Mahusiano kati ya namba ya NIDA na mfumo wa ajira yakoje? Dogo kazinguliwa ajira mpya, naomba ushauri wenu

Mahusiano kati ya namba ya NIDA na mfumo wa ajira yakoje? Dogo kazinguliwa ajira mpya, naomba ushauri wenu

majina ya cheti cha kuzaliwa ni mawili na vyeti vingine mawili ila NIDA matatu
Cheti cha kuzaliwa lazima yawe matatu maana jina la Baba lazima liwe ELIAS MMASI, halafu la mtoto JOYCE.

Kwa hiyo hapo mtoto atajulikana kama JOYCE ELIAS MMASI(hili jina ndio linakuwa na NIDA, kwa sababu wakati wa kuandikishwa NIDA huwa wanatumia vyeti vyakuzaliwa).
 
ndio maana kukuta nida na cheti cha kuzaliwa yanatofautiana ni ngumu sana ila kipengele ni vyeti vya shule
 
wamepokelewa kimakosa... amini ninacho kwambia...
Kama ni hivyo basi wengi tupo kwenye msala.

Nakumbuka chimbuko la majina mawili/matatu kwenye vyeti limeanzia form 2 kwa sababu tulipofika form 4 tulitakiwa kusajili majina yetu kama tulivyosajili wakati tunafanya mtihani wa form 2.

Darasa letu(kwenye shule niliyosoma) asilimia 99% tuliandikisha majina 2 ambayo yameendelea kuonekana kwenye vyeti vyetu hadi tunahitimu chuo(kwa waliofika huku). Wakati huo huo vyeti vyetu vya kuzaliwa vina majina 3 na sijawahi kuona utata unaousema wewe hapa kuwa itakuwa ni watu tofauti.

Kwenye mfumo wa Application wa online huwa unataka mtu aandike namba ya kidato cha 4 halafu mfumo utascan data kutoka NECTA na majina yako yataonekana pamoja na shule uliyosoma(ambayo ni 2 au 3), hapo hapo pia ukiingiza namba ya NIDA huwa ni mwanzoni kabisa itakuleta majina 3 uliyosajiliwa NIDA. Sasa iweje wakatae? lazima kuna tatizo, wachunguze vizuri
 
mkuu huwenda kuna kitu kingine labda, maana wapo walioripoti na wana majina mawili kwenye vyeti na nida matatu ila wamepokelewa
Mimi ni mmoja wao. Labda kama yeye kulikuwa na shida sehemu nyingine. Mi vyeti vya taaluma vyoote vi3 ni majina mawili lkn nida ni ma3 na ilikubali bila shida yoyote.
 
wamepokelewa kimakosa... amini ninacho kwambia...
Mfumo ndo umekosea? Maana ukisema kimakosa siyo tatizo la wapokeaji, basi na walioajiri waliajiri kimakosa. Huwezi kuajiri NIDA huku vyeti vya taaluma ukiona majina hayapo ma3 kama ya NIDA unayohitaji.
 
Dogo ni mwalimu idara ya msingi,

majina yake ya vyeti vyote ni MARIAM ELIAS (mfano)

Majina ya Nida ni MARIAM ELIAS MMASA.

wakati wa kuomba ajira Tamisemi details zilikubali vizuri kabisa na mimi ndiye nilimuombea,

selection zimetoka kachaguliwa lakini halmashauri wanamiweka kwenye mfumo eti nida inagoma!

Tunashangaa hata sisi, sababu inaweza kuwa ipi, wazoefu tatizo linaeza kuwa nn details zimepishana wapi
Andika taarifa zieleweke watu wamsaidie huyo ukificha haina maana
 
mkuu huwenda kuna kitu kingine labda, maana wapo walioripoti na wana majina mawili kwenye vyeti na nida matatu ila wamepokelewa
Nahisi hapo kuna hila inataka kufanyika!! Anaweza kupokonywa nafasi kwa hila. Cheti cha kuzaliwa kina majina yote ya baba. Kwa mfano: Vyeti- John Makoye, Jina la baba- Alfonce Makoye. Jina la mtoto NIDA- John Alfonce Makoye.

Hapo huwezi kumwambia mtoto NIDA imegoma, kama ukilinganisha na cheti chake cha kuzaliwa.
 
Mfumo wa majina matatu ulipaswa utumike tangu zamani.

Mifumo mipya ya seriksli inaleta tabu kwa watu tuliosoma zamani enzi za majina mawili
 
majina ya cheti cha kuzaliwa ni mawili na vyeti vingine mawili ila NIDA

Kama ni hivyo basi wengi tupo kwenye msala.

Nakumbuka chimbuko la majina mawili/matatu kwenye vyeti limeanzia form 2 kwa sababu tulipofika form 4 tulitakiwa kusajili majina yetu kama tulivyosajili wakati tunafanya mtihani wa form 2.

