Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

KAMEMBE NEAR LAKE KIVU.......!!!
NAENDELEA.........!!!
Afande"f" anasema kua aliona hakuna maisha tena Rwanda kwa wakati ule,maana uwepo wa wanajeshi wa umoja wa mataifa na wanajeshi wa ufaransa na wa uganda na ushindi wa vikosi vya RPF ulimfanya plan A aliyokua nayo aachane nayo na afuate plan B.
Toka mjini Kamembe plan ikawa ni kuvusha magari yote ya kijeshi na vifaru na yale marolo ya logstic kwa kupitia njia isiyo rasmi ya Cyangugu,ila wale wanajeshi kikosi kizima wakavuka upande ule wa ziwa mpaka upande wa pili wa nchi ya Zaire.
Shughuli hii nzito ilimchukua wiki nzima kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na wakati huo huo alikua anazuia askari wa RPF wasiweze kumsogelea mjini Kamembe na alituma vikosi vya asikari kulinda barabara kuu ya kuingia mjini Kamembe mpaka pale atakapomaliza kuvivusha vikosi vyake na silaha salama mpaka upande wa pili wa ziwa Kivu hadi mjini Bukavu.
Na ikumbukwe kwa wakati huo Zaire ndio ilikua inaongoza afrika kwa kua na mtandao wa barabara mbovu sana kuliko maelezo.
Na kutokea upande ule wa kusini mwa ziwa Albert vikosi vya afande""f""_vilijisogeza mpaka upande wa Zaire katika mji wa Bukavu.
Na alipofika mjini Bukavu akawakuta wakuu wake wa kijeshi,chini ya serikali ya mpito iliyokua inaongozwa na raisi aliyepinduliwa na RPF Theodore Sindikubwabo.
Mzee Sindikubwabo mpaka anafariki yeye alikataa kabisa kukubali kua yale mauaji ya watusi yalikua genocide.Bali yeye anadai ilikua self defence ya wahutu.
Alikua ni bingwa wa kufanya mahojiano na alikua mtaalamu wa kukwepa maswali magumu na bingwa wa kuhalalisha chochote kile ambacho serikali yake ya mpito ilikifanya nchini Rwanda na hakujutia kwa lolote lile kwa kumaanisha
Maana alikua anapenda siasa za kinafiki sababu ya uchu wa madaraka
THEODORE SINDIKUBWABO
Mzee Theodore Sindikubwabo yeye alishiriki na kuandaa mikakati ya kuua watusi na alishirikiana na tajiri mkubwa mjini Chigali (Kigali) enzi hizo aitwae Felix Kabuga.
Hawa kwa kushirikiana na watu wengine wenye ushawishi kama Mama Agatha the first lady.
Mzee Sindikubwabo alikua na roho ya kikatili sana ,sababu alishuudia mauaji ya raia hasa watusi mjini Gitarama na mjini Kigeme,lakini yeye kama raisi wa mpito hakuwakemea intarehamwe waache kuua watu bali aliwachochea.
Na hii ndio ilifanya na wanajeshi wa RPF kua wanawaua wahutu kwa kulipiza kisasi,kwao ule mwaka waliochukua nchi kila muhutu alikua Intarehamwe,haijalishi ni mtoto au mtu mzima.
Huyo ndio mzee Theodore Sindikubwabo mwanasiasa aliyekimbilia Bukavu na serikali yake ya mpito na ambae afande""f"" anasema hakumuamini kabisa katika lolote ila halimueshimu kama mkuu wake wa kiheshi.
MAMA AGATHA.
Huyu alikua ndio mratibu wa mipango yote ya wanasiasa wenye misimamo mikali ambao walikataa kabisa kufikiria au kuwaza kua ipo siku watakuja kuondolewa madarakani na mahasimu wao kijeshi.
Alipanga na kuandaa mengi since 1987 na 1992.
Aghata alikua mwanamke anayependa madaraka kuliko hata familia yake binafsi,na alikua ni milionea kwa kujilimbikizia mali binafsi kwa wingi katika nchi ya ubelgiji na ufaransa,miaka yote ambayo famikia yake ilikua madarakani nchini Rwanda.
Na kwenye baraza la mawaziri la mumewe alikua na influence kubwa mno mpaka mwaka 1994.
FELIX KABUGA""DON KING""
Huyu alikua ndio mfadhili mkubwa wa shughuli za mama Aghata na Mzee Theodore.
Na aliitwa Don king kwa sababu alikua tajiri na alikua na pesa.Everyone in rwanda politics kipindi hicho walitegemea msaada wake kufanya mambo yao.
Alikua tycoon mfanyabiashara mkubwa na mtu wa watu.
Cha ajabu yeye binafsi alihusika na mauaji ya watu zaidi ya elfu nane na wote walikua ni jamii ya watusi,na alifadhili vipindi vya redio na magazeti ya kibaguzi vilivyochochea mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Nimewataja hawa watu wawili sababu wamehusiana kwa ukubwa na Mzee Theodore na huwezi kumtaja Mzee Theodore bila kuwataja wao.
Sasa nadhani umejua kwanini afande""f"" alikua hamwamini kabisa mzee Theodore Sindikubwabo kisiasa.
AFANDE""F"""
Afande"" f""anasema alikua hawaamini kabisa viongozi wake hao sababu walishiriki mauaji ya watusi wasio na hatia kwa tamaa zao za kisiasa.
Vilevile serikali ya Zaire ilikua inawapa presha waondoke maeneo ya Bukavu na kuelekea kaskazini zaidi.
Serikali ya Zaire haikutaka hali ya usalama iliyokua tete kivu ya kusini iendelee kua tete.
Maana katika kivu kusini tayari kulikua na makundi yanayoipinga serikali ya Mobutu japokua hayakua na nguvu kubwa za kijeshi.
Hapa nazungumzia makundi ya kikabila ya wabangu bangu na walende na wa mulenge.
Serikali ya Zaire chini ya mpambe wa Mobutu ambae alikua Kenge wa Dondo ilikua haina stratigic za kijeshi za kuweza kuzuia kuenea kwa huo uasi uliokua unamea taratibu na haikua tayari kupokea mzigo mwingine kutoka kwa banyarwanda,wakati wao masuala yao ya ndani nchini Zaire yalikua yanawaelemea na siasa zao za ndani toka ule uasi wa wanajeshi mjini kinshasa mwaka 1992 na 1993
Na vilevile serikali ya Zaire haikutaka kuingia katika ugomvi na mshirika wake mkubwa kibiashara,,hapa namaanisha serikali ya Uganda ambayo alikua ni mshirika mzuri kiusalama kwa eneo la mashariki mwa Zaire ya wakati huo chini ya Mobutu.
Ndio maana ilikua inawasukumiza waende kivu ya kaskazini na kuweka makambi yao huko karibu na kambi za kubwa za wakimbizi karibu na mji wa Goma na mpakani na Rwanda
Afande f anasema,kwa mara ya kwanza ndio alianza maisha ya ukimbizini huku akiwa kama mwanajeshi na sio raia.
Aliondoka mjini Bukavu na kusogea mjini Kalehe ambapo ndipo alijiandaa na mpango kazi wa kufungua kambi zake za kijeshi maeneo ya karibu na Goma.
ITAENDELEA............!!!!
Hii nchi ya Zaire ilikuwa na jeshi kweli? Jeshi la nchi nyingine linaingia bila vikwazo
 
Back
Top Bottom