"....Nina mwezi wa 3 sasa sijamruhusu kunigusa"...!
Ni jana tulikuwa na mkasa wa aina hii ukiwa umeletwa na mdada ambaye ni family friend wetu, kisa amepata habari kuwa bwanake ambaye anafanya kazi na kontrakta wa barabara ya Arusha-Namanga, ana mahusiano na mwanadada mwingine...
Kwa ufupi ni wazi silaha hiyo ya kunyimana tendo takatifu la ndoa ni ya hatari sana...maana party inayolalamika lazima itatafuta namna fulani ya kumkomoa mwenzie kwa kuwa na mahusiano ya tofauti nje ya ndoa, halafu meli yote inakuwa inazama taratibu...
Maongezi ni ufunguo...familia zipate wakati muafaka wa KUSEMEZANA...kwa mazuri na mabaya, hapo mndipo miarobaini ya shida zote itatolewa.