Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Nakupa zoezi dogo sana...Tembelea huyo mtoto wake shule, jifanye wewe ni rafiki wa babake then fanya kama mwanamme utapata ukweli wote wa lini babake ameonana nae, vp anamkubali nani zaidi baba au mama..
Tofauti na hapo kuna hatari inakuja mbele yako, wanaomwona huyo sister wako wengi sana au unadhani kitu gani anakificha hadi bodabada amwone kuwa ni wife materials?
 
Hapa unatakiwa ucheze kete vizuri mkuu
 
Aisee [emoji119]

Nimekuelewa sana mkuu. Una hoja.

Ngoja nifanye kama ulivyoshauri halafu nitakuja na mrejesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo nilipobold….. sidhani kama ni jambo la kukutia wasiwasi… sababu mahusiano lazima yaanzie mahali, na hatujui yataelekea wapi….

Kikubwa kama umempenda na we mpambanie. Usikae tu kinyonge….wanawake tunapenda kupendwa na kuongozwa. Tusipoongozwa tunakinai haraka.

Man up!
 
Kwanza ujue humu unaongea na watu tofauti tofauti. Wamo vijana,wastaarabu na wah*****.

Kama upo serious uje inbox nikupe akili
 
Nashukuru kwa kunitia moyo mkuu.

Hapo kwenye wanawake kupenda kuongozwa, I second you. Kuna siku aliniambia kinachomfanya anipende zaidi ni kwasababu mimi ni 'problem(s) solver', yaani nyakati zote akiwa hana majibu ya changamoto zake akani-consult, huwa namshauri vizuri kwasababu ushauri ninaompaga huwa unamletea matokeo chanya, nadhani hii ni sawa na kusema namuongoza vizuri.

Hayo mengine uliyonishauri nitayafanyia kazi mkuu. Asante.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume unataka nn sasa ukiombwa pesa ulalame ukipewa pesa ww unalalama sa unataka nn tumia nafasi yako na mda wako ulonao kwa sasa utajuta ukiipoteza nafas iyo
 
Labda ni manzi mwarabu Mkuu
 
Wengine mna bahati sana, jitahidi kuitumia vizuri. Kumbuka kuna wanawake wengine hawana tamaa ya pesa ya mtu.

Jaribu kumuuliza kama alishapewa talaka na huyo mumewe.
 
Wengine mna bahati sana, jitahidi kuitumia vizuri. Kumbuka kuna wanawake wengine hawana tamaa ya pesa ya mtu.

Jaribu kumuuliza kama alishapewa talaka na huyo mumewe.
Talaka hawajapeana mkuu. Naweza kusema baada ya kugombana wakatengana. Hawakupeana talaka.

Sijamkatia tamaa bado. Muda utaamua mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…