INAENDELEA,,,,,,,,,,,!!!!
Afande ""f"" anasema namnuku:
Askari wa RPF walikua wanazidi kusonga mbele na hali ilikua tete upande wa majeshi ya serikali sababu walikua hawana wanajeshi wa akiba na hata waliokua wanajeshi wa akiba,,,namaanisha vijana wa intarehamwe walikua hawana nidhamu na taaluma ya kijeshi.
Anasema na mauaji ya kimbari na ubakaji wa raia ulikua unafanywa na pande zote mbili wakati wa vita na kuongeza uhasama kati yao.
Majeshi ya serikali ya wahutu walio wengi jeshini waliendekeza uhasama kwa kuua raia na kupandikiza chuki kwa raia wawaue watusi.
Na kwa upande wa watusi walio wengi RPF walikua pia wanaendekeza chuki baina ya Watusi na Wahutu,,,,na pia walikua wanaua Wahutu na kusababisha uhasama.
Afande""f""" anasema uhasama huu ulichochewa na mauaji ya pande zote mbili mwaka 1993 na 1994 ila mauaji ya wahutu yaliyofanywa na RPF waga hayazungumzwi na jambo hilo limeendelea kuweka uhasama baina ya jamii hizi mbili.
Anasema wakati vikosi vya serikali vinarudi nyuma mpaka mji wa Gitarama,yeye ndipo alipewa tena jukumu la kuvizuia vikosi vya RPF kwa mda ili aweze kusaidia majeruhi waliotolewa Kigali baada ya kuzidiwa na vikosi vya RPF na kurudishwa kutokea mjini Kigali.
Na pia alipewa jukumu la kuandaa mashambulizi ya kuvizia kutokea njia ya Runda ili kuzuia kwa haraka vikosi vya RPF visiuzingire mji wa Gitarama.
Anasema afande""f"" alikua na idadi ya wanajeshi 4000 na alikataa usaidizi wa vikosi vya intarehamwe zaidi ya 6000 ambao kazi yao kubwa ilikua kubaka na kuua Watusi tu na Wakongomani.
Anasema afande""f""jeshi la serikali lilikua limepoteza wanajeshi wengi na lilikua na majeruhi wengi na kulikua na malalamiko toka kwa wanajeshi wa ngazi za chini kua,,walikua wanalazimishwa kuua na kubaka na kupora na makamanda wao walikua wamekataa kwenda msitari wa mbele,,wote walikua wanakimbilia miji ya mpakani na Zaire na Tanzania.
Alichokifanya afande""f"" anasema alichokifanya ni kuwasiliana kwa simu ya upepo na rafiki yake PAULO na kumwambia haya yafuatayo
"""""""""""""""""Namnukuuu""""""""""""
Nilichukua simu ya upepo na kumpigia ndugu yangu PAULO ambae toka mwaka 1990 tumekua maadui wa kisiasa ila sio kiundugu.
AFANDE: Paulo naona mmetunyanganya Kigali na mumemuua ""KINANI""
PAULO: Sio mimi niliyetoa amri ya kumuua ""KINANI"" ila ni vijana wangu walikua wanajihami sababu walijua ni ndege ya mzigo ya kivita ya ufaransa ilikua inashusha silaha na Kigali hatujawanyanganya bali wamekimbia wenyewe.
AFANDE:Nikuombe kitu Paulo?
PAULO :Yeah go ahead ila mimi nipo Byumba mda huu kanali.
Na siwezi kukusaidia lolote sababu upo upande wa adui,hivyo watu wangu hawatonielewa.
AFANDE: Ni kitu cha mwisho kati yangu mimi na wewe.Maana vikosi vyote vinarudi nyuma na wafaransa hawatusaidii tena kwa lolote na wewe mwenyewe unajua sijawahi kukutana na wewe kwenye uwanja wa vita tokea mwaka 1987 so kiasilia mimi sio adui yako.
PAULO: Ooh oky proceed ( Go ahead)
AFANDE: Naomba uwazuie vijana wako wasivuke Rundwa na Butamwa ili niondoe majeruhi wote mpaka Gitarama.Nimepewa amri ya kukushambulia ila sitofanya hivyo bali tufanye cease fire ya siku tano.
Hii vita sisi tunaelekea kushindwa na hii nchi tayari imeshakua tayari yenu.
PAULO: Wewe una nafasi gani sasa jeshini maana najua kila kitu kuhusu wewe na cha kukushauri ni kwamba uende Bukavu ukae huko maana ndani ya mwezi nchi nzima itakua chini yetu na napenda ujue kua sikukusaliti bali kila mtu anapenda madaraka hivyo sikua na jinsi.
