Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Ikiwa wewe unaamini katika mapenzi na mahaba, hapo sio mahala sahihi.
Huyo dada ameyakinai mapenzi, huenda alitendwa sana.

Mkioana kwake haitakuwa vigumu kukwambia muachane mkitofautiana kidogo.
Abaki kama rafiki wa kukatana kiu lakini kwa habari ya mke hapo ni chaka
Nadhani uko sahihi mkuu.

Lakini je, kwa maoni yako, siwezi nikambadilisha akayaamini tena mapenzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama Miaka 28 ana mtoto ambaye yupo form one.

Tafuta umri wa mama alio beba mimba.

Je, tukifanya 28-14 =14

Kwahiyo alibeba mimba na miaka 14 siyo.

Au honi hapa utakua umetudanganya sana mkuu
Kwanini uhitimishe kuwa amedanganya ikiwa biologically binti wa umri huo anaweza kushika mimba? Huoni kuwa kimantiki wewe ndio una shida ya uelewa mdogo?

Mimi mdogo wangu alipewa mimba akiwa form one ana miaka 13, tena aliyempa mimba ni mwanafunzi mwenzie aliyekua na miaka 17 yuko form 3.

sasa hivi huyo dogo yuko form 2 na mwezi uliopita Amefikisha miaka 14. Mama yake sasa hivi yuko mzumbe anafanya masters.
 
Iko hivi,

Huu mkoa niliopo kuna dogo mmoja wa bodaboda huwa namuagiza vitu nikipata dharura, tumezoeana sana. Hata akipata shida ndogondogo sitosita kumsaidia.

Sasa siku moja nilimualika kwangu aje tupate chakula cha mchana. Kwenye maongezi akaniuliza, "Bro hivi huna mtoto?". Nikamjibu sina. Akauliza tena, "Mke je?". Nikamwambia sijao. Akaniuliza, "kwanini?". Na mimi nikamuuliza, "Sasa nitamuoa nani?". Akasema bro hukosi wa kuoa labda kama hujaamua tu. Akaniambia kuna dada anamfahamu anafaa kuwa mke. Kweli akanilengesha kwake.

Siku moja nikaenda kwa huyo dada. She is 28 years, ana mini-supermarket kubwa tu, lakini pia ni wakala wa M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa na CRDB. Nikashtuka kidogo kwa namna alivyo stable kiuchumi katika umri wake. Mwanzoni nikajua ni mwajiriwa, baadaye ndio nikagundua vyote ni mali yake.

Basi tukazoeana. Nikawa mteja wake mzuri tu. After a while tukawa wapenzi. Nikaanza kumdadisi, ndio nikajua umri wake. Pia akanieleza kwamba alishafunga ndoa, akazaa na mumewe wakaachana, so ana mtoto mmoja wa form one. Hakutaka tena kumzungumzia huyo mtalaka wake.

Kinachonishangaza ni hiki. Nisipomtafuta halalamiki wala hanitafuti. Nikizidiwa nikamcheki anakuja kwangu nalala nae. Akizidiwa ananicheki, naenda kwake kumuhudumia. Hajawahi kuniomba hela hata siku moja! Nikiwa na shida na hela ndogondogo kwa dharura ananitumia kwenye simu na hanidai, unakuta najishtukia mwenyewe ndio namlipa.

Kuna siku lock ya lango kuu la chuma la kuingia dukani kwake lilikataa kufunguka akaniomba nimtafutie fundi welding, nikamtuma fundi aende ila asichukue hela nitamlipa mimi. Nikaenda dukani wakati fundi anaendelea na kazi. Alipomaliza ile jioni nampigia fundi aniambie gharama, fundi ananiambia dada kashamlipa, nikamwambia kamrudishie pesa yake, dada kagoma kuipokea!

Juzi Ijumaa akaniomba nikae dukani kwake aende msikitini, nikakubali ila nikamwambia sitauza kitu, so wateja wakawa wakija nawaambia ametoka. Pembeni ya kiti chake akaacha 'safe' wazi, nikaifungua nikakuta miburungutu ya hela, nikaifunga nikanyamaza.

Leo ni siku ya 4 tangu niuze gari yangu ndogo, lengo ni kuongeza hela ninunue ingine, asubuhi kanipigia anasema kwasababu yeye anashinda dukani basi naweza kutumia gari yake kwa muda ili nisipate shida, nimeogopa nikaona huu ni mtego, nikamwambia asante nikamchomolea.

Sasa wakuu nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke! Ni kwamba ameyachoka mapenzi au nini nini hiki! Amejenga nyumba yake ya vyumba 2 na sebule, majuzi kanunua kiwanja kingine kikubwa mji mpya na ameshapeleka mchanga, kokoto, mawe na kapiga uzio.

Hebu tusaidiane wajameni, usije ukawa ni mtego huu, pengine ana sponsor naweza kujikuta naishia pabaya. Kiukweli sijawahi kuwa suspicious hata siku moja kwamba ana mahusiano mengine. Simu yake yuko free nayo sana, ndio anazidi kunichanganya!

Nje ya mada:
Pamoja na miaka yangu 11 humu JF, nashindwa kuona notifications mpya, ni wiki sasa inakatika, sijui nimebonyeza wapi, wajuvi mnisaidie.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
endeleea watakuokota ukiwa kwenye deadly zone mtaroni
 
Mama Miaka 28 ana mtoto ambaye yupo form one.

Tafuta umri wa mama alio beba mimba.

Je, tukifanya 28-14 =14

Kwahiyo alibeba mimba na miaka 14 siyo.

