Mahubiri ya Baba Askofu Mtetemela pale KKKT Mbezi Beach yamenishawishi kuachana na siasa za "Kishabiki"

Mahubiri ya Baba Askofu Mtetemela pale KKKT Mbezi Beach yamenishawishi kuachana na siasa za "Kishabiki"

Kwani kuwa mwanaccm ni dhambi mbele za Mungu?!!
Kuwa mwanachama wa chama chochote au kikundi chochote siyo dhambi alimradi tu chama hicho au kikundi hicho kiwe na nia iliyo njema.

Lakini kwa CCM ya sasa nina mashaka makubwa kama kweli ni chama cha siasa. Kwa kiasi kikubwa kimekuwa kama genge la wahalifu. Kama fikra zangu ni sahihi, kuwa mmoja wa wanachama katika kundi la kihalifu, hata usipokuwa mhalifu, utakuwa ni sehemu ya uhalifu kwa sababu unasaidia kuongeza nguvu ya uhalifu.

Kwa sasa, chama hiki CCM, ndiyo kimekuwa chanzo cha mauaji ya watu wasio na hatia. Chama hiki kimekuwa chanzo cha watu wasiojulikana ambao wanaua, wanateka, wanatesa, wanajeruhi na wanapoteza watu. Wengi waliomo kwenye kundi hili ni greenguards. Je, wewe unafurahia kuwa sehemu ya wanaoua bindamu wenzako?

Binafsi kama ningekuwa nina tamaa ya cheo, ningekuwa mmoja wa viongozi katika serikali iliyopita na hii ya sasa. Nimeshawishiwa na watu wengi wenye mamlaka mara kadhaa lakini amani yangu zaidi ipo katika jitihada zangu za kutaka kuwa mtu mwema mbele ya binadamu wenzangu na Mungu wangu. Cheo na madaraka kwa njia chafu, ni takataka na ni chukizo mbele za Mungu na wanadamu wema.

Usiishie tu kuacha siasa za kishabiki bali ujitahidi wakati wote kusimama na watu wenye haki kuliko wadhulumu haki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuwa mwanaccm ni dhambi mbele za Mungu?!!

Umesema unaachana na siasa za ushabiki huku unasema unabaki kuwa mwana-CCM.

Sasa kama unaacha siasa za kishabiki, ni kwanini usiache kuwa mwanachama wa chama chochote ?

Huwezi kusema unaachana na siasa za kishabiki huku unasema unabaki kuwa mwana-CCM.
 
Huyo askofu namsikia toka kitambo sana alipokuwa anapita kuelekea Milo Ludewa. Jina lake ni kubwa sana.
 
Kiukweli jana nilibarikiwa sana na mahubiri ya askofu mkuu mstaafu wa Kanisa Anglican Donald Mtetemela aliyoyatoa kwenye mkutano mkuu wa Sinodi ya DMP katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach.

Kwamba William Wilberfoce aliingia bungeni huko Uingereza na kujenga hoja zilizopelekea biashara ya utumwa duniani kukomeshwa na yule mmiliki wa meli za kusafirisha watumwa akaokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa bwana na mwokozi wake.

Baba askofu amesisitiza Yesu anatutaka sisi waumini wa Kanisa kuwa nuru ya Ulimwengu.

Natangaza kuachana na siasa za kishabiki na nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM.

Ngoja nichukue clip ya mahubiri hapo Upendo TV niwawekee.

Mungu wa mbinguni awabariki!
So chadema watapumua Sasa sio[emoji1787][emoji1787]

Bila Shaka mbinguni watakatifu watapiga vigelegele[emoji3577]
 
Back
Top Bottom