Wewe mwenyewe unajua ilibidi wengine wafe ili sisi tuwepo hapa tulipo leo.Hata wewe ulitusaliti kwa kukataa kutupatia taarifa nyeti za mtu uliyekua unamlinda"""KINANI"""
AFANDE: Nitapata cease fire au???
PAULO: Ya siku tatu sababu sisi ni maadui na wewe unajua hilo.
AFANDE: Sawa Paulo nashukuru ila kumbuka tukikutana uwanja wa vita sitokuonea huruma.
PAULO:Risasi haina macho sitokulaumu tupo vitani.
AFANDE: Najisikia vibaya kuikimbia nchi niliyozaliwa niwe mkweli tu.
PAULO: Hata mimi nilijisikia vibaya kuikimbia nchi niliyozaliwa nikiwa mtoto.
AFANDE: Asante kwa cease fire.
PAULO: Ninalipa fadhila kwa access ulizonipa mwaka 1985 mjini Kampala.
AFANDE:Sitosahau fadhila japokua watu wetu hawaelewani na wanauana kama kuku.
PAULO: Siasa ni mchezo mchafu wa kumlaumu ni ""KINANI""
Basi mazungumzo yao yakaishia hapo na afande""f"" aliyafanya haya mazungumzo kwa siri kubwa ili wakuu wake wa kijeshi wasijue kama amewasiliana au anawasiliana na adui wa serikali inayoelekea kupinduliwa madarakani.
Afande"""F"""anaendelea kusimulia kua mazungumzo yake na PAULO yalimsaidia kuweza kuokoa maisha ya askari zaidi ya 900 ambao walikua wamejeruhiwa mjini Rundwa na mjini Mugesera na hiyo ilikua mara ya mwisho ya wao kuongea mpaka mwaka 1998 mjini Kisangani Congo DRC,walipokutana wakati yeye afande ""f"" akiwa na vikosi vya Proffesa wamba dia wamba na washirika wao wa Uganda katika kutafuta cease fire ya kuondoa mapigano ndani ya mji wa Kisangani nchini DRC au Zaire ya zamani.
Anasema kua alifanikuwa kuweka cease fire kati ya vikosi vyake na vikosi vya RPF na ilimsaidia kuwashawishi wakuu wake wa kijeshi waondoke pia katika mji wa Gitarama na wasogee mji wa mpakani wa Bugarama na waweke makao yao makuu ya kijeshi,kwa maana Gitarama sio sehemu sahii kabisa.
Na anasema aliwaambia waziwazi makamanda wake kua yale mauaji ya kuua watu kiholela kwa kutumua intarehamwe yanapandikiza chuki kati yao na watu wa RPF na hizi chuki zinaweza kudumu kizazi mpaka kizazi.
Vile vile anasema vikosi vya RPF vilikua pia vinatekeleza mauaji maeneo yote vilivyoyateka kwa kudai wakazi wote wa maeneo hayo ni washirika wa intarehamwe na wameua watusi,hivyo nao wanasitahili kuuawa.
BUGARAMA JANUARY 06 1994
Afande""f""anasema kua baada ya kuweza kuongea na PAULO na kuweza kupata cease fire ya kimya kimya ndani ya siku tano na alifanikiwa kupata haueni ya kuokoa majeruhi na kurudisha nyuma vikosi vilivyokua tayari vimepoteza muelekeo na ilikua haina maana kuendelea kuungangania mji wa Gitarama na mji wa Rundwa na mji wa Butamwa na mji wa Mugesera.
Kama wangeendelea kungangania mji wa Rundwa na mji wa Butamwa na mji wa Mugesera basi wangeshindwa kwenye uwanja wa mapambano na wasingeweza kupambana na vikosi vya RPF kwa wakati huo,,suluhisho pekee lilikua ni kurudi nyuma mpaka mji wa Bugarama
Na alifanikiwa katika hilo la kuwashauri wanajeshi wenzake warudi mpaka mji wa Bugarama na kujipanga upya na hapa ndipo mawazo ya chuki na uhasama yalipoanza kumea zaidi kwa wanajeshi wa serikali ya kihutu na waasi wa RPF.
Na kila upande ukiwa unajiona upo sahii kwa hoja zake zenye mashiko ya ubaguzi wa kisiasa na kikabila.
ITAENDELEA..........!!!!