Kiukweli jana nilibarikiwa sana na mahubiri ya askofu mkuu mstaafu wa Kanisa Anglican Donald Mtetemela aliyoyatoa kwenye mkutano mkuu wa Sinodi ya DMP katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach.
Kwamba William Wilberfoce aliingia bungeni huko Uingereza na kujenga hoja zilizopelekea biashara ya utumwa duniani kukomeshwa na yule mmiliki wa meli za kusafirisha watumwa akaokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa bwana na mwokozi wake.
Baba askofu amesisitiza Yesu anatutaka sisi waumini wa Kanisa kuwa nuru ya Ulimwengu.
Natangaza kuachana na siasa za kishabiki na nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM.
Ngoja nichukue clip ya mahubiri hapo Upendo TV niwawekee.
Mungu wa mbinguni awabariki!
Kila siku nakukumbushia hili.
Zaburi 1: 1 - 6
1.Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2.Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3.Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
4.Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5.Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6.Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.