Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

KALEHE ZAIRE 1994
:Afande"F"" alikua amesogea mjini Kalehe yeye na logstic zake na adhima ilikua ni kuelekea mjini Goma.
Sasa kabla hatujamuelezea afande f na harakati zake,ebu tuutazame kidogo mji wa Kalehe.
Watu wengi wa nje ya zaire wataiona kalehe kama kamji kadogo,ila ndio mji mkubwa sana wa wafanyabishara wa biashara za magendo za madini.
Matajiri wengi wa mjini Goma walikua wanakuja kwenye mji huu ,,miaka ya 80,s ili kuuza na kununua madini.
Ni mji ambao ndio ulikua makazi na chimbuko la viongozi wengi wa maasi ya Kivu kaskazini na Kivu kusini.
Afande f na vikosi vyake vya wanajeshi wa kilichokua kikosi maalumu cha kumlinda rais,hawakutaka kukaaa sana mjini Kalehe,bali walipita nje ya mji wakati wakielekea mjini Goma.
Afande f anasema kua lengo lilikua ni kukaa sehemu ambazo walikua wamependekezewa na serikali ya Zaire,na hawakutaka migogoro na serikali ya Mobutu ya wakati huo.
GOMA ZAIRE 1994
Wakazi wa mji wa Goma walikua wameshazoea wimbi la wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi kwa miongo kadhaa,ila huu mwaka hali ilikua tofauti.
Kwanza mauaji ya kimbari ya jamii ya watusi yalikua yakutisha.
Pili mauaji ya jamii za kihutu ya kulipiza kisasi kwa watu wa jamii za kitusi yalitisha zaidi,maana baada ya kuchukua madaraka basi watusi nao walianza mauaji ya kulipiza visasi na walikua wanashirikiana bega kwa bega na wana mulenge wa Zaire.
Hii ni kwa mujibu wa mahojiano yangu na Afande""f"".
Mji wote wa Goma uligubikwa na habari hizo,pia na habari za kuanguka kwa utawala wa Kanali Habyrimana na habari pia za vikosi vya RPF vilivyokua vinafanya mauaji ya kutisha ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kimbari yaliyokua yanafanywa na vikosi vya intarehamwe na vya serikali iliyopinduliwa madarakani..Na wahutu wengi walikimbia kwa kuhofia usalama wa maisha yao na future yao chini ya utawala wa RPF.
Na watu wengi wa jamii za kihutu walikua wamevuka mpaka kama wakimbizi wakitokea Rwanda,na kiukweli hata hali ya kiusalama mjini humo ilikua tete.
KIGALI (CHIGALI) RWANDA.
Mjini Chigali kulikua na ile inayoitwa safisha safisha ya mabaki ya serikali iliyopinduliwa,iliyokua inaratibiwa na viongozi wa serikali ya RPF,lakini ukiangalia kwa undani zaidi utaona ilikua na mabaki ya ukabila na kulipiza kisasi zaidi dhidi ya Wahutu.
Raia walikamatwa na kuwekwa vizuizini na wengi kuuawa kwa tuhuma za kua ni intarehamwe au wafadhili wa intarehamwe.Hali hiyo ilifanya Wahutu wengi kuanza kukimbilia nje ya nchi wakihofia mauaji ya kulipizana visasi.