Darasa letu(kwenye shule niliyosoma) asilimia 99% tuliandikisha majina 2 ambayo yameendelea kuonekana kwenye vyeti vyetu hadi tunahitimu chuo(kwa waliofika huku). Wakati huo huo vyeti vyetu vya kuzaliwa vina majina 3 na sijawahi kuona utata unaousema wewe hapa kuwa itakuwa ni watu tofauti.

Kwenye mfumo wa Application wa online huwa unataka mtu aandike namba ya kidato cha 4 halafu mfumo utascan data kutoka NECTA na majina yako yataonekana pamoja na shule uliyosoma(ambayo ni 2 au 3), hapo hapo pia ukiingiza namba ya NIDA huwa ni mwanzoni kabisa itakuleta majina 3 uliyosajiliwa NIDA. Sasa iweje wakatae? lazima kuna tatizo, wachunguze vizuri
mtafute mwanasheria aliye karibu nawe atakusaidia... maana hutaki kuelewa kuwa ni makosa...

una fahamu kufanya biashara katika gari ni makosa? lakini watu wana fanya, kununua bidhaa barabarani ukiwa kwenye gari/basi ni makosa lakini watu wana nunua... ndio nchi yetu...

unapo ambiwa ni umekosea na una taka halalisha makosa kwa namna yako sina neno ila jifunze kuona namna gani una jifunza ili makosa yasijilejee

taasisi nyingi kama mabenki ukipeleka taarifa zenye mkanganyiko kama hivi wa majina ni ngumu kukufungulia acc... maana ni watu wawili tofauti... nida jina lingine na cheti cha kuzaliwa ni jina lingine...
 
Cheti cha Kuzaliwa na NIDA hayatofautiani kwa sababu wakati unaadikishwa NIDA walitumia cheti cha kuzaliwa.

Ebu tuambie kuna kosa gani kuwa na majina 2 kwenye vyeti halafu ukawa na majina 3 kwenye cheti cha kuzaliwa na NIDA?
 
Abdul Juma sio Abdul Juma Salum

AU

Salehe Fikiri sio Salehe Mabrouk Fikiri

nazani utakuwa umeelewa sasa... kwa maana kuwa sajili ni kuajili watu wawili ktk nafasi moja...
 
Abdul Juma sio Abdul Juma Salum

AU

Salehe Fikiri sio Salehe Mabrouk Fikiri

nazani utakuwa umeelewa sasa... kwa maana kuwa sajili ni kuajili watu wawili ktk nafasi moja...
Ninatumia majina 2 kwenye vyeti na siku zote huwa natambulika kwa majina 2, sijawahi kupata kikwazo chochote unachokisema wewe ingawa kwenye NIDA nina majina 3 ambayo chimbuko lake ni cheti cha kuzaliwa.

Kuna siku nilitembelea ofisi ya utumishi, kwenye daftari la kurecord watu wanaokuja na kuelezea shida zao ili watatuliwe niliandika majina 2 pia nikamuambia mtumishi aliyenipa hilo daftari kuwa ninatumia majina 2 ingawa kwenye NIDA ni 3, kwa sababu nilihitajika kuandika namba ya NIDA, aliniambia hamna tatizo.
 
mtoa mada labda kama kuna yatizo lingne kabisa majina mawili kwenye vyeti haina shida yoyote kama jina la tatu kwenye kitambulisho cha nida na cheti cha kuzaliwa yanafanana

mfano cheti cha kuzaliwa yanatakiwa yasomeke
birth name Mariam
jina la baba elias mmasa

hapa hakuna shida yoyote ile ila

majina ya kwenye vyeti yakitofautiana hata herufi moja kwenye nida umeenda na maji maana nida kubadilisha ni mlolongo ila cheti cha kuzaliwa kubadili ni simple

mfano nida Mariam elius mmasa
vyeti mariam elias
yaani elias na elius zikatofautiana iyo a na u ni kwisha

mwisho vyeti vikiwa na majina mawili halafu nida majina matatu hamna tatizo lolote lile sema jina la tatu la nida liwe sawasawa na jina la tatu kwenye cheti cha kuzaliwa
mkuu embu nisaidie na mimi kimawazo,mimi majina yangu ya vyeti vya taalumu ni “hance prosper paul” cheti cha nida ni “hance prosper massawe” ila majina yote hayo yapo kwenye cheti cha kuzaliwa ni kwamba nida walitumia jina la ukoo badala ya jina la babu,je kunachangamoto yotote itayonikumba hasa kwenye application za kazi?? nini nifanye?,natanguliza shukrani zangu aksante
 
Inabidi uwaambie NIDA watoe Massawe waweke Paul
 
Back
Top Bottom