Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,576
- 13,545
- Thread starter
- #221
KALEHE ZAIRE 1994
:Afande"F"" alikua amesogea mjini Kalehe yeye na logstic zake na adhima ilikua ni kuelekea mjini Goma.
Sasa kabla hatujamuelezea afande f na harakati zake,ebu tuutazame kidogo mji wa Kalehe.
Watu wengi wa nje ya zaire wataiona kalehe kama kamji kadogo,ila ndio mji mkubwa sana wa wafanyabishara wa biashara za magendo za madini.
Matajiri wengi wa mjini Goma walikua wanakuja kwenye mji huu ,,miaka ya 80,s ili kuuza na kununua madini.
Ni mji ambao ndio ulikua makazi na chimbuko la viongozi wengi wa maasi ya Kivu kaskazini na Kivu kusini.
Afande f na vikosi vyake vya wanajeshi wa kilichokua kikosi maalumu cha kumlinda rais,hawakutaka kukaaa sana mjini Kalehe,bali walipita nje ya mji wakati wakielekea mjini Goma.
Afande f anasema kua lengo lilikua ni kukaa sehemu ambazo walikua wamependekezewa na serikali ya Zaire,na hawakutaka migogoro na serikali ya Mobutu ya wakati huo.
GOMA ZAIRE 1994
Wakazi wa mji wa Goma walikua wameshazoea wimbi la wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi kwa miongo kadhaa,ila huu mwaka hali ilikua tofauti.
Kwanza mauaji ya kimbari ya jamii ya watusi yalikua yakutisha.
Pili mauaji ya jamii za kihutu ya kulipiza kisasi kwa watu wa jamii za kitusi yalitisha zaidi,maana baada ya kuchukua madaraka basi watusi nao walianza mauaji ya kulipiza visasi na walikua wanashirikiana bega kwa bega na wana mulenge wa Zaire.
Hii ni kwa mujibu wa mahojiano yangu na Afande""f"".
Mji wote wa Goma uligubikwa na habari hizo,pia na habari za kuanguka kwa utawala wa Kanali Habyrimana na habari pia za vikosi vya RPF vilivyokua vinafanya mauaji ya kutisha ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kimbari yaliyokua yanafanywa na vikosi vya intarehamwe na vya serikali iliyopinduliwa madarakani..Na wahutu wengi walikimbia kwa kuhofia usalama wa maisha yao na future yao chini ya utawala wa RPF.
Na watu wengi wa jamii za kihutu walikua wamevuka mpaka kama wakimbizi wakitokea Rwanda,na kiukweli hata hali ya kiusalama mjini humo ilikua tete.
KIGALI (CHIGALI) RWANDA.
Mjini Chigali kulikua na ile inayoitwa safisha safisha ya mabaki ya serikali iliyopinduliwa,iliyokua inaratibiwa na viongozi wa serikali ya RPF,lakini ukiangalia kwa undani zaidi utaona ilikua na mabaki ya ukabila na kulipiza kisasi zaidi dhidi ya Wahutu.
Raia walikamatwa na kuwekwa vizuizini na wengi kuuawa kwa tuhuma za kua ni intarehamwe au wafadhili wa intarehamwe.Hali hiyo ilifanya Wahutu wengi kuanza kukimbilia nje ya nchi wakihofia mauaji ya kulipizana visasi.
Wakati huohuo serikali ya RPF ilikua inajitahidi kujenga taswira yake mpya ya kimataifa nje ya Rwanda kama chama cha kisiasa zisizo za ubaguzi au ukabila.
Maisha yalikua sio mepesi mjini Kigali,sababu kila kitu kikiharibiwa na vita vilivyokua vinaelekea ukingoni ndani ya Rwanda.
Afande f anasema baada ya yeye na vikosi vyake kukaribia mji wa Goma,basi waliweka kambi yao nje kidogo ya mji wa Goma,ila karibu na kambi za wakimbizi mpakani na Rwanda.Alikua tayari kwa kujiandaa kuingia Rwanda kwa nguvu kurudisha himaya ya kiserikali iliyopotea.
Na upande wa pili upande wa Rwanda hali ilikua hivyo hivyo ,maana vikosi vya RPF vilikua vinajazana mpakani pia katika kuhofia kua kuna vikosi vya serikali iliyopinduliwa vinaweza kujaribu kutaka kurudi nchini Rwanda kuchukua madaraka tena kwa njia ya mtutu wa bunduki.
Afande """F""anasema namnukuu
VISASI UKABILA NI UGONJWA AMBAO UNASABABISHA MASUMBUKO MAKUBWA KWA RAIA WA KAWAIDA AMBAO HAWAJIUSISHI NA SIASA KATIKA LOLOTE LILE.***
Mwisho wa kumnukuuu""""""""""""
Hali ya kutoaminiana ilikua kubwa,pia chuki kati ya jamii za kinyarwanda ilikua kubwa pia.
GOMA ZAIRE:JULY 12 MPAKA JULY 20
Kulikua na wakimbizi wa kinyarwanda,wengi wao wahutu zaidi ya milioni moja mjini Goma wote wakikimbia mashambulizi ya ulipaji kisasi ya vikosi vya watusi vya RPF.
Na humo kulikuwamo na mchanganyiko wa wanajeshi wa serikali na vikosi vya intarehamwe na raia wa kawaida.Wote walijichanganya kwenye hayo makambi ya wakimbizi wakiwa wamevaa kiraia,ila na silaha zao mikononi mwao.
Na hilo jambo serikali ya RPF ilikua imeshaanza kulilalamikia na kutishia kuvamia Goma ili kuwaondoa hao watu katika kambi za wakimbizi walimokuwamo wamejichanganya na raia zaidi kwa kujificha na kuvaa kiraia.
Hata afande""f"" anadai kua na yeye pia hakupendezwa na vikosi vya intarehamwe na wanajeshi wa serikali kujichanganya na raia na kujifanya hawana hatia.
Kiufupi hali ya kiusalama mjini Goma ilikua tete na pia kulizuka uganjwa wa kipindupindu mjini Goma.
Haya yote yalikua maelezo ya Afande""F"" alipokua anajaribu kuelezea hali aliyoikuta mjini Goma kuanzia July 12 mpaka July 20 mjini Goma na masahibu aliyowakuta nayo zaidi ya wakimbizi milioni moja waliokimbilia nchini Zaire,katika kukwepa mauaji ya kulipiza kisasi yaliyokua yanafanywa na vikosi vya RPF dhidi ya wanamgambo wa intarehamwe na vikosi vya serikali ambavyo vilihusika na mauaji ya zaidi ya wanyarwanda milioni mbili na ushee hivi wenye asili ya Kitusi.
GOMA CITY ZAIRE 1994: ITAENDELEA!!!!!!!!!