Mkuu, umenyumbulisha kwa ustadi wa hali ya juu sana.
Kusema ukweli, huyu binti ananiheshimu sana. Yani kuna wakati huwa navunga nimechukia, mara zote huwa anashuka na kuniomba msamaha, tena kwa upole mno, no arrogance at all.
Nimewahi kumtania mara kadhaa kuhusu kuishi nae, hakukataa. Alichosema nimpe muda aendelee kuniamini.
Likizo ya juzi nilibahatika kukutana na mwanae, akanitambulisha. Ila kuna kitu kilinipa moyo, manake alinielezea tabia za huyo mtoto wake wa kiume kwamba anafanya vizuri sana darasani ila he is too demanding, yani akitaka kitu anataka hapohapo, sasa yeye anakereka anasema hawezi kumlea mtoto hivyo hata kama anacho, kwasababu akimzoesha halafu ikatokea siku kakosa mtoto hatamuelewa. Nikamuahidi nitazungumza na dogo, ilikuwa too late coz dogo alisharudi Shule.
Kwa kifupi ni kama ananielewa ingawa simuamini sana. Pia ameniomba nimsindikize kwa mwanae siku ya visiting day, anataka nikaongee nae siku hiyo kama mwanaume mwenzangu.
She is cooperative, understanding and humble. Sema ni vile tu moyo wa mtu ni kichaka mkuu [emoji28]
Sent using
Jamii Forums mobile app