Iko hivi,
Huu mkoa niliopo kuna dogo mmoja wa bodaboda huwa namuagiza vitu nikipata dharura, tumezoeana sana. Hata akipata shida ndogondogo sitosita kumsaidia.
Sasa siku moja nilimualika kwangu aje tupate chakula cha mchana. Kwenye maongezi akaniuliza, "Bro hivi huna mtoto?". Nikamjibu sina. Akauliza tena, "Mke je?". Nikamwambia sijao. Akaniuliza, "kwanini?". Na mimi nikamuuliza, "Sasa nitamuoa nani?". Akasema bro hukosi wa kuoa labda kama hujaamua tu. Akaniambia kuna dada anamfahamu anafaa kuwa mke. Kweli akanilengesha kwake.
Siku moja nikaenda kwa huyo dada. She is 28 years, ana mini-supermarket kubwa tu, lakini pia ni wakala ya M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa na CRDB. Nikashtuka kidogo kwa namna alivyo stable kiuchumi katika umri wake. Mwanzoni nikajua ni mwajiriwa, baadaye ndio nikagundua vyote ni mali yake.
Basi tukazoeana. Nikawa mteja wake mzuri tu. After a while tukawa wapenzi. Nikaanza kumdadisi, ndio nikajua umri wake. Pia akanieleza kwamba alishafunga ndoa, akazaa na mumewe wakaachana, so ana mtoto mmoja wa form one. Hakutaka tena kumzungumzia huyo mtalaka wake.
Kinachonishangaza ni hiki. Nisipomtafuta halalamiki wala hanitafuti. Nikizidiwa nikamcheki anakuja kwangu nalala nae. Akizidiwa ananicheki, naenda kwake kumuhudumia. Hajawahi kuniomba hela hata siku moja! Nikiwa na shida na hela ndogondogo kwa dharura ananitumia kwenye simu na hanidai, unakuta najishtukia mwenyewe ndio namlipa.
Kuna siku lock ya lango kuu la chuma la kuingia dukani kwake lilikataa kufunguka akaniomba nimtafutie fundi welding, nikamtuma fundi aende ila asichukue hela nitamlipa mimi. Nikaenda dukani wakati fundi anaendelea na kazi. Alipomaliza ile jioni nampigia fundi aniambie gharama, fundi ananiambia dada kashamlipa, nikamwambia kamrudishie pesa yake, dada kagoma kuipokea!
Juzi Ijumaa akaniomba nikae dukani kwake aende msikitini, nikakubali ila nikamwambia sitauza kitu, so wateja wakawa wakija nawaambia ametoka. Pembeni ya kiti chake akaacha 'safe' wazi, nikaifungua nikakuta miburungutu ya hela, nikaifunga nikanyamaza.
Leo ni siku ya 4 tangu niuze gari yangu ndogo, lengo ni kuongeza hela ninunue ingine, asubuhi kanipigia anasema kwasababu yeye anashinda dukani basi naweza kutumia gari yake kwa muda ili nisipate shida, nimeogopa nikaona huu ni mtego, nikamwambia asante nikamchomolea.
Sasa wakuu nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke! Ni kwamba ameyachoka mapenzi au nini nini hiki! Amejenga nyumba yake ya vyumba 2 na sebule, majuzi kanunua kiwanja kingine kikubwa mji mpya na ameshapeleka mchanga, kokoto, mawe na kapiga uzio.
Hebu tusaidiane wajameni, usije ukawa ni mtego huu, pengine ana sponsor naweza kujikuta naishia pabaya. Kiukweli sijawahi kuwa suspicious hata siku moja kwamba ana mahusiano mengine. Simu yake yuko free nayo sana, ndio anazidi kunichanganya!
Nje ya mada:
Pamoja na miaka yangu 11 humu JF, nashindwa kuona notifications mpya, ni wiki sasa inakatika, sijui nimebonyeza wapi, wajuvi mnisaidie.
Asanteni.
Sent using
Jamii Forums mobile app