Mahusiano mabaya aliyopitia Kasinde kwenye maisha yake (uhalisia)

Umezua mjadala mwengine bila kujua kuufunika ...........

"Jamaa aliyenitoa bikira akaniambia hapa hatuna la kufanya turudi nyumbani tukaendelee kupoozana kesho alfajiri unaondoka na gari za Mombasa saa moja na nusu uko Tanga unaingia kazini."

Haya tuambie kumbe watoa bikra wana special place kwenye mioyo ya watu?
 
Ubaya wa wanaume wapigaji ni kuwa wanajua kubembeleza....kujitoa kwao ni hadi upate msaada wa Mungu.
Unakuwa na mtu anakupiga matukio lakini umo tu.
Siku ukifanikiwa kutoka unajiuliza hivi ilikuwa akili yangu ama kumbe kuna kitu kulikuwa kinakusababisha uwe pale ambapo kwingine huwezi kukipata.
 
Kuna point umesema kwamba akina baba waongee vizuri na watoto wao wa kike kujua maswahibu wanayokutana nayo na kuwapa msaada na kama siyo wao basi kaka wachukue nafasi.

Mimi binafsi huwa sipendi kuona mtoto wa kike akinyanyasika mbele yangu halafu nishindwe kumsaidia, huwa ninaingilia ugomvi kwasababu mama yangu aliwahi kusema 'tangia niwe na baba yako sikuwahi kupigwa hata kibao '

Kuna mzee mmoja aliwahi kunambia hata siku moja usikubali mwanamke akanyanyasika na kuonewa mbele yako,ukimuacha bila kumsaidia utaonekana dhaifu.

Sasa dada yangu mmojawapo aliolewa, akapata watoto ,baadaye mwanaume akaanza kumzingua akimuona hana maana tena, kesi zote napewa mimi, nilivyovumilia nikachoka, siku moja nilikwenda na gari la mizigo nikamwambia fungasha kila kilicho chako nakurudisha nyumbani.

Yeye na watoto wake mpaka leo hii wapo nyumbani nilichomwambia kama atahitaji kuona watoto aje hapa hapa nyumbani maana hawezi kukunyanyasa ukiwa kwenu, shemeji yangu sikuwahi kumwambia chochote na huwa tukikutana ni salamu na story as if hakijatokea kitu.

Kwahiyo kaka ku- act kuisadia jinsia ya kike haijalishi ni mkubwa kwako au mdogo cha msingi simama kwenye uanaume wako. Nyinyi mnatutegemea sana kwenye kuwapa miongozo.

Pole sana Kasie.
 
Pole sana Kasie
 
Kuna limjomba langu hua linampiga mke wake, natamani siku niende kwake alaf lianzishe timbwili niingilie nizichape nalo
Wewe mnyamwezi chunga laana inakusogelea. Upigane na mjombako unajua anayoyapitia kwa huyo mke wake? Shenzi kabisa
 
Kuna uzi nilisema. Mahusiano yanayovunjwa na mwanaume hayafi, ila mwanamke akisema never imeisha.
 
Pole! Nusu ya maisha imekwenda hivi hivi! Ila yote ni maisha, haya na kanuni!
 
Chai Yako ya moto mwaka 1990 upate simu ya mkononi we mrembo acha utani
 
Amekwishajibu na hakujibu hivi. Mnapenda sana uongo. Unatamani kuongopa kwa niaba ya mtu mwingine!! Loh!! Unapata raha gani lakini?
Hakusema kuwa 1990 alikuwa na cell phone, na uhusiano ulidumu miaka 10.
 
Naelezeaga nusunusu, huwa sipendi kuzungumzia uhalisia wangu wote humu, hamna msaada wowote humu zaidi ya bullying tu,

Sio tu bullying, watu humu wanajiona wasafi kila sekta ni vile tuu mambo yao hayajulikani.

Kikubwa usijifungamanishe na maisha ya mtu. Kila mtu akale, kuoga na kulala kwake.

Humu inabaki story tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…