Au honi hapa utakua umetudanganya sana mkuu,

Au ndugu zangu ni mimi sijamuelewa mtoa mada?

Jitajidi ukienda kulala kwake uwe na roho ya spare
inawezekana maisha wanawake wanapitia mengi ukute alibakwa akiwa na miaka 13/14
 
Kwani huyo dogo aliekuunganishia ukimuuliza kuhusu historia ya huyo mwanamke anasemaje mkuu?
 
Iko hivi,

Huu mkoa niliopo kuna dogo mmoja wa bodaboda huwa namuagiza vitu nikipata dharura, tumezoeana sana. Hata akipata shida ndogondogo sitosita kumsaidia.

Sasa siku moja nilimualika kwangu aje tupate chakula cha mchana. Kwenye maongezi akaniuliza, "Bro hivi huna mtoto?". Nikamjibu sina. Akauliza tena, "Mke je?". Nikamwambia sijao. Akaniuliza, "kwanini?". Na mimi nikamuuliza, "Sasa nitamuoa nani?". Akasema bro hukosi wa kuoa labda kama hujaamua tu. Akaniambia kuna dada anamfahamu anafaa kuwa mke. Kweli akanilengesha kwake.

Siku moja nikaenda kwa huyo dada. She is 28 years, ana mini-supermarket kubwa tu, lakini pia ni wakala wa M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa na CRDB. Nikashtuka kidogo kwa namna alivyo stable kiuchumi katika umri wake. Mwanzoni nikajua ni mwajiriwa, baadaye ndio nikagundua vyote ni mali yake.

Basi tukazoeana. Nikawa mteja wake mzuri tu. After a while tukawa wapenzi. Nikaanza kumdadisi, ndio nikajua umri wake. Pia akanieleza kwamba alishafunga ndoa, akazaa na mumewe wakaachana, so ana mtoto mmoja wa form one. Hakutaka tena kumzungumzia huyo mtalaka wake.

Kinachonishangaza ni hiki. Nisipomtafuta halalamiki wala hanitafuti. Nikizidiwa nikamcheki anakuja kwangu nalala nae. Akizidiwa ananicheki, naenda kwake kumuhudumia. Hajawahi kuniomba hela hata siku moja! Nikiwa na shida na hela ndogondogo kwa dharura ananitumia kwenye simu na hanidai, unakuta najishtukia mwenyewe ndio namlipa.

Kuna siku lock ya lango kuu la chuma la kuingia dukani kwake lilikataa kufunguka akaniomba nimtafutie fundi welding, nikamtuma fundi aende ila asichukue hela nitamlipa mimi. Nikaenda dukani wakati fundi anaendelea na kazi. Alipomaliza ile jioni nampigia fundi aniambie gharama, fundi ananiambia dada kashamlipa, nikamwambia kamrudishie pesa yake, dada kagoma kuipokea!

Juzi Ijumaa akaniomba nikae dukani kwake aende msikitini, nikakubali ila nikamwambia sitauza kitu, so wateja wakawa wakija nawaambia ametoka. Pembeni ya kiti chake akaacha 'safe' wazi, nikaifungua nikakuta miburungutu ya hela, nikaifunga nikanyamaza.

Leo ni siku ya 4 tangu niuze gari yangu ndogo, lengo ni kuongeza hela ninunue ingine, asubuhi kanipigia anasema kwasababu yeye anashinda dukani basi naweza kutumia gari yake kwa muda ili nisipate shida, nimeogopa nikaona huu ni mtego, nikamwambia asante nikamchomolea.

Sasa wakuu nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke! Ni kwamba ameyachoka mapenzi au nini nini hiki! Amejenga nyumba yake ya vyumba 2 na sebule, majuzi kanunua kiwanja kingine kikubwa mji mpya na ameshapeleka mchanga, kokoto, mawe na kapiga uzio.

Hebu tusaidiane wajameni, usije ukawa ni mtego huu, pengine ana sponsor naweza kujikuta naishia pabaya. Kiukweli sijawahi kuwa suspicious hata siku moja kwamba ana mahusiano mengine. Simu yake yuko free nayo sana, ndio anazidi kunichanganya!

Nje ya mada:
Pamoja na miaka yangu 11 humu JF, nashindwa kuona notifications mpya, ni wiki sasa inakatika, sijui nimebonyeza wapi, wajuvi mnisaidie.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
1 Usirudie kwenda kulala kwa huyo dada muwe mnakutana lodge na hapo unapoishi hama asipajue kabisa.
2 Usichukue pesa yake yoyote, ukiwa na shida waombe watu ulokua ukiwaomba zamani.
 
Kwanini uhitimishe kuwa amedanganya ikiwa biologically binti wa umri huo anaweza kushika mimba? Huoni kuwa kimantiki wewe ndio una shida ya uelewa mdogo?

Mimi mdogo wangu alipewa mimba akiwa form one ana miaka 13, tena aliyempa mimba ni mwanafunzi mwenzie aliyekua na miaka 17 yuko form 3.

sasa hivi huyo dogo yuko form 2 na mwezi uliopita Amefikisha miaka 14. Mama yake sasa hivi yuko mzumbe anafanya masters.
Asante sana mkuu kwa back up hii. Kuna watu humu ndani sijui wanatumia akili zao kufanyia nini! Yani nyakati zote mtu akishare kisa chake humu ndani wao wanadhani ni hadithi za kutunga! Mimi nina mwaka wa 11 humu JF na sidhani kama naweza kufanya utoto kama watoto wengi wa 2000 ambao wameingia humu juzijuzi.

Nashukuru kwamba JF bado ina watu wa sampuli yako. Kongole mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom