: Hata mimi nilijisikia vibaya kuikimbia nchi niliyozaliwa nikiwa mtoto.
AFANDE: Asante kwa cease fire.
PAULO: Ninalipa fadhila kwa access ulizonipa mwaka 1985 mjini Kampala.
AFANDE:Sitosahau fadhila japokua watu wetu hawaelewani na wanauana kama kuku.
PAULO: Siasa ni mchezo mchafu wa kumlaumu ni ""KINANI""
Basi mazungumzo yao yakaishia hapo na afande""f"" aliyafanya haya mazungumzo kwa siri kubwa ili wakuu wake wa kijeshi wasijue kama amewasiliana au anawasiliana na adui wa serikali inayoelekea kupinduliwa madarakani.
Afande"""F"""anaendelea kusimulia kua mazungumzo yake na PAULO yalimsaidia kuweza kuokoa maisha ya askari zaidi ya 900 ambao walikua wamejeruhiwa mjini Rundwa na mjini Mugesera na hiyo ilikua mara ya mwisho ya wao kuongea mpaka mwaka 1998 mjini Kisangani Congo DRC,walipokutana wakati yeye afande ""f"" akiwa na vikosi vya Proffesa wamba dia wamba na washirika wao wa Uganda katika kutafuta cease fire ya kuondoa mapigano ndani ya mji wa Kisangani nchini DRC au Zaire ya zamani.
Anasema kua alifanikuwa kuweka cease fire kati ya vikosi vyake na vikosi vya RPF na ilimsaidia kuwashawishi wakuu wake wa kijeshi waondoke pia katika mji wa Gitarama na wasogee mji wa mpakani wa Bugarama na waweke makao yao makuu ya kijeshi,kwa maana Gitarama sio sehemu sahii kabisa.
Na anasema aliwaambia waziwazi makamanda wake kua yale mauaji ya kuua watu kiholela kwa kutumua intarehamwe yanapandikiza chuki kati yao na watu wa RPF na hizi chuki zinaweza kudumu kizazi mpaka kizazi.
Vile vile anasema vikosi vya RPF vilikua pia vinatekeleza mauaji maeneo yote vilivyoyateka kwa kudai wakazi wote wa maeneo hayo ni washirika wa intarehamwe na wameua watusi,hivyo nao wanasitahili kuuawa.
BUGARAMA JANUARY 06 1994
Afande""f""anasema kua baada ya kuweza kuongea na PAULO na kuweza kupata cease fire ya kimya kimya ndani ya siku tano na alifanikiwa kupata haueni ya kuokoa majeruhi na kurudisha nyuma vikosi vilivyokua tayari vimepoteza muelekeo na ilikua haina maana kuendelea kuungangania mji wa Gitarama na mji wa Rundwa na mji wa Butamwa na mji wa Mugesera.
Kama wangeendelea kungangania mji wa Rundwa na mji wa Butamwa na mji wa Mugesera basi wangeshindwa kwenye uwanja wa mapambano na wasingeweza kupambana na vikosi vya RPF kwa wakati huo,,suluhisho pekee lilikua ni kurudi nyuma mpaka mji wa Bugarama
Na alifanikiwa katika hilo la kuwashauri wanajeshi wenzake warudi mpaka mji wa Bugarama na kujipanga upya na hapa ndipo mawazo ya chuki na uhasama yalipoanza kumea zaidi kwa wanajeshi wa serikali ya kihutu na waasi wa RPF.
Na kila upande ukiwa unajiona upo sahii kwa hoja zake zenye mashiko ya ubaguzi wa kisiasa na kikabila.
ITAENDELEA..........!!!!
 
Back
Top Bottom