Habarini za humu Wana Jf wote!
Niwape hongera kwa ufafanuzi mzuri wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa na sintofahamu.
Binafsi nina suala kama hilo, japo sijabahatika kupata ajira zilizopita, ila huwa nawaza itakuwaje siku nikipata, Ni hivi...
Vyeti vyangu vyote vina majina matatu pamoja na kitambulisho cha NIDA, na yapo sahihi kabisa(yanaendana) ila shida ni zile namba za mwanzoni kwenye kitambulisho zile 4,ambazo huendana na Mwaka wa kuzaliwa zipo tofauti na zile za kwenye cheti cha kuzaliwa, mfano, 1989XXXX....,katika NIDA, ilihali Mwaka kwenye cheti ni 1987,....
je hii haiwezi kuja kuleta shida pindi niliingia kwenye mfumo wa ajira?