Wakati huohuo serikali ya RPF ilikua inajitahidi kujenga taswira yake mpya ya kimataifa nje ya Rwanda kama chama cha kisiasa zisizo za ubaguzi au ukabila.
Maisha yalikua sio mepesi mjini Kigali,sababu kila kitu kikiharibiwa na vita vilivyokua vinaelekea ukingoni ndani ya Rwanda.
Afande f anasema baada ya yeye na vikosi vyake kukaribia mji wa Goma,basi waliweka kambi yao nje kidogo ya mji wa Goma,ila karibu na kambi za wakimbizi mpakani na Rwanda.Alikua tayari kwa kujiandaa kuingia Rwanda kwa nguvu kurudisha himaya ya kiserikali iliyopotea.
Na upande wa pili upande wa Rwanda hali ilikua hivyo hivyo ,maana vikosi vya RPF vilikua vinajazana mpakani pia katika kuhofia kua kuna vikosi vya serikali iliyopinduliwa vinaweza kujaribu kutaka kurudi nchini Rwanda kuchukua madaraka tena kwa njia ya mtutu wa bunduki.
Afande """F""anasema namnukuu
VISASI UKABILA NI UGONJWA AMBAO UNASABABISHA MASUMBUKO MAKUBWA KWA RAIA WA KAWAIDA AMBAO HAWAJIUSISHI NA SIASA KATIKA LOLOTE LILE.***
Mwisho wa kumnukuuu""""""""""""
Hali ya kutoaminiana ilikua kubwa,pia chuki kati ya jamii za kinyarwanda ilikua kubwa pia.
GOMA ZAIRE:JULY 12 MPAKA JULY 20
Kulikua na wakimbizi wa kinyarwanda,wengi wao wahutu zaidi ya milioni moja mjini Goma wote wakikimbia mashambulizi ya ulipaji kisasi ya vikosi vya watusi vya RPF.
Na humo kulikuwamo na mchanganyiko wa wanajeshi wa serikali na vikosi vya intarehamwe na raia wa kawaida.Wote walijichanganya kwenye hayo makambi ya wakimbizi wakiwa wamevaa kiraia,ila na silaha zao mikononi mwao.
Na hilo jambo serikali ya RPF ilikua imeshaanza kulilalamikia na kutishia kuvamia Goma ili kuwaondoa hao watu katika kambi za wakimbizi walimokuwamo wamejichanganya na raia zaidi kwa kujificha na kuvaa kiraia.
Hata afande""f"" anadai kua na yeye pia hakupendezwa na vikosi vya intarehamwe na wanajeshi wa serikali kujichanganya na raia na kujifanya hawana hatia.
Kiufupi hali ya kiusalama mjini Goma ilikua tete na pia kulizuka uganjwa wa kipindupindu mjini Goma.
Haya yote yalikua maelezo ya Afande""F"" alipokua anajaribu kuelezea hali aliyoikuta mjini Goma kuanzia July 12 mpaka July 20 mjini Goma na masahibu aliyowakuta nayo zaidi ya wakimbizi milioni moja waliokimbilia nchini Zaire,katika kukwepa mauaji ya kulipiza kisasi yaliyokua yanafanywa na vikosi vya RPF dhidi ya wanamgambo wa intarehamwe na vikosi vya serikali ambavyo vilihusika na mauaji ya zaidi ya wanyarwanda milioni mbili na ushee hivi wenye asili ya Kitusi.
GOMA CITY ZAIRE 1994: ITAENDELEA!!!!!!!!!
Screenshot_20231115-025549.png
Screenshot_20231115-025706.png

Screenshot_20231115-025631.png
 
Kwa mara ya kwanza naelewa historian ya rwanda toka miaka ya 80, uhasama wa FDLR vs RPF... Lakini nishapata picha chimbuko la M23 na Mengineyo. Kimsingi niseme ahsante kwa mtoa huu Uzi. Umetufungua wengi macho hasa sisi kizazi Cha 90's
Shukurani mkuu na ndio kazi ya waandishi habari huru
 
Mkuu Kagame safi sana kwa uzi huu mujarabu....
Kuna maswali machache naomba sana unisaidie hapa....

1.Rwigema alikua Boss wa PJK...baada ya kuuawa wale watu waliokua loyal kwa rwigema hawakufanya kitu au na wao walikua wiped out.
?

2.Nini kilimpata mama Agatha..je afande F alimlinda kama alivyombwa na Late big Boss...

3.Hii Cabal ya The Don kabugo mama agatha na boss wako wa jeshini muheshimiwa habyarimana hakujua ipo au aliziba macho..

4.Mahusiano ya Mzee Kabila na PK ulikuaje kipindi hicho najua mzee alikua anapambana mida hiyo....

5.kwa Ukubwa wa Jeshi La Tanzania je Huoni kwamba tulikua tunaweza kufanya intervention kwa muda mfufi na tukazuia mauaji kwa kiasi kikubwa mauaji ya kimbari..?
 
Mda si mrefu naweka vitu.
Lakini usome uzi wangu mwingine wa risasi sio suluhisho 1996
Bro nitag asee kwenye uzi huo. Ujue hapa tz kwa sasa hii generation ya tz haijui lolote kuhusu huu mgogoro wa maziwa makuu. Nimewai kukaa hata na vijana wadogo wa idara ile nyeti hapa tz ni weupo kuhusu migogoro ya nchi za maziwa makuuu hawajui lolote nikasema hiiiiiiiiiiii
 
Bro nitag asee kwenye uzi huo. Ujue hapa tz kwa sasa hii generation ya tz haijui lolote kuhusu huu mgogoro wa maziwa makuu. Nimewai kukaa hata na vijana wadogo wa idara ile nyeti hapa tz ni weupo kuhusu migogoro ya nchi za maziwa makuuu hawajui lolote nikasema hiiiiiiiiiiii
Andika tu risasi sio suluhisho 1996
 
Mkuu Kagame safi sana kwa uzi huu mujarabu....
Kuna maswali machache naomba sana unisaidie hapa....

1.Rwigema alikua Boss wa PJK...baada ya kuuawa wale watu waliokua loyal kwa rwigema hawakufanya kitu au na wao walikua wiped out.
?

2.Nini kilimpata mama Agatha..je afande F alimlinda kama alivyombwa na Late big Boss...

3.Hii Cabal ya The Don kabugo mama agatha na boss wako wa jeshini muheshimiwa habyarimana hakujua ipo au aliziba macho..

4.Mahusiano ya Mzee Kabila na PK ulikuaje kipindi hicho najua mzee alikua anapambana mida hiyo....

5.kwa Ukubwa wa Jeshi La Tanzania je Huoni kwamba tulikua tunaweza kufanya intervention kwa muda mfufi na tukazuia mauaji kwa kiasi kikubwa mauaji ya kimbari..?
Nakujibu mkuu kama ifuatavyo
1: RWIGEMA WAS SOROUNDED WITH CON PEOPLE WHO ONLY CARE FOR POWER
2:SHE ESCAPE TO FRANCE
3: THERE'S NOTHING HE CAN DO
4:THEY USED TO BE COMRADE IN FRONTLINE 1996 TO 1998
5:FEW ELITE UNIT WAS THERE TO PROTECT EMBASSY.
TO INTERFERE NO BECAUSE OF FRANCE MILITARY PRESENCE UP THERE
 
KAMEMBE NEAR LAKE KIVU.......!!!
NAENDELEA.........!!!
Afande"f" anasema kua aliona hakuna maisha tena Rwanda kwa wakati ule,maana uwepo wa wanajeshi wa umoja wa mataifa na wanajeshi wa ufaransa na wa uganda na ushindi wa vikosi vya RPF ulimfanya plan A aliyokua nayo aachane nayo na afuate plan B.
Toka mjini Kamembe plan ikawa ni kuvusha magari yote ya kijeshi na vifaru na yale marolo ya logstic kwa kupitia njia isiyo rasmi ya Cyangugu,ila wale wanajeshi kikosi kizima wakavuka upande ule wa ziwa mpaka upande wa pili wa nchi ya Zaire.
Shughuli hii nzito ilimchukua wiki nzima kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na wakati huo huo alikua anazuia askari wa RPF wasiweze kumsogelea mjini Kamembe na alituma vikosi vya asikari kulinda barabara kuu ya kuingia mjini Kamembe mpaka pale atakapomaliza kuvivusha vikosi vyake na silaha salama mpaka upande wa pili wa ziwa Kivu hadi mjini Bukavu.
Na ikumbukwe kwa wakati huo Zaire ndio ilikua inaongoza afrika kwa kua na mtandao wa barabara mbovu sana kuliko maelezo.
Na kutokea upande ule wa kusini mwa ziwa Albert vikosi vya afande""f""_vilijisogeza mpaka upande wa Zaire katika mji wa Bukavu.
Na alipofika mjini Bukavu akawakuta wakuu wake wa kijeshi,chini ya serikali ya mpito iliyokua inaongozwa na raisi aliyepinduliwa na RPF Theodore Sindikubwabo.
Mzee Sindikubwabo mpaka anafariki yeye alikataa kabisa kukubali kua yale mauaji ya watusi yalikua genocide.Bali yeye anadai ilikua self defence ya wahutu.
Alikua ni bingwa wa kufanya mahojiano na alikua mtaalamu wa kukwepa maswali magumu na bingwa wa kuhalalisha chochote kile ambacho serikali yake ya mpito ilikifanya nchini Rwanda na hakujutia kwa lolote lile kwa kumaanisha
Maana alikua anapenda siasa za kinafiki sababu ya uchu wa madaraka
THEODORE SINDIKUBWABO
Mzee Theodore Sindikubwabo yeye alishiriki na kuandaa mikakati ya kuua watusi na alishirikiana na tajiri mkubwa mjini Chigali (Kigali) enzi hizo aitwae Felix Kabuga.
Hawa kwa kushirikiana na watu wengine wenye ushawishi kama Mama Agatha the first lady.
Mzee Sindikubwabo alikua na roho ya kikatili sana ,sababu alishuudia mauaji ya raia hasa watusi mjini Gitarama na mjini Kigeme,lakini yeye kama raisi wa mpito hakuwakemea intarehamwe waache kuua watu bali aliwachochea.
Na hii ndio ilifanya na wanajeshi wa RPF kua wanawaua wahutu kwa kulipiza kisasi,kwao ule mwaka waliochukua nchi kila muhutu alikua Intarehamwe,haijalishi ni mtoto au mtu mzima.
Huyo ndio mzee Theodore Sindikubwabo mwanasiasa aliyekimbilia Bukavu na serikali yake ya mpito na ambae afande""f"" anasema hakumuamini kabisa katika lolote ila halimueshimu kama mkuu wake wa kiheshi.
MAMA AGATHA.
Huyu alikua ndio mratibu wa mipango yote ya wanasiasa wenye misimamo mikali ambao walikataa kabisa kufikiria au kuwaza kua ipo siku watakuja kuondolewa madarakani na mahasimu wao kijeshi.
Alipanga na kuandaa mengi since 1987 na 1992.
Aghata alikua mwanamke anayependa madaraka kuliko hata familia yake binafsi,na alikua ni milionea kwa kujilimbikizia mali binafsi kwa wingi katika nchi ya ubelgiji na ufaransa,miaka yote ambayo famikia yake ilikua madarakani nchini Rwanda.
Na kwenye baraza la mawaziri la mumewe alikua na influence kubwa mno mpaka mwaka 1994.
FELIX KABUGA""DON KING""
Huyu alikua ndio mfadhili mkubwa wa shughuli za mama Aghata na Mzee Theodore.
Na aliitwa Don king kwa sababu alikua tajiri na alikua na pesa.Everyone in rwanda politics kipindi hicho walitegemea msaada wake kufanya mambo yao.
Alikua tycoon mfanyabiashara mkubwa na mtu wa watu.
Cha ajabu yeye binafsi alihusika na mauaji ya watu zaidi ya elfu nane na wote walikua ni jamii ya watusi,na alifadhili vipindi vya redio na magazeti ya kibaguzi vilivyochochea mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.
Nimewataja hawa watu wawili sababu wamehusiana kwa ukubwa na Mzee Theodore na huwezi kumtaja Mzee Theodore bila kuwataja wao.
Sasa nadhani umejua kwanini afande""f"" alikua hamwamini kabisa mzee Theodore Sindikubwabo kisiasa.
AFANDE""F"""
Afande"" f""anasema alikua hawaamini kabisa viongozi wake hao sababu walishiriki mauaji ya watusi wasio na hatia kwa tamaa zao za kisiasa.
Vilevile serikali ya Zaire ilikua inawapa presha waondoke maeneo ya Bukavu na kuelekea kaskazini zaidi.
Serikali ya Zaire haikutaka hali ya usalama iliyokua tete kivu ya kusini iendelee kua tete.
Maana katika kivu kusini tayari kulikua na makundi yanayoipinga serikali ya Mobutu japokua hayakua na nguvu kubwa za kijeshi.
Hapa nazungumzia makundi ya kikabila ya wabangu bangu na walende na wa mulenge.
Serikali ya Zaire chini ya mpambe wa Mobutu ambae alikua Kenge wa Dondo ilikua haina stratigic za kijeshi za kuweza kuzuia kuenea kwa huo uasi uliokua unamea taratibu na haikua tayari kupokea mzigo mwingine kutoka kwa banyarwanda,wakati wao masuala yao ya ndani nchini Zaire yalikua yanawaelemea na siasa zao za ndani toka ule uasi wa wanajeshi mjini kinshasa mwaka 1992 na 1993
Na vilevile serikali ya Zaire haikutaka kuingia katika ugomvi na mshirika wake mkubwa kibiashara,,hapa namaanisha serikali ya Uganda ambayo alikua ni mshirika mzuri kiusalama kwa eneo la mashariki mwa Zaire ya wakati huo chini ya Mobutu.
Ndio maana ilikua inawasukumiza waende kivu ya kaskazini na kuweka makambi yao huko karibu na kambi za kubwa za wakimbizi karibu na mji wa Goma na mpakani na Rwanda
Afande f anasema,kwa mara ya kwanza ndio alianza maisha ya ukimbizini huku akiwa kama mwanajeshi na sio raia.
Aliondoka mjini Bukavu na kusogea mjini Kalehe ambapo ndipo alijiandaa na mpango kazi wa kufungua kambi zake za kijeshi maeneo ya karibu na Goma.
ITAENDELEA............!!!!
Kuna huyo felix kabuga lakini kuna mwingine ROBERT KAJUGA. It is all white truth that KAJUGA ROBERT alikuwa royal kwa inkontanyi ya PK. How Kajuga the tutsi tycoon in Kigal funded Intarahamwe ya wahutu. And all missions za intarahamwe ambazo zilikuwa funded na KAJUGA zilikuwa open book kwa PK at his finger tips.
Kajuga alikuwa chawa wa PK.
 
Kuna huyo felix kabuga lakini kuna mwingine ROBERT KAJUGA. It is all white truth that KAJUGA ROBERT alikuwa royal kwa inkontanyi ya PK. How Kajuga the tutsi tycoon in Kigal funded Intarahamwe ya wahutu. And all missions za intarahamwe ambazo zilikuwa funded na KAJUGA zilikuwa open book kwa PK at his finger tips.
Kajuga alikuwa chawa wa PK.
Kajuga was double agent mkuu
 
Kuna huyo felix kabuga lakini kuna mwingine ROBERT KAJUGA. It is all white truth that KAJUGA ROBERT alikuwa royal kwa inkontanyi ya PK. How Kajuga the tutsi tycoon in Kigal funded Intarahamwe ya wahutu. And all missions za intarahamwe ambazo zilikuwa funded na KAJUGA zilikuwa open book kwa PK at his finger tips.
Kajuga alikuwa chawa wa PK.
Na vipi yule Georges Lutaganda..
 
Back
Top Bottom