Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Mama Miaka 28 ana mtoto ambaye yupo form one.

Tafuta umri wa mama alio beba mimba.

Je, tukifanya 28-14 =14

Kwahiyo alibeba mimba na miaka 14 siyo.

Au honi hapa utakua umetudanganya sana mkuu,

Au ndugu zangu ni mimi sijamuelewa mtoa mada?


Jitajidi ukienda kulala kwake uwe na roho ya spare
 
Mkuu umezungumza kwa busara ya hali ya juu.

Ila siwezi kufanya haraka hadi nijiridhishe kuhusu usalama wangu kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujaizoea pesa na hujakulia kwenye pesa, pesa itakutisha, kwanza ni mkoa Gani huo na wilaya ipi?
 
Kamata mtoto huyo unaogopa kupiga mtungo
 
Kwenye kutokulala kwake tena nimelichukua na nitalizingatia.

Kuhusu kuachana na mumewe kwa taratibu za kimahakama nimeshamuhoji, hawakufanya hivyo ila anajaribu kuniaminisha kwamba anamchukia sana huyo mwanaume na kamwe hawezi kumrudia, anaishia hapo. Hamtaji jina, kazi yake wala chanzo cha kuachana.

Ni kweli ni vizuri nimtumie huyu bodaboda kuujua ukweli kwasababu huyu dogo wa boda anamuita huyo dada "mama", na huyo dada anamuita "mwanangu", so wamezoeana sana, nitalifanyia kazi.

Asante kwa ushauri mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, umezungumza vizuri sana na nadhani hauko mbali na ukweli.

Huyo mtalaka wake atakua alimpiga tukio la kihistoria kwasababu hataki kabisa kumzungumzia, anachofanya ni kuniaminisha kwamba kamwe hawezi kurudiana nae. Hamtaji jina, kabila, kazi wala sababu ya kuachana nae. Ukianzisha hiyo mada anakuwa mwekundu. Pengine uko sahihi kwamba sitakiwi kumkumbusha machungu yake ya zamani.

Kuhusu kumtumia huyu bodaboda pia uko sahihi, kwasababu huyu dogo anamuita "mama" na huyu bidada anamuita "mwanangu", so naona huyo dogo yuko kwenye nafasi nzuri ya kunisaidia kuujua ukweli.

Asante mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamata mtoto huyo unaogopa kupiga mtungo
Siogopi mkuu ila nahofia usalama wangu [emoji28]. Dunia imebadilika sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kwa sehemu.

Two things are involved here. Inawezekana kanidanganya umri au alipata mimba za utotoni, jamaa akaja kumuoa baadaye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sioni tatizo lolote....lakini siwezi nikamruhusu mwanangu au mwana wa rafiki yangu akaoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto au aliyewahi kuolewa na akaachika. Hata binti kuolewa na mwanaume aliyeacha mke, ni lazima kuwa makini sana. Pengine mwanamke aliamua kukimbia mateso.
Never! hata kama ana qualities zote
 
sioni tatizo lolote....lakini siwezi nikamruhusu mwanangu au mwana wa rafiki yangu akaoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto au aliyewahi kuolewa na akaachika.
Never! hata kama ni qualities zote
Kwanini mkuu? Sio kwamba umefanya fallacy of generalization? Manake wapo wanawake wenye watoto na wameachika ila ni wife material bado